Sahau Kabisa Kubahatika Mpaka Usome Kwanza Hii...


Makala iliyopita ilidokeza hoja nne kuhusu namna gani unaweza ukaivuta Bahati Maishani Mwako!

Leo umeletewa mwendelezo wa somo hili, ungana na wanafamilia wenzako ambao wamekuwa wakifuatilia masomo haya pamoja na kunufaika nayo!

Je unataka uvute bahati ije katika maisha yako?...
Kama jibu lako ni ndiyo basi kuna ujumbe wako mzuri hapaa...

5. Fanya Jambo Litakalopelekea Bahati Yako Kwa Mwendelezo...
Hutakiwi kuwa mtu wa kufanya mambo kwa kudonoa donoa wala kwa ulegevu, bali unatakiwa kila siku ufanye jambo Fulani litakalokusogeza pale ambapo hatima ya bahati yako ilipo! 

Kuna kanuni moja inaitwa kanuni ya mlimbikizano, kanuni hii inasema kwamba “unapata matokeo makubwa kutokana na kufanya mambo madogo kwa mwendelezo ndani ya kipindi cha muda fulani”

Sikiliza my friend, sharti la kupata matokeo makubwa (bahati yako) liko wazi kabisa kwamba, ni lazima ukubali kufanya mambo madogomadogo kwa mwendelezo ndani ya kipindi cha muda Fulani. 

Na endapo hutafanya kwa mwendelezo basi huwezi ukayapata hayo matokeo makubwa (bahati yako). Kwani sharti likivunjwa matokeo yake huwa ni kinyume chake…

Mpenzi unatakiwa kujua kwamba unatakiwa uwe mvumilivu sana kwani kuna wakati utakuwa unafanya baadhi ya mambo kwa mwendelezo, cha ajabu ukawa huoni matokeo ya maana kwenye juhudi zako.
Nipo hapa kukusihi kwamba wewe endelea kufanya kwa mwendelezo tu, kwani kanuni ya mlimbikizano iko inakungojea mwisho wa siku utapata matokeo makubwa kutokana na kile unachokifanya.
The end shall speak, just keep sowing the seeds!

6. Kuwa Tayari Kulipa Gharama Zinazotakiwa...
Tufanye tayari ushapata maana kamili ya bahati kwako, ushaweka na mkakati wa kuifikia, na ulishachukua na hatua za kuvuta bahati hiyo maishani mwako.
Unatakiwa kujua pasipo kujua gharama zitakazohitajika unaweza usiivute bahati katikati ya maisha yako. 

Gharama huwa ni kama kichocheo kitakachokufanya uweze kuifikia bahati yako. Kwani kiwango cha gharama utakacholipa ndicho kitapima kiwango cha bahati utakachovuta maishani mwako… 

Ukweli ni kwamba, kuna baadhi ya fursa zilizobeba bahati yako, ambazo kupatikana kwake ni lazima ukubali kulipa gharama kwanza. 
Na, usipokuwa tayari kulipa gharama hakuna mtu atakayekuja kulipa gharama kwa ajili ya bahati yako!
Yes kuwa tayari kulipa gharama bosi. 
Huenda ukawa unajiuliza ni gharama gani ambayo inazungumziwa hapa, ukweli ni kwamba kuna gharama ya fedha, gharama ya muda, gharama ya kujitoa sadaka pamoja na gharama ya kihisia.

Mpenzi endapo utakuwa tayari kulipa gharama zote hizo ni lazima utatengeneza fursa ya bahati yako na hapo ndipo utakapofanikisha kuivuta bahati katika maisha yako.

7. Weka Mpaka Ukomo Wa Muda Ambao Unataka Uwe Umeifikia Bahati Yako...
Ni muhimu ukaweka muda maalumu ambao unataka uwe umefanikisha kuipata bahati yako.

Unapoweka ukomo wa muda maana yake utakuwa unaweza wa kujipa tathmini ya maendeleo yako juu ya kile ambacho umepanga kukipata, na utajikuta unatumia muda wako vizuri ili uweze kufanya mambo yote yatakayokusaidia uweze kuivuta bahati katika maisha yako.

Unatakiwa kujua kwamba usipoweka ukomo wa muda utashindwa kujipa tathmini, na ukishindwa kujipa tathmini maana yake utashindwa kujisimamia na ukishindwa kujisimamia hutaweza kuipata bahati yako kwa wakati.

Na, ifahamike kwamba endapo hutaweka ukomo wa muda wa kupata bahati yako, utashindwa kuweka ukomo pia katika kusubiri bahati hiyo katika maisha yako.  
Kutokana na kutokuweka ukomo wa muda unaweza ukajikuta ukitumia muda wa maisha yako yote kuisubiri bahati na usiipate mpaka siku unaingizwa kaburini, kwa sababu hukuweka ukomo wa muda juu ya lini hasa unataka uweze kuivuta hiyo bahati katika maisha yako.

8. Pigana Na Vipingamizi Vyote...
Hakuna kitu kizuri ambacho hupatikana kwa urahisi. 
Unatakiwa kujua kwamba kwa kila jambo utakaloazimia kulifanya ni lazima kuna vikwazo huibuka.
Na, endapo hutakuwa na misimamo vikwazo hivyo vitakutoa nje ya mfumo na kukufanya uishie kukata tamaa. 
Kitu kimoja unachotakiwa kujua ni kwamba bahati inatafutwa tena kwa nguvu zote.

Hivyo basi ikitokea kuna vikwazo vimeibuka kwenye utakelezaji wa hatua za kuitafuta wewe pambana navyo.

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya. 

Ndimi Emmanuel Samuel King’ung’e; Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No +255744284329 Au Tembelea Blogu Yangu Kwa Kuandika ekingunge.blogspot.com 

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...