Njia Kuu Tatu Rahisi Za Kubadili Mitizamo Yako Juu Ya Namna Unavyojiona...
4. Jione Sawa Na Vile Muumba Wako Akuonavyo...
Vile Muumba anavyokuona huenda ikawa ni tofauti kabisa na wewe unavyojiona!
Kwamba wewe unajiona kwa namna hii ikiwa Mungu anakuona kwa namna nyingine!
Kwa mfano unaweza ukajikuta unajiona huwezi, hustahili na si kitu, lakini Mungu akawa anakuona kuwa unaweza, unastahili na wewe ni mtu wa thamani sana kuwahi kutokea hapa duniani!
Na ifahamike kwamba, Mungu wetu ni Mungu wa yawezekanayo na si Mungu wa wasiyowezekana, hivyo basi endapo utajiona kama yeye akuonavyo kwako wewe kila jambo litawezekana.
Hebu tuangalie maandiko matakatifu yanachosema kuhusu vile Mungu atuonavyo:
"Ee bwana umenichunguza na kunijua, Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu;
Umelifahamu wazo langu tokea mbali". Zaburi 139
"Kabla sijakuumba katika tumbo la mama yako nalikujua na kabla hujatoka tumboni nalikutakasa"… “Yer 1:5”.
Friend, umeona Sasa? Mungu anakujua wewe vizuri kuliko hata wewe mwenyewe unavyojijua!
Unatakiwa kujua kwamba Mungu anaujua mwanzo na mwisho wako, lakini ili uuone mwanzo na mwisho wako ni lazima umfanye yeye awe kama kioo kwako!
Kwamba ni lazima ujitizamie kwake kwanza, na kile utakachokiona kukuhusu ndivyo yeye anavyokuona wewe!
Mpenzi msomaji, unatakiwa kujua kwamba "moyo wa mtu huifikiri njia yake, bali Bwana huziongoza hatua zake" mithali 16:9
Kinachomaanishwa hapa ni kwamba, Moyo wa Mtu ni namna wewe unavyiojiona na kujifikiria, lakini kumbe yupo Mungu anayeingoza hatua zako!
Mungu amekuwa akikuongoza katika maisha yako yote pasipo hata wewe mwenyewe kujua kwamba unaongozwa.
Kwa mantiki hiyo huna budi kujiona sawa na yeye akuonavyo ili uifanikishe safari yako!
Na, ndiyo maana Isaya 48:17 Neno la BWANA linasema “BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israel, asema hivi, Mimi ni BWANA, MUNGU wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongazaye kwa njia ikupasayo kuifuata.
Friend unatakiwa kujua kwamba mawazo yetu na mitizamo yetu juu ya namna tujionavyo si kitu, kwani huwa na ukomo, kwamba unaweza ukaifuata na usifike popote pale kwa sababu hujajiona kama Mungu anavyokuona!
Ushuhuda wake upo kwenye Isaya 55:8-9, Neno la Mungu linasema: “maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zangu zenu si zangu; asema BWANA, kwa maana kama mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu ziko juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu”
Hata hivyo, unaweza ukajiona wewe pekee unaweza na hivyo ukaamua kufuata njia zako ukaishia mautini...
Na ndiyo maana mithali 14:12 neno la BWANA linasema, “iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake ni njia za mauti”.
Unachotakiwa kujifunza hapa ni kwamba huenda ulitumainia njia zako zinazotokana na namna unavyojiona ambazo mwisho wa siku zimekupeleka kwenye mauti na siye kule ulikopaswa uende, na ndiyo maana ninakusihi uanze kujiona upya kama vile Mungu akuonavyo!
Friend jione kadri Mungu anavyokuona! Mfanye Mungu awe kama kioo kwako!
Kumbuka Mungu ametuonesha sisi ni nani na anatuonaje kupitia Neno lake!
Kwa minajiri hiyo, endapo utakuwa unasoma Neno lake utaanza kujijua wewe ni nani!
Unatakiwa kujua kwamba Mungu husema nasi kupitia neno lake, hii ni sawa na kusema ukilipokea Neno lake ni sawa na umempokea Mungu, kwa maana Mungu mwenyewe ni Neno. Yohana 1:1
Na, ukishampokea Mungu utajijua wewe ni nani!
Friend badili mitizamo yako kwa kumpa Mungu nafasi ili abadili maisha yako!
Yeremia 33:3 "niite, nami, nitakuitikia, nami nitakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua"
5. Futa Picha Zote Mbaya Zilizopo Akilini Mwako...
Huwezi ukajiona katika ukuu ilihali kichwani mwako unajiona ukiwa u mdhaifu na mnyonge, kwa mantiki hiyo huna budi kufuta picha zote mbaya unazoziona akilini mwako!
Na, endapo utaweza kufanya hivyo, utatakiwa uweze kutengeneza picha nzuri akilini mwako zinazokuonesha wewe katika ubora wako!
Kumbuka kile unachokiona ndicho unachokipata, hii inamaanisha kwamba yule unayemuona kupitia picha ulizozitengeneza akilini ndiye utakayekuwa! Kwani "yule mtu unayemuona ndiye unayekuwa"
Hata hivyo kanuni ya msawazo wa akili inasema kwamba “kile unachokipata kwenye maisha yako ni uakisi wa kile unachokitengeneza akilini mwako”
Hata hivyo ukishauona mwisho wako utapata utayari wa kuufikia mwisho huo!
Hii inamaanisha kwamba ukishajiona katika ubora wako yule uliyemuona ndiye utakayemfikia.
Na utaanza kujiona hivyo saa hiyohiyo, na ndiyo maana hapa duniani kuna watu ambao wanaziishi kesho zao leo!
Hata Mimi ni miongoni mwa watu hao, siishi leo bali naiishi kesho yangu kwani picha za kesho yangu zipo akilini mwangu!
Hivyo basi, kama ulikuwa ni mtu ambaye umejitengenezea picha mbaya akilini mwako, huna budi kuzifuta picha hizo na kujaza pichaa nzuri zikikuonesha wewe katika ubora wako.
Futa picha mbaya kuhusu wewe akilini mwako, then tengeneza picha nzuri kuhusu wewe, huo ni mwanzo mzuri wa kubadili maisha yako!
6. Badili Matarajio Yako...
Kanuni ya matarajio inasema kwamba; “chochote utakachokitarajia kuhusu wewe kwa imani kitakuja kuthibitisha unabii ulioutabiri kuhusu wewe”.
Unachopaswa kujua ni kwamba kile unachokitarajia kupitia kujiona kwako ndicho unachokivuta!
Kwamba ukitarajia matukio mema utayavuta katika maisha yako kwa sababu uliwekea matarajio juu yake!
Sikiliza my friend; unachokitarajia kinapima unachokivuta, unachokivuta kinapima unachokiona, unachokiona kinapima unachokiheshimu, unachokiheshimu kinapima unachokipata katika maisha yako!
Mpenzi huhitaji kingine zaidi ya kubadilisha matarajio yako!
Badilisha matarajio yako na kuyafanya yawe halisi, yawe mazuri na mema, na ndivyo matukio mema yatakavyokujia katika maisha yako!
Na huu ndiyo mwisho wa somo letu! Next week nitakuja na Somo Jipya
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya!
Ndimi Emmanuel Samuel King’ung’e; Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach & Consultant!
Unaweza kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No +255744284329 Au Wasiliana Kupitia Blog Yangu Kwa Kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment