Huwezi Kuishinda Hofu Mpaka Usome Kwanza Hii...
Habari yako rafiki? Ni matumaini yangu u mzima wa afya!
Ashukuriwe Mungu kwa neema zake nyingi!
Hatimaye leo hii somo letu la Mbinu tisa za kuikabili hofu linaenda kutamatika kwa kuangazia hoja tatu zizokuwa zimebaki!
Karibu uweze kupata mbinu hizi tatu za mwisho zikusaidie katika Kuikabili Hofu...
Siyo kila anayeona, anaona, na siye kila anayesikia, anasikia.
Kuna wengine wanaona lakini ni vipofu, na kuna wengine wanasikia lakini ni viziwi.
Ninasema hivi kwa sababu watu wengi huwa hatuoni vitu kwa namna ile inavyopaswa iwe, bali tunaona vitu kutegemeana na sisi tulivyo…
Ukweli ni kwamba tupo watu wengi ambao tunaona mambo kwa kulinganisha na jinsi sisi wenyewe tulivyo, kutokana na hilo tutajikuta tukijitengnezea milima na mwisho wa siku tunaanza kuhofia mambo hayo!
Mwanzo 1:26 Neno la Mungu linasema;
Mungu akasema, “Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu”…
Chukua neno “kwa mfano wetu”, halafu weka akilini mwako!
Iko hivi my friend, kama umeumbwa kwa mfano wa Mungu maana yake una uwezo wa kufanya makubwa tu kama yeye alivyoweza kufanya mambo makubwa…
Kumbuka hata mbingu na nchi pamoja na vyote vilivyomo vimepatwa kuwako kutokana na yeye…
Hata hivyo Mithali 3:16 Neno la Mungu linasema,
“kwa hekima Bwana aliiweka misingi ya nchi, kwa akili zake akazifanya mbingu imara;"
Unachotakiwa kuondoka nacho hapa ni kwamba, kwa busara yake mbingu na dunia na vyote vilivyomo vimekuwepo.
Hii inamaanisha kwamba hata huu uzuri wa dunia unauona pamoja na vitu vyote vilivyomo umekuwepo kwa sababu ya busara zake, sasa kama wewe umeumbwa kwa mfano wake, kwanini usijione kama vile yeye aliyekuumba anavyokuona?
Friend unamiliki busara, nguvu, maarifa, na uwezo mkubwa sana lakini unajiona kinyonge kwa sabu hautaki kujiona kama muumba wako anavyokuona na ndiyo maana umekuwa na hofu muda wote…
Ukweli ni kwamba vile Mungu anavyokuona huenda ikawa tofauti sana na vile wewe unavyojiona.
Kwamba wewe unajiona huwezi, hustahili na sikitu, lakini Mungu akawa anakuona kuwa unaweza, unastahili na wewe ni mtu wa thamani kubwa sana hapa duniani.
Friend badili mitizamo yako na kujiona kama vile Mungu anavyokuona, muweke Mungu awe kama kioo kwako ama hakika kila jambo litawezekana nawe hutakuwa na hofu tena…
Isaya 55:8-9 Neno la Mungu linasema;
“Maana mawazo yangu siyo mawazo yenu, wala njia zenu si zangu, asema Bwana”.
“Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu”
Mpenzi ukitaka kuishinda hofu huna kujiona kama vile Muumba wako anavyokuona, endapo utaweza kufanya hivyo nina hakika utabaki mawinguni, nawe hutakuwa chini bali utakuwa juu tu…
Na, ukishakuwa juu tu ni kipi kitakutia hofu tena mashani mwako?
Friend badili mitizamo yako kwa kujiona kama vile Mungu anakuvyokuna…
8. Chuja Taarifa Kabla Hujaziruhusu Ziingie Ubongoni Mwako…
Kuwa na utaratibu wa kuchuja taarifa my friend. Usiwe unamsikiliza kila mwenye mdomo kwani siye kila anayetoa sauti anazungumza, sauti zingine huwa ni kelele tu kwa hiyo usiziruhusu zikutie hofu ukashindwa kunywa maji…
Wewe ni tembo my friend usimruhusu chura akutie hofu nawe ukashindwa kunywa maji.
