Nifanye Nini Ili Nivute Bahati Maishani Mwangu?


Mithali 22:29
“Je, wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme, hatasimama mbele ya wasio na cheo”

Neno liko wazi kabisa kwamba bidii ndiyo mbegu  sahihi ya bahati ni siyo kukaa tu huku ukingojea upepo! 
Kwa mantiki hiyo ukiona mtu amesimama mbele ya wafalme, watu wakuu na wenye vyeo pamoja na kufanya mambo makubwa haimaanishi kwamba ana bahati bali bidii yake ndiyo imemstahilisha!

Najua unajiuliza ninaweza nikafanya nini ili niweze kuvuta bahati maishani mwangu?
...Usijali ndani ya muda mfupi ujao unaenda kugundua siri kubwa sana zinazoenda kubadilisha kabisa maisha yako...

Je unataka kuvuta bahati maisha yako? Kama jibu ni ndiyo huna budi kufanya yafuatayo:

1. Pata Maana Kamili Ya Bahati...
Katika hali ya kawaida huwezi ukavuta kitu katika maisha yako ambacho hata wewe mwenyewe hukijui vizuri. 

Kwako wewe bahati ni nini? Je, ni kuokota nyumba? Je, ni kuokota gari? Je, ni kuokota kiasi kingi cha fedha? Je, ni kupata kazi nzuri? Je, ni kupata mchumba? Je, ni kuoa au kuolewa? Je, ni kufanikiwa kiuchumi?
Je, kwako wewe bahati ni nini? Ikitokea mtu amekuuliza ni jambo gani ambalo ukilipata litakuwa kama ni bahati kubwa sana kwako utamueleza jambo gani?

Ndugu ni lazima uweze kujua kwako bahati ni nini, ili unapoitafuta uweze kujua unachokitafuta ni nini na ufanye nini ili uweze kukivuta. 

Huenda tayari ushabahatika na unaishi kwenye bahati yako, ila kwa sababu hujui kwako bahati ni nini unajiona bado hujabahatika...

Friend pata maana kamili juu ya bahati kwako ni nini ili siku ukiipata ujue kwamba lile tukio nililokuwa nalitafuta kwa muda mrefu nimelipata tayari.
Kwani huwezi ukajua kuwa umepata kitu ambacho hukijui vizuri. Hivyo ni muhimu ukapata maana kamili ya bahati ili siku ikitokea ujue kwamba sasa naanza kuiishi bahati yangu.

2. Eleza Kwa Uwazi Hatima Ya Bahati Yako...
Awali nilidokeza kwamba bahati hutengenezwa, na kama bahati hutengenezwa basi wewe hapo ndiyo una wajibu wa kuchagua hatima ya bahati yako unayoitaka...
Je, kama unataka ubahatike kwenye eneo la kiuchumi ni kiasi gani cha pesa ambacho endapo utakimiliki ndipo utasema umebahatika kuishi maisha ya ndoto yako? 

Na, kama ni kazi ni aina gani ya kazi ambayo ukiifanya utasema hii ndiyo kazi ya bahati yangu?
Kwa mfano kwangu mimi nilikuwa napenda sana kazi ya ushauri.
Kwamba kazi ya ushauri ndiyo ilikuwa kama hatima ya bahati yangu, na endapo ningefanya kazi kama mshauri ningejiona ni miongoni mwa watu wenye bahati kubwa sana hapa duniani. 

Sikuishia hapo nikatengeneza mazingira ya kuandaa bahati yangu mpaka sasa nashauri watu kupitia uandishi, ana kwa ana pamoja na njia ya mtandao.
Kumbuka nilianza kufafanua kwangu bahati ni nini, na sikuishia hapo nikatengeneza hatima ya bahati yangu na sasa naiishi bahati yangu...
Je, kwako wewe ukiulizwa juu ya hatima ya bahati yako utaeleza nini? 
Hicho utakachoeleza ndicho kitakuwa maana ya bahati kwako. 

3. Weka Mkakati Utakaopelekea Bahati Yako Ije Katika Maisha Yako...
Tufanye umeshajua hatima ya bahati yako itakuwa nini! Unatakiwa kujua kwamba kuifahamu hatima ya bahati siyo kigezo cha wewe kuweza kuifikia.

Kwani hakuna bahati ambayo hujitengeneza yenyewe, bali wewe ndiyo una wajibu wa kuweka mikakati itakayopelekea bahati yako iweze kutokea.
Unatakiwa kujua kwamba mkakati utakaoweka ni muhimu kuliko bahati yenyewe, kwani ni kupitia mkakati utakaoweka ndipo utakapoweza kuvuta bahati katika maisha yako.

Kwa mfano mara baada ya kujua kwamba nitajiona ni mwenye bahati sana endapo nitakuwa mashauri huku nikifahamika na watu wengi nikaweka mkakati wa kusoma vitabu vya saikolojia, vya dini, vya uchumi pamoja na vitabu vya maendeleo binafsi.
Mara baada ya kusoma vimenisaidia niweze kupata maarifa ambayo kupitia hayo mpaka leo hii naiishi kazi ya bahati yangu.
Je umeandaa mkakati gani wa kuhakikisha unaivuta bahati katika maisha yako?

Friend ni lazima uweke mkakati kwani ni kupitia mkakati wako ndipo utakapoweza kuvuta bahati maishani mwako.

4. Chukua Hatua Kwenye Mkakati Yako...
Kuishia kuweka mkakati pasipo kuchukua hatua hatua ni kazi bure.
Unatakiwa kujua kwamba hatua moja iliyochukuliwa ina thamani zaidi ya mikakati 1000 ambayo haijachukuliwa hatua yoyote ile.

Ukiweka mikakati wa kuifikia bahati yako ni lazima uchukue hatua kwenye mikakati yako.
Kwa mfano ningeishia tu kuweka mkakati wa kusoma vitabu pasipo kusoma vitabu hivyo nisingeweza kuishi kazi ya bahati yangu.

Hii ni sawa na kusema lazima uchukue hatua kwenye mikakati yako kwa kupitia kufanya kwa vitendo, kile ulichokikusudia kukifanikisha kwenye bahati yako.

Ahsante sana kuwa mwanafamilia wa masomo haya mazuri!
Mwendelezo Wa Somo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e, Mwl, Mwandishi Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No +255744284339 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...