Njia kuu tisa za kuikabili hofu yoyote ile...

Kwa kila hali au tatizo lolote lile lililo katika maisha yako, linakuhitaji wewe mwenyewe uchukue hatua katika kulikabili au kulitatua!

Na endapo hautachukua hatua katika kulitatua, hakuna atakayechukua hatua kwa niaba yako.

Kumbuka mambo yaliyotulia yatabaki katika hali ile ile ya utulivu mpaka pale yatakapobadilishwa.

Je, umekuwa ukihofu kwa muda mrefu sana maishani mwako? 
Kama jibu ni ndiyo basi ndani ya sekunde chache zijazo unaenda kubadili kabisa historia ya maisha yako...

Na, endapo utafuata kilichoandikwa katika makala hii hatua kwa hatua, nakuhakikishia hutoogopa chochote kile isipokuwa hofu ndiyo itaanza kukuhofia wewe...
Je nifanye nini niikabili hofu? Usijalii fanya yafuatayo:- 

1. Rejesha Imani Kwa Mungu Wako…
            Zaburi 34:4
“Nalimtafuta BWANA akanijibu, akaniponya na hofu zangu zote”
Mpenzi ni mara ngapi umelia na Mungu kuhusu hofu zako au hata hujawahi kabisa kumueleza? 

Daudi anakuhabarisha kwamba umtafute BWANA naye atakuponya na hofu zako zote...

Unatakiwa kujua kwamba Mungu pekee ndiye anayeujua mwanzo na mwisho wako, hivyo ukijikabidhi kwake yeye atakupigania huku wewe ukiwa umelala na ukishaamka utajikuta ushakuwa mshindi.

Uzuri wa Mungu ni kwamba yeye atatenda kupitia wewe, kwa hiyo ukijikabidhi kwake kwa imani hata mambo uliyokuwa unahofia kuyafanya utajikuta ukifanya pasipo hata kusitasita...

Mpenzi msomaji Mungu anasema na wewe kwa uwazi kabisa kwamba umtafute naye atakujibu na atakuponya na hofu zako zote…

Hata hivyo ukisoma warumi 8:31 Neno la Mungu linasema; 
“basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwa upande wetu ni nani aliye juu yetu?

Friend ni kipi hicho kitakuwa juu yako ilihali Mungu yuko upande wako?

Hebu jaribu kuvuta picha Mungu yule asiyeshindwa na chochote kile yuko upande wako,  je ni kipi kitakufanya upoteze tumaini na kuanza kuhofu? 

Hata hivyo mwandishi wa kitabu hiki (Paulo) anaendelea kufafanua zaidi kwenye, Warumi 8:35 akisema...
“Ni nani atakayetutenga na upendo wa kristo?  Je, ni dhiki, au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga”?

Kwa lugha nyepesi naweza kusema kwamba upendo wa Mungu kwa wanadamu ni mkubwa sana, na kwa sababu ya upendo huo kuwa mkubwa ni dhahiri kwamba, ukimueleza chochote kile atakupigania,  mpaka ahakikishe wewe kama mtoto wake mpenzi unatimiziwa mahitaji yako...

Kinyume chake kikiwa, kadri unavyoipa hofu nafasi ndivyo unavyompoteza Mungu na upendo wake katika maisha yako!
Kumbuka Mungu huwa hakai kwa mtu wa kusitasita…

Na, ifafahamike kwamba mtu wa kusitasita huwa hafiki mbali, kwani mwisho wa siku hujikuta akiruhusu hofu imuongoze na siyo kweli tena, hali hii humpelekea ashindwe nguvu za kulikabili tatizo linalomsibu!

Kingine unachopaswa kuondoka nacho hapa ni kwamba, mtu mwenye hofu huwa haogopi kitu kingine zaidi ya fikra alizozitengeneza mwenyewe, na kinachosikitisha zaidi ni kwamba fikra zenyewe mara nyingi huwa siyo za kweli. 

