Huwezi Kujua Kusudi La Kuumbwa Kwako Mpaka Usome Kwanza Hii...
Hivi unafahamu kwamba zaidi ya asilimia 80 ya watu duniani kote hawaliishi kusudi la kuumbwa kwao, bali wanaishi huku wakitimiza kusudi ambalo hawakuumbiwa huku wengine wakikosa kabisa kitu cha kufanya?
Huenda hata wewe umekuwa ni mtu ambaye mpaka sasa hujajua kwanini uliumbwa, upo hapa duniani kwa kusudi gani na unatakiwa ufanye nini ili uweze kutimiza kusudi la kuumbwa kwako!
Rafiki unatakiwa kujua kwamba maisha pasipo kusudi si kitu, kwa sababu maana halisi ya maisha imebebwa na kusudi.
Hii ni sawa na kusema kama haujui kusudi la kuumbwa kwako maana yake umeshapoteza maana halisi ya maisha yako!
Na, ikiwa ushapoteza maana halisi ya maisha yako maana yake hakuna ulazima wa wewe kuendelea kuishi tena…
Kwa sababu hata kama utaendelea kuishi hakuna kitu chochote cha maana ambacho unaweza ukakifanya kwa ajili ya maisha yako, dunia yako, jamii yako pamoja na maisha ya watu wengine.
Sijui kwanini unasoma makala hii, lakini uamuzi ulioufanya wa kusoma makala hii ni uamuzi mkubwa sana kuwahi kuufanya maishani mwako, kwa maana unaenda kubadili kabisa historia ya maisha yako sekunde chache zijazo…
Ukweli ni kwamba kila mtu kaumbwa kwa kusudi Fulani, lakini kuligundua kusudi siyo kitu rahisi na ndiyo maana makala hii imeandikwa ili ikusaidie katika kugundua kusudi lako pamoja na kuliishi kusudi hilo!
Na, moja ya sababu ambayo huwafanya watu wengi washindwe kugundua kusudi la kuumbwa kwao, ni kwa sababu kuna mifumo ambayo tayari imeshawatengenezea kusudi jingine (kusudi dogo) ambalo ni tofauti na kusudi la kuzaliwa kwao (kusudi kuu).
Ukweli ni kwamba ukishatengenezewa kusudi na mfumo Fulani utajikuta ukiridhika kabisa na ukaishia kuona kama hilo ndilo lilikuwa kusudi la kuumbwa kwako kitu ambacho siyo kweli kabisa!
Kutokana na hilo watu wengi hujikuta wakitumia muda wa maisha yao yote kuliishi kusudi dogo na siyo kusudi la kuumbwa kwao, hali ambayo hushusha hadhi ya maisha yao pamoja na kuwafanya wapige hatua ndogo kimaisha…
Mara nyingi hali hii huchangiwa na watu hao kuiamini zaidi mifumo iliyowatengenezea kusudi hilo, pasipo kuangalia wao wenyewe wanapenda kufanya nini na wanaweza wakatumikaje hapa duniani ukiachilia mbali na vile mifumo ilivyowatengeneza.
Mpenzi msomaji unatakiwa kujua kwamba hakuna raha yoyote ile utakayoipata ikiwa utaliishi kusudi dogo tu, zaidi ya yote utakutana na changamoto pamoja na makwazo ya hapa na pale.
Hii ni kwa sababu mfumo unaokutengeneza utakuonesha kwamba unastahili kuwa mtu Fulani kwa sababu umekutengeneza uwe hivyo, lakini wewe ukawa hukuzaliwa uje uwe huyo uliyetengenezwa!
Kusudi Ni Nini Labda?
Kwa tafsiri nyepesi kusudi ni kutekeleza mpango wa Mungu kukuumba hapa duniani!
Au
kusudi ni kufanyika kwa jambo Fulani. Hii ni sawa na kusema kwamba kuna kusudi lililopo kutokana na kufanyika kwa maisha yako hapa duniani.
Ukweli ni kwamba kila mtu kaumbwa kwa kusudi Fulani, lakini kutokujua kusudi la kuumbwa kwako isiwe sababu ya kukufanya useme ulipaswa uwe hivyo ulivyo sasa.