Friend unatakiwa kujua kwamba, siyo kila linalosemwa inatakiwa ulipokee, mengine yatakuwa ni sumu kwako na yatakumaliza kabisa. Kumbuka “maneno ya watu ni sumu huponya na kuua”.
Kwanini uchafue ubongo kwa kunywa maji machafu? Kwanini usichuje?
Weka mipaka juu ya kusikiliza hata vyombo vya habari basi bosi wangu, kwani siyo kila taarifa inayosomwa inakuhusu wewe…
Ukweli ni kwamba katika kuishi kwetu taarifa mbaya huvuma zaidi kuliko taarifa nzuri, na kuvuma sana kwa taarifa mbaya haimaanishi kwamba hakuna taarifa nzuri.
Kinachostaajabisha ni kwamba kwa siku moja matukio mazuri huwa ni mengi kuliko matukio mabaya, lakini hayavumi huku taarifa mbaya zikivuma zaidi!
Hata hivyo taarifa hizi mbaya zinavyoingia akilini mwako, hukutia hofu, na kwa sababu ubongo wako haukumbwa ukupe furaha utajikuta ukianza kutengeneza hofu juu ya kilichosemwa mwisho wa siku unapoteza kabisa furaha ya maisha yako na kuanza kuhofu.
Mpenzi msomaji kuwa na utaratibu wa kuchuja mambo yanayosemwa, kumbuka siyo kila ujumbe ni wako, na siyo kila taarifa ni yako.
Mengine ni sumu yatakumaliza kabisa kwa kukutia hofu…
9. Ishi Kimalengo…
Malengo humhamamasisha mtu, huchochea nguvu zake, huchochea bidii zake, hufungua macho yake pamoja na kufanya maisha yake yawe na kusudi.
Mtu mwenye malengo ni vigumu sana kuwa na hofu kwa sababu tayari kuna vitu kashapanga kuvifanikisha maishani mwake.
Na, muda wake wote atakuwa ametingwa kuvitafuta mpaka avipate.
Hii ni sawa na kusema badala ya kuhofu atakuwa anatumia hofu yake kama fursa ya kumtoa hatua aliyonayo na kumpeleka hatua nyingine.
Kwa mfano kama ulikuwa unahofu juu ya kutengeneza kipato cha chini unaweza ukaamua kuweka lengo la kuongeza kipato chako.
Ukishaweka tu lengo la kutatua tatizo lako hofu yako juu ya jambo hilo itapotea kwa sababu tayari kuna njia ya kulitatua umeshaiandaa.
Hivyo basi ili kutokuwa na hofu ni muhimu ukawa ni mtu wa kuishi kimalengo kwa maana malengo yatakupa ujasiri vilevile yatakupa uelekeo sahihi hivyo hutairuhusu hofu itawale maisha yako tena…
Neno La Mwisho…
Maisha ni mapambano lakini yule mwenye kuhofu ndiye hutolewa kwenye mchezo.
Siyo kila kitu kinatakiwa kikuogopeshe, vitu vingine vitafutie maarifa tu, halafu mchezo wa hofu unakuwa umeishia hapo…
Kwanini uogope? My friend wewe unaweza, unastahili na upo hapa kuishi maisha yenye furaha, amani na mafanikio.
Ahsante sana kuwa mwanafamilia wa masomo haya..
Ndimi Emmanuel Samuel King’ung’e; Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach & Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Name Kupitia Whatsapp No +255744284329 Au Tembelea Blogu Yangu Kwa Kuandika ekingunge.blogspot.com
Kwa Ushauri Zaidi Na Kwa Mafunzo Zaidi Karibu Inbox
Comments
Post a Comment