Hebu jaribu kuvuta picha mtu unahofia fikra zako mwenyewe na ubaya ni kwamba fikra zenye zinazoogopwa hazina ukweli wowote ule!

Nini ufanye? ...Unachopaswa kufanya ni kutoa hiyo fikra hasi uliyoipeleka ubongoni mwako kupitia kuwaza kwako.

Na, ifahamike kwamba utaitoa hofu siku utakayojua ukuu, mamlaka, nguvu na uwezo wa Mungu!

Ukienda kusoma kitabu cha Ayubu ile sura ya 22:21; Neno la Bwana linasema...
“Mjue sana mungu, ili uwe na amani, ndivyo mema yatakavyokujia”

Mpenzi msomaji ukimjua Mungu vizuri, ukajua uweza wake, ukatambua na miujiza pamoja na uponyaji alioachilia kwa ajili ya watu wake nina hakika hutoogopa tena.

Ukweli ni kwamba Mungu wako ni mkuu sana na kila jambo mbele zake linawezekana, chakufanya wewe mueendee halafu mueleze shida yako kwa uwazi huku ukitarajia mwisho mwemaa nawe utaufikia...
 
Kumbuka ilishasemwa kwamba, "kwa sababu hiyo nawaambia: Yoyote myaombayo mkisali aminini ya kwamba mnayapokea nayo yatakuwa yenu" Marko 11:24..
 
Hata hivyo unatakiwa kujua kwamba ili umjue Mungu ni lazima utimize sharti kuu moja, ambalo ni kujifunza Neno lake. 
Na ifahamike kwamba Mungu ni neno hai linaloishi. 
Hivyo basi endapo utakubali kulipokea Neno lake, utakuwa ni sawa na umempokea Mungu mwenyewe. 
Kwani Mungu ni neno, na hili limejithibitisha katika Yohana 1:1-4 ambayo inasema...

“Hapo mwanzo kulikuwako Neno,
Naye Neno alikuwako kwa Mungu,
Naye Neno alikuwa Mungu.
Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu, vyote vilifanyika kwa huyo;
Wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika.”

Unachopaswa uondoke nacho hapa ni kwamba Mungu hutuongoza sisi wanadamu kupitia Neno lake…
Habari njema ni kwamba Neno lake linaponya, linatakasa, linaleta ujasiri na kuponya hofu, linaokoa pamoja na kufanya miujiza mingi.

Hata hivyo, ili uweze kujiponya na hofu huna budi ulipokee neno lake na kulifanya liwe kila kitu kwako. 

Kadhalika katika kitabu cha Yoshua 1:9 Neno la Mungu linasema;
“Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo na ushujaa. Usiogope wala usifadhaike, kwa kuwa Bwana Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako”

Mpenzi Mungu anakuamuru ujivike uhodari wala usiogope tena, kwani ukiwa na hofu Mungu hatakuwa pamoja na wewe, bali ukiacha kuogopa Mungu wako atakuwa pamoja na wewe na kila uendako.

Je ni kipi unachokihofia? Ni kipi hicho kinamzidi Mungu? Mungu si yupo juu ya yote au? 

Kama ulimwengu na vyote vilivyomo vimepata kuwako kutokana na mkono wake Mungu, je ni kipi kitamshinda yeye aliyeviumba vitu vyote?
Ndugu usiogope tena yakabidhi maisha yako yote kwa Mungu. 

Mtolee Mungu yote yaani: maradhi, maumivu, mateso, hofu, taabu, shida, dhiki, njaa, umaskini vyote mtolee mungu naye atakupumzisha. 

Mathayo 11:28
"Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha" 

Mpenzi huo mzigo wa kuhofu muda wote mtolee Mungu naye atakupumzisha!

Kesho Nitakusogezea Mbinu ya pili, fuatilia kwa mwendelezo upokee uponyaji.

Ahsante sana kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No +255744284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...