Ni Lini Utaacha Kuutumikia Utumwa Wa Hofu Usiokuwa Na Manufaa?...
Hivi unafahamu kwamba zaidi ya 80% ya watu duniani kote wanaishi maisha yaliyojaa hofu, wasiwasi pamoja na mashaka kiasi kwamba wanakosa kabisa hata uthubutu wa kutoka pale walipo na kwenda hatua nyingine ya juu zaidi?
Huenda hata wewe ukawa ni miongoni mwa watu hao ambao pasipo kujua wamejikuta wakiipa hofu mamlaka ya kuendesha na kutawala maisha yao, kuliko hata wao wenyewe walivyojipa mamlaka na ukuu wa kutawala na kuongoza maisha yao.
Ukweli ni kwamba hakuna uhalisia wa kitu ambacho huwa kinaogopwa, bali nafsi ya mtu kupitia fikra zake ndizo humuweka mashakani.
Na, ifahamike kwamba kila kitu katika maisha ya mwanadamu huanzia ndani ya nafsi yake kwanza ndipo sasa hujidhihirisha nje ya maisha yake.
Hii inamaanisha kwamba hata hofu hutengenezwa…
Na, uhalisia wa jambo hili unajidhihirisha kwenye kanuni ya uakisi wa mambo ambayo inasema: “ulimwengu wako wa nje ni uakisi wa ulimwengu wako wa ndani” hii inaamanisha kwamba vile unavyotengeneza hofu ndani ya nafsi yako ndivyo utakavyoonesha mwitikio wa hofu katika maisha yako...
Labda huenda ukawa unajiuliza hofu inatokana na nini?
…usijali ndani ya muda mfupi unaenda kufahamu chanzo cha hofu…
Unatakiwa kujua kwamba hofu hutokea pale ambapo kifikra mtu kaona mwisho wa mbaya wa jambo Fulani hata kama jambo hilo halitakuwa kama vile yeye alivyoliona.
Kutokana na hilo hujikuta akianza kupatwa na kimuhemuhe kuhusu jambo hilo, hali ambayo hummaliza kabisa na kumfanya akose nguvu na uthubutu katika utekelezaji wa jambo hilo na hii ni kwa sababu kashaona mwisho wake utakuwa mbaya…
Na, huo ndiyo huwa ndiyo huwa mwanzo wa hofu, kwamba fikra za mwanadamu mwenyewe ni mbegu ambazo huzaa hofu…
Kinachosikitisha zaidi ni kwamba mtu mwenye hofu huwa anahofia fikra zake mwenyewe na si kitu kingine, kwani ni yeye mwenyewe kupitia fikra zake ndiyo katengeneza hofu hizo.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba mtu mwenye hofu pasipo kujua hujikuta akijiadhibu mwenyewe kwa kutumia fikra zake vibaya na kujitengenezea mlima, ambao humtatiza na kumfanya ashindwe kuupanda ili avuke ng’ambo ya pili…
Kwa mantiki hiyo tatizo huwa siyo kile kinachoogopwa bali tatizo huwa ni fikra hasi zilizotengenezwa juu ya kile kinachoogopwa…
Unachotakiwa kujua ni kwamba, fikra hasi huvuta matukio hasi maishani, ikiwa fikra chanya huvuta matukio chanya.
Hivyo basi endapo utakuwa na fikra hasi juu ya jambo Fulani kwa kuliona kama halitafanikiwa hutapata ujasiri wa kulikabili jambo hilo bali utaanza kulihofia…
Kwa mantiki hiyo kuna wakati mtu hutakiwi kupambana na hofu bali inatakiwa upambane na fikrza zako mwenyewe, kwa sababu hizo fikra ndizo zimepelekea hofu maishani mwako.
Ukienda kuchunguza kuanzia ulimwengu wa michezo, siasa, sayansi, elimu, dini pamoja na uchumi utagundua kwamba kuna watu ilitakiwa wawe wameshafanya mambo makubwa sana na wawe wameshafika mbali sana kimaisha lakini kutokana na kuendekeza hofu wamejikuta wakishindwa kupiga hatua…
Kwa mfano kuna watu watu wanahofia juu ya vifo vyao. Kuna watu wanahofia kuhusu kazi zao, kuna watu wanahofia kuhusu muda wa kustaafu ukifika, kuna watu wanahofia kuhusu umaskini, kuna watu wanahofia kuhusu ndoa zao, kuna watu wana hofu kuhusu mahusiano yao, kuna watu wana hofu kuhusu kesho zao, kuna watu wana hofu kuhusu magonjwa n.k
Na, ifahamike kwamba kuhofu huwa hakutatui tatizo zaidi ya kulikuza na kulifanya liende hatua mbaya zaidi hasa ukihusisha na jinsi vile siku zinavyozidi kwenda mbele…
My friend huenda hata wewe upo kwenye ulimwengu wa hofu, na huenda ukawa una hofu juu ya maisha yako.
Je, unahofia kuhusu nini? Na kama unachohofia chenyewe hukijui kwanini uwe na hofu?
Je, utahofu mpaka lini? Au unataka kumaanisha kwamba utabaki na hofu maisha yako yote?..
My friend ni dhahiri umeona ni jinsi gani wewe mwenyewe ulivyojiweka hatarini kwa kupitia fikra zako hasi, huu ni wakati wa kubadili fikra zako. Kumbuka usipobadili fikra zako hakuna chochote kile kitakachobadilika maishani mwako.
Badili fikra zako, badili maisha yako!
Fahamu Kuhusu Aina Za Hofu...
Zipo aina nyingi sana za hofu, lakini kwa kutumia kigezo cha asili ya hofu tutapata aina mbili za hofu. na, Aina hizo ni kama inavyodokezwa hapa chini:-
1. Hofu Ya Kuzaliwa Nayo…
Hii ni aina ya hofu ambayo kila mtu anazaliwa nayo. Mungu alituumbia aina hii ya hofu ili iweze kutukinga dhidi ya hatari.
Kwa mfano tufanye uko barabarani unatembea ukasikia mlio wa honi ukaamua kupisha, maana yake umepisha kwa kuhofia kuhatarisha uhai wako pamoja na usalama wako.
Hii ni hofu ambayo umeumbiwa ili ikuweke salama pale kunapotokea hatari Fulani.
Sasa aina nyingine za hofu zitaingia kwenye aina hii moja ya hofu kama itakavyooneshwa kwenye makala ijayo!
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri...
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No +255744284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment