Fahamu Kuhusu Maeneo Matatu Ya Uwezo Ambao Kila Binadamu Huzaliwa Nao....
Habari yako rafiki! Ni matumaini yangu u mzima wa afya! Kwa upande wangu namshukuru Mungu niko vizuri na ninaendelea vyema kabisa!
Karibu kwenye mwendelezo wa somo letu linaloangazia uwezo wa maeneo kumi ambayo kila binadamu huzaliwa nao!
Kama unakumbuka vizuri, makala iliyopita ilidokeza hoja tatu za maeneo uwezo! Hii ni sawa na kusema, makala hii ni mwendelezo wa makala iliyopita!
Kwa leo utaenda kuoneshwa uwezo mwingine wa maeneo matatu ambayo kila binadamu huzaliwa nao!
Angalizo: unaposoma maeneo haya ya uwezo, uwe unahusisha na maisha yako ili utambue unamiliki uwezo gani!
Ukishatambua eneo la uwezo wako kwa msaada zaidi nitafute nami nitakupa mawili matatu juu ya kipi unatakiwa ufanye!
Karibu sasa kwenye uchambuzi wa maeneo mengine matatu:-
5. Uwezo Wa Uchoraji (Spatial Intelligence)
Hawa ni wataalamu katika kuona matukio fulani na kisha kwenda kuyatengenezea picha kwa kuyachora na kuyawasilisha kupitia michoro mbalimbali...
Wana uwezo mzuri sana wa kuchora picha zinazopendeza na kuvutia!
SIFA ZAO
✔️Wanakumbuka rangi mbalimbali kama vile: nguo za watu, majengo, magari n.k
✔️Wanaweza kueleza vizuri hadi anayesikiliza akajenga picha ya wanachoongea.
✔️ Wanapenda kuchora picha mbalimbali hata hata kama siyo wachoraji wazuri sana...
✔️ Wanapenda kumechisha rangi za vitu mfano, mavazi, nyumbani na simu..
✔️ Wanapenda sana kuona picha na filamu (movies)
✔️ Akianza kuelekