Huwezi Ukafahamu Madhara Ya Kuendekeza Hofu Mpaka Usome Kwanza Hii...

Hakuna kitu ambacho hufanyika kisicholeta matokeo fulani!
Unachopaswa kujua ni kwamba, kwa chochote kile unachokifanya ni lazima kitaleta matokeo fulani maishani mwako!
Na ifahamike kwamba, matokeo hayo huwa ya aina mbili, aidha matokeo mazuri au mabaya.
Yafuatayo ni matokeo ya kuendekeza hofu:

1. Utampoteza Mungu Katika Maisha Yako…
Mtu ambaye ana hofu cha kwanza haamini katika Mungu, kwa maana kila jambo linawezekana kwake yeye aaminiye. 

Hivyo basi pasipo kujua hofu humuondoa kwenye chanzo chake na kumfanya aendelee kutapatapa.

Ukweli ni kwamba Mungu hashindwi na chochote kile, kwake yeye kila jambo linawezekana…
Hivyo basi kwa yule mtu ambaye ana hofu ni rahisi sana kumpoteza Mungu kwa maana anakuwa hana tumaini… 

Na ukishampoteza Mungu maana yake utakuwa unaongozwa na akili zako pamoja na kutumainia njia zako ambazo mwisho wa siku zitakupeleka mautini…
Mithali 14:12 neno la BWANA linasema;
“iko njia ionekanayo sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake njia za mauti”

Friend unatakiwa kujua kwamba, ukishampoteza Mungu ni rahisi kuteseka kwa hofu maisha yako yote pamoja na kukosa kabisa uelekeo sahihi maishani mwako…

Na ukishapoteza uelekeo, utapoteza dira, ukipoteza dira huwezi kuifikia hatima yako badala yake utakuwa unahofu tu.

Kwa hiyo hofu ikishakutoa kwenye njia sahihi (kumuacha Mungu), wewe hutakuwa tofauti na nyumbu na farasi ambao hawana akili! 
Kwani wanyama hawa utawaona wakitembea lakini hawajui wanakoenda ni wapi!
Zaburi 32:9
“msiwe kama farasi wala nyumbu, walio hawana akili”

2. Utakosa Uthubutu Wa Kufanya Jambo Fulani...
Ni ngumu sana kupata uthubutu wa kufanya jambo Fulani ilihali ndani yako una hofu…
Unatakiwa kujua kwamba mtu mwenye hofu hana tofauti na mgonjwa ambaye yupo hoi kitandani na hajiwezi kabisa.

Unachopaswa kujua ni kwamba, ukiwa na hofu ni ngumu sana kupata nguvu na hamasa za kufanya jambo Fulani, kwani utakuwa unahofia jambo hilo kutokukuletea matokeo mazuri!

Kwa mantiki hiyo kila ukijaribu kufanya jambo hilo utajikuta ukikosa nguvu za kufanya, pamoja na kukosa hamasa mwisho wa siku utaishia kukata tamaa.
Kuna watu wamebaki kwenye hatua ileile kwenye maisha siyo kwa sababu inatakiwa wabaki hatua hiyo tu, ila ni kwa sababu hofu zao zimekuwa ni kama mlima kwao unaowazuia washindwe kwenda hatua nyingine.
Friend hofu ikiendelea huzaa kilema, na ukishakuwa kilema ni ngumu sana kuweza kufanya jambo Fulani…

Utajikuta ukiingia kwenye orodha ya wale watu ambao wanataka kuonewa huruma....
Sasa kama wewe mwenyewe umeamua kutokujionea kwa kuhofia na kuogopa kitu ambacho hata hukijui vizuri, je ni nani atakayekuonea huruma? 
Unahitaji kufikiri juu ya hili my friend.

