Fahamu Kuhusu Mbinu Ya Pili Ya Kuikabili Hofu...

Hello habari yako rafiki? Ni matumaini yangu u mzima wa afya! 
Karibu kwenye mwendelezo wa somo linaloangazia kuhusu mbinu tisa za kutumia ili uikabili hofu!
Kwa leo umesogeweza mbinu ya pili unayoweza kutumia ili uikabili hofu! 
Ikumbukwe makala iliyopita ilidokeza hoja moja!
Bila kukupotezea muda ngoja nikuoneshe mbinu ya pili unayoweza kutumia ili uikabili hofu...

2. Tumia Conscious Mind Na Subconscious Mind...

Unamiliki akili moja ambayo hufanya kazi kwa kutumia sehemu mbili za akili ambazo ni: conscious mind (akili dhamiri) pamoja na subconscious mind (sehemu ya akili usiyo na mamlaka nayo).

Nini Maana Ya Conscious Mind?
Conscious mind, ni sehemu ya akili ambayo huchukua wazo, taarifa, hisia au dhana ya kitu chochote kile na kisha kukipeleka ubongoni.

Sehemu hii ya akili ndiyo huongoza maisha ya binadamu na hii ni kutokana na sehemu hii ya akili kuwa na uwezo wa kudadisi pamoja na kuchagua vitu mbalimbali kuhusu machaguo ayafanyayo huyo binadamu. 

Jambo moja la msingi unalopaswa kujua kuhusu conscious mind ni kwamba sehemu hii ya akili ni maalumu kwa ajili ya kufanya machaguo mbalimbali. 
Kwa mfano umechagua kuwa na hofu, kuogopa pamoja na kuwa na wasiwasi kwa kutumia sehemu hii, (kumbuka hukuzaliwa ukiwa na hofu nyingine zaidi ya ile hofu ya kuzaliwa nayo). 
Na, unaweza kuamua na kuchagua kabisa kutokuogopa kabisa maisha yako yote kwa kutumia sehemu hii ya akili. 

Pia, kwa kutumia sehemu ya akili unaweza kuchagua:  mke wa kuoa, biashara unayotaka ufanye, kazi unayoipenda, nyumba utakayoishi, marafiki unaotaka kuambatana nao, maisha unayoyataka, fikra utakazochukua juu ya jambo Fulani lililopo mbele yako pamoja na machaguo mbalimbali uyafanyayo kila leo.        
 
Kwa ujumla conscious mind ndiyo kiongozi ambaye huongoza maisha yako na una mamlaka naye kwa sababu unaweza kumtawala kwa kumpa machaguo sahihi ili upate matokeo mazuri. 

Mbali na hilo unatakiwa kujua kwamba conscious mind huongozwa na mazingira uliyopo (cues) ambapo itakupasa utumie milango yako ya fahamu katika kudadisi na kuchagua vyema. 

Nini Maana Ya Subconscious Mind?
Subconscious mind, hii ni sehemu ya akili ambayo hupokea kile kilichoamuliwa pamoja na kuaminiwa na conscious mind kuwa kipo hivi ama vile na kuanza kukichakata mpaka upate matokeo Fulani. 

Kwa mfano kama utapeleka fikra za kujiona kujiona wewe ni mtu wa kuogopa, mwenye wasiwasi, mtu wa kuhofu tu, huwezi kuzungumza mbele za watu, huwezi kuwa na maisha mazuri, huwezi kufungua biashara yako, huwezi kuwa mtu mkuu, huwezi kufanya jambo Fulani kwa ufanisi n.k.

Itakachofanya akili hii ni kupokea kile ulichokipeleka pamoja na kukichakata mwishowe utapata matokeo yatakayoakisi kile ulichokiwasilisha (mawazo yako). 

Kutokana na hilo endapo itatokea siku umeulizwa ufanye jambo hilo hofu ya kuanza kufanya jambo hilo itakuja na utashindwa kabisa kulifanya. 