Kwa maneno mengine ni sawa na kusema, kama vile mtu alivyotengeneza kisu alivyotambua kusudi la kutengeneza kisu (matumizi yake) vilevile hata Mungu alikuwa na kusudi la kukuumba hapa duniani.
Hata ukienda kusoma maandiko matakatifu utagundua kwamba, Mungu huwa ana kusudi la kumuumba kila mwanadamu!
Yeremia 1:5- Neno la Bwana linasema: “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa”
Kama vile Mungu alivyokuwa na kusudi la kumuumba Yeremia, vivyo hivyo ndivyo alivyokuwa na kusudi la kuruhusu uumbwaji wako!
Kwa hiyo leo kabla hujafanya chochote kile jaribu kufikiri kwa undani, uliumbwa ili uje ufanye nini hapa duniani.
Hata hivyo unatakiwa kujua kwamba kusomea taaluma Fulani, au kufanya kazi Fulani haimaanishi kwamba unaliishi kusudi la kuumbwa kwako.
Huenda kusudi lako lipo nje na kazi unayoifanya, na hiyo kazi huenda ikawa haihusiani kabisa na kusudi la kuuumbwa kwako!
Hivi ushawahi kujiuliza vipi kama ungekuwa hujasomea hivyo kozi uliyosomea ungekuwa nani?
Je, ushawahi kujiuliza vipi kama ungekuwa hufanyi hiyo kazi unayofanya ungekuwa unafanya nini?
Hicho utakachokijibu kitathimini vizuri, huenda ndilio kusudi la kuumbwa kwako!
Rafiki unatakiwa kujua kwamba kusudi lako limebebwa kwa ajili ya watu wengine, hii inamaanisha kwamba kutokuliishi kusudi lako ndicho kimekuwa chanzo cha watu wengine kushindwa kufurahia maisha…
Na, ndiyo maana hata kama mti utazalisha matunda mazuri kiasi gani hauwezi ukayala matunda hayo wenyewe. Kwa mantiki hiyo ni sawa na kusema, tunaishi hapa duniani kwa ajili ya watu wengine.
Kutokana na ukweli huo, ukiwa hai maana yake una nafasi nzuri ya kuyafanya maisha ya watu wengine yawe mazuri, kwa kuliishi kusudi lako!
Hivi ushawahi kujiuliza ni mara ngapi umepelekea watu wengine wakashindwa kuishi maisha makamilifu hapa duniani kutokana na kutokuliishi kusudi lako?
Mpenzi huu ni wakati wa kulitafuta kusudi lako, unatakiwa kujua kwamba kuna watu ambao waliandikiwa wataishi kutokana na kusudi lako la kuumbwa kwako hapa duniani.
Hivyo basi unaposhindwa kuliishi kusudi lako, maana yake unakuwa unawaweka wenzako katika mazingira magumu na katika hali tata zaidi.
Huu siyo wakati wa kuendelea kubaki gizani tena bali ni wakati wa kuamua kuifuata nuru ilipo.
Nuru ya maisha yako itakuangaza siku utakayolijua kusudi la kuumbwa kwako hapa duniani.
By the way, tar 23/08/2023 nilichapisha kitabu changu ambacho kilitolewa bure kabisa kwa wapenzi wasomaji wa makala zangu!
Jina la kitabu chenyewe ni; Sikuja Duniani Kwa Bahati Mbaya; Bali Nilikuja Kwa Kusudi Maalumu...
Ni KITABU ambacho ni kizuri kuwahi kuandikwa!
Na ninaamini ukikisoma chote utagundua kusudi la kuumbwa kwako, na hutaishia kuligundua tu bali utaanza kuliishi hali itakayobadili historia ya maisha yako!
Huenda ulipitwa na ofa ya kitabu Hicho!
Kitabu hicho kitatolewa bure muda wote, kwa hiyo kama ulipitwa na ofa fanya yafuatayo!
Andika Neno KITABU kwenda no +255744284329, nawe Utatumiwa kitabu chako mapema iwezekanavyo!
Comments
Post a Comment