3. Utabaki Katika Kiwango Kilekile Cha Ufahamu...
Watu wengi wenye hofu huwa wanageuka na kuwa wakosoaji hasa wanapokutana na fursa fulani maishani mwao! 
Na hii ni kwa sababu wanakuwa wameruhusu hofu iweze kuongoza na kutawala maisha yao.

Na, ndiyo maana ni ngumu sana kumpata mtu mwenye hofu anayependa kujifunza.

Unatakiwa kujua kwamba hofu humuweka mtu kwenye kiwango kimoja cha ufahamu kwani kupitia hofu zake atajiona kuwa yeye ni mtu wa kufanya mambo kwa kiwango alichonacho tu, na si mtu wa kufanya mambo yaliyo kiwango cha juu zaidi ya pale alipo!

Dunia tuliyonanyo sasa inabadilika kila leo hivyo kila mtu hana budi kuwa mwanafunzi wa kujifunza kila kinachoendelea…

Kumbuka kama hujitengenezi kuwa wa kisasa utapitwa na wakati, kama hautafuti taarifa sahihi utakosa matumizi, kama hauna ufahamu wa kutosha huwezi ukawa kwenye mlolongo mzuri…
Friend endapo utaendelea kuhofu utabaki kwenye kiwango hicho hicho cha ufahamu. 

4. Utabaki Kuwa Maskini…
Ni ukweli usio na kipingamizi kwamba hakuna mtu ambaye huzaliwa akiwa na: nyumba, pesa kwenye akaunti ya benki, gari au maisha mazuri basi sote huja duniani tukiwa sawa.
Lakini tunakuja kutofautiana kimaisha kutokana na namna tunavyotumia hofu zetu!
Unatakiwa kujua kwamba hofu ya umasikini imetengeneza makundi mawili ya watu…
Kuna watu wamekuwa matajiri kwa sababu ya hofu ya umaskini. Vilevile kuna watu wanazidi kuwa maskini kwa sababu ya hofu ya umaskini…

Watu hawa ndiyo huona umaskini kama umaskini, na kwamba wao wamezaliwa kwenye familia maskini, kwenye jamii maskini pamoja na kuzaliwa kwenye nchi maskini.
Hivyo hujikuta wakihofu muda mrefu mwisho wa siku wanaamua kuridhika na hali zao kitu ambacho siyo sahihi kabisa!

Sikiliza my friend… “ni ngumu sana kuwa tajiri, lakini vilevile ni ngumu sana kuishi ukiwa maskini” chagua ugumu wako…

Na, ukichagua kuendelea kuhofu badala ya kupambana utakuwa umechagua umaskini…

Na, ifahamikie kwamba hofu humhamasisha mshindi huku ikimshinda mpotezaji… 
Endapo utaruhusu hofu ikushinde basi hutakuwa na tumaini lolote lile lililo jema utaendelea kuwa maskini maisha yako yote…

5. Utazidi Kudumaa Na Kudidimia
Nioneshe mtu mwenye hofu aliyepiga hatua kimaisha nami nikuoneshe mtu aliyepata bahati ya kuokota nyumba…
Unatakiwa kujua kwamba ukiwa na hofu ni ngumu sana kuvuka na kwenda ng’ambo ya pili…
Na, hii ni kwa sababu hofu itakuwa inakudamaza na kukufanya ubaki palepale.

Kwenye fahamu zako unatambua kwamba inatakiwa uondoke uende sehemu Fulani, lakini kinachotokea unajikuta huondoki kwani hofu inakuwa imefunga miguu yako pamoja na kudhibiti mwili wako usiweze kuondoka kabisa…

Kwa hiyo utajikuta ukibaki palepale huku miaka ikizidi kusonga mbele.
Wenzako wanazishinda hofu na kupiga hatua huku wewe ukibaki palepale pasipokusonga mbele…

Je Nini Nifanye Ili Niweze Kuishinda Hofu?
Usijali Kesho Litajadiliwa Hilo Kwa Undani Zaidi!

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No +255744284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...