Hapa ndipo pale mtu utajikuta ukipokea mabadiliko ya haraka mwilini mwako kama vile: mapigo ya moyo kuanza kwenda mbio, jasho kuanza kukutoka, maumivu ya tumbo pamoja na kuongea kwa kigugumizi,
Na, kama utakuwa umesimama miguu itaanza kutetemeka, kufa ganzi na mwisho wa siku utaharibu kabisa. 

Ukichimba kwa undani suala hili utagundua kwamba hayo yote siyo kweli lakini kwa sababu umepeleka fikra za hofu ndizo zimepelekea matokeo hayo! 

Kumbuka utaitikia kutegemeana na fikra ulizoziwasilisha, kwa mantiki hiyo kama utakuwa umepeleka fikra za hofu, mashaka pamoja na wasiwasi ndivyo utakavyoonesha mwitikio huo, na kujikuta unaanza kuhofia. 

Na, ndiyo maana Kanuni ya mwititikio na vitendo inasema kwamba "matendo yako ni mwititikio wa fikra zako" hii inamaanisha kwamba endapo utapeleka fikra za hofu kwenye fahamu zako ndivyo utakavyoonesha mwititikio wa kuhofu katika maisha yako ya nje!

Vilevile kanuni ya msawazo wa akili inasema kwamba “kile unachokipata katika maisha yako ni uakisi wa kile unachokitengeneza akilini mwako”

Kwa mantiki hiyo endapo utapeleka fikra hasi za kuhofu, kuogopa, wasiwasi ndivyo utakavyopokea matukio hayo kwenye maisha yako halisi!

Mbali na hilo ni vema ukafahamu kwamba, sehemu hii ya akili hupokea oda na komandi zitokazo kwa conscious mind na kuanza kuzichakata mpaka kukuletea matokeo Fulani. 

Mpendwa endapo utaamini kwamba “huwezi ukafanya jambo Fulani” basi subconscious itakuza suala hilo na kukufanya usiweze kabisa kulifanya jambo hilo.  

Kwa mantiki hiyo utajikuta ukiwa unaendeshwa na hofu maisha yako yote. 
Hii ni sawa na kusema utakuwa umeipa hofu mamlaka ya kuongoza maisha yako kuliko hata wewe mwenyewe ulivyojipa mamlaka ya kuongoza na kutawala maisha yako.
 
Jinsi Ya Kutumia Subconscious Mind Ili Kuishinda Hofu…
Siku moja kijana mmoja alikuja kwangu kuomba ushauri.
 Aliniambia kwamba amekuwa ni mtu wa kuhofu sana maishani mwake na ameshindwa mpaka kwenye usaili zaidi ya mara kumi kutokana na hofu.
Na, kibaya zaidi ni kwamba alikuwa amefika kwenye hatua ambayo hawezi kabisa kufanya chochote kile kutokana na hofu…

Alijaribu kutumia kila mbinu lakini zote zilifeli, ilifika muda akawa anawaza bora hata ardhi ingepasuka ili imfukie kuliko kuendelea kuishi kwenye mateso ya hofu, wasiwasi na kuogopa! 

Basi siku moja alijikuta amepata ujasiri na kujiambia “itabidi niiache tabia hii ya kuhofu na kuogopa ili nibadili maisha yangu”… 

Ona sasa nimekosa mpaka kazi ya ndoto yangu kutokana na kuhofu na kuogopa… 

Ona sasa nimeshindwa hata kufungua biashara yangu ili nijitengenezee kipato cha ziada kwa sababu tu ya hofu…

Ona sasa nimeizuia mpaka hatima ya kesho yangu njema kutokana na kuhofu! 

Akajisemea… “Sitaki Tena Kuwa Mtumwa Wa hofu Nataka Kuwa Mshindi Kwenye Maisha Yangu”…

Na, nitajitoa kwa hali na mali mpaka niache kabisa tabia ya kuwa na hofu ya kupindukia… 


Jinsi Alivyotumia Subconscious Mind Kujiponya Na Tatizo La hofu…
Nilimueleza kuhusu mwingiliano uliopo kati ya conscious mind na subconscious mind katika utendaji kazi. 
Kwamba hofu ni tatizo alilolitengeneza yeye mwenyewe kupitia mfumo wake wa kuamini na atafanikiwa kuiacha kabisa endapo atafanikiwa kutoa “mental block”. 

Na, nikamueleza kwamba kupitia conscious na subconscious mind amejikuta akijiadhibu mwenyewe kwa kuamini katika dhana potofu. Na, sote tunafahamu kabisa kwamba utapokea kwa kadri ya uaminivyo…

Nguvu Ya Picha Akilini Ilivyomfanya Aweze Kuishinda Hofu… 

Nikamueleza kwamba ili uache tabia ya kuhofu jambo la kwanza kufanya ni kufuta picha zote mbaya ulizozitengeneza akilini mwako. 
Unatakiwa kujua kwamba subconscious mind ina nguvu sana katika kuchakata picha. 

Nikamuambia mara baada ya kufuta picha hizo hakikisha kwamba unatengeneza picha mpya na nzuri kuhusu wewe. 
Jione vile utakavyokuwa ukiacha kuhofu na kuogopa ogopa… 
Jione tayari ukiwa unafanya jambo lako ulilokuwa ukilihofu kwa muda mrefu, huku watu wakikupongeza kwa ufanywaji wa jambo hilo kwa weledi na ufasaha. 

Hatua Tatu Alizotumia Zilizomtoa Kwenye Tatizo La Hofu Mpaka Kumfanya Awe Mtu Huru…
Nilimueleza kwamba kama ameweza kujenga tabia ya hofu kwa kutumia subconscious mind, vilevile anaweza kutumia subconscious mind kubomoa tabia hiyo. 
Kumbuka awali tuliona kwamba hakuna mtu ambaye huzaliwa na tabia. 
Hivyo basi nikamuambia kwamba endapo utazingatia hatua hizi kuu tatu utalitibu kabisa tatizo lako na utafanikiwa kurudisha uhuru wako uliopotea kutokana na hofu… 

Naye alizingatia kwa umakini kwa kufanya kila siku hatua zifuatazo: 
1. Kila siku asubuhi na jioni alituliza akili zake, kwa kuingia katika hali ya utulivu uliotukuka, akijilaza chini au kitandani lakini hakusinzia huku akiruhusu kila kitu kipite then akarelax. 
Hii ilikuwa ni hatua ya kwanza katika kuiandaa subconscious iweze kupokea ombi lake. Alihakikisha anapata utulivu wa akili ili ombi lake lijibiwe na subconscious mind. 
Unatakiwa kujua kwamba subconscious mind hufanya kazi katika mazingira yaliyojaa utulivu. Hivyo basi alivyofanikiwa katika hatua ya kwanza alikuwa tayari kuingia kwenye hatua ya pili ifuatayo…

2. Alichukua kipande kifupi cha sentensi kinachohusu ombi alilotaka kuliwasilisha kwenye subconscious mind kisha akaanza kukitamka kwa kukirudia kwa dakika kumi hivi au zaidi. 

Alifanya hivyo kila siku asubuhi na jioni jioni ili ombi lake liweze kuzama kwenye subconscious mind lengo likiwa ni kuruhusu wazo hilo lipate kuchakatwa. 

Unatakiwa kujua kwamba kufanya hivyo alikuwa anaiandaa subconscious mind imtengenezee tabia mpya, ndiyo maana alikuwa anarudia kutamka kipande hicho mara kwa mara mpaka pale alipohakikisha ombi lake limepokelewa na subconscious mind automatiki…

Kwa mfano kila siku asubuhi akishaamka na kila jioni kabla ya kulala alikuwa anatamka kipande kifuatacho: “ujasiri, uhuru, utulivu wa akili, Amani, upendo na furaha navimiliki kuanzia saa hii. 
Niko huru kutoka kwenye tabia ya kuhofu, kuanzia saa hii sitahofu tena maishani mwangu mwote na ninaamini hili linaenda kutokea kupitia nguvu za subconscious mind…  

…na alihakikisha anarudia sala hiyo kwa dakika kumi hivi mpaka wazo hilo lilipozama kabisa kwenye subconscious mind. 
Ambayo huruhusu kila kinachowasilishwa kitokee. Kumbuka ishaandikwa katika Ayubu 22:28 kuwa;
 “nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako”.

3. Alitengeneza Picha Ya Uhuru Akilini Mwake…
Alichofanya katika hatua hii alianza kutengeneza uhuru akilini mwake. 
Unatakiwa kujua kwamba hakuna uhuru mzuri kama uhuru anaoutengeneza mtu akilini mwake mwenyewe. 
Mara baada ya kufanikiwa kuikomboa akili yake kifikra akaanza kutengeneza picha kamili juu ya yule atakayekuwa pindi akiwa huru kabisa kutoka kwenye kuhofu. 

Hata hivyo ili kutumia mbinu hii vyema alifanya yafuatayo: akiwa bado katika hali ya utulivu alitengeneza picha akilini mwake inayomuonesha yeye vile atakavyokuwa hapo baadae pindi akiwa huru kabisa kutoka kwenye tabia ya kuhofu na kuogopa. 

Na alifanya hivyo kwa kuhusisha hisia zake, baada ya miezi kadhaa kile alichokiona kilikuja kikatokea kwenye maisha yake kama alivyokiona akilini mwake.

Baada ya miezi mitatu kupita alinijuza kwamba kuna muujiza umetokea! 
…Nikiwa katika hali ya kuduwaa nikamuuliza kuna muujiza gani umetokea?
 ...Akanifahamisha kwamba tatizo lake la kuwa na hofu lililomtesa kwa muda mrefu limeisha na haogopi kitu chochote kile isipokuwa hofu yenyewe…
Nguvu ya subconscious mind ilimponya. 
Hiki ndicho kinachoenda kutokea kwenye maisha yako endapo utazingatia pamoja na kufanya yale ambayo yalifanywa na kijana huyu…

Jambo moja unalopaswa kujua ni kwamba hakuna kitu chenye nguvu kama picha hasa linapokuja suala la ubongo katika kufanya uchakataji. Unapaswa kujua kwamba picha zina nguvu sana katika kupelekea matokeo unayoyataka yaweze kutokea. 
Katika maisha unatakiwa kujua kwamba ni muhimu kuanza na picha kamili juu ya mwisho ule unaoutaka. 
Na, ukishauona mwisho wako ni lazima utaufikia. 
Kwanini nasema ni lazima utaufikia sabababu kubwa ni kwamba utaupata utayari wa kuufikia mwisho huo. 
Tengeneza picha inayoonyesha ule mwisho unaoutaka (uhuru wa kutokuhofia chochote kile) halafu ishikilie kwa muda mrefu mpaka pale utakapoufikia. 

Hitimisho hivyo ndivyo unavyotakiwa kutumia conscious na subconscious mind katika kubadili tabia ya kuhofu na kuogopa. 

Unatakiwa kujua kwamba ni lazima uamue kwa dhamiri yako (yaani kwa kutumia conscious mind) kuwa unataka kuacha tabia ya hofu ya kupindukia. Halafu wasilisha ombi kwenye subconscious mind, ambayo itachakata ombi lako na kukupa matokeo unayoyataka. Tumia hatua hizo tatu ili zikusaidie.

NB: Kuishinda hofu siyo suala la siku moja, bali wewe endelea kufanya hivyo kwa muda mrefu tu, unaweza kufanya hata kwa mfululizo wa siku tisini. 
Yaani kila siku asubuhi jitamkie maneno ya kukulinda dhidi ya tabia ya kuhofu pamoja na kujitengenezea picha akilini juu ya yule utakayekuwa pindi ukiacha kuwa muoga na hofu…
Kumbuka nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako!
Ahsante sana kwa muda wako na kusoma makala hii ndefu Sana! Kesho utasogezewa Mbinu ya tatu.

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No +255744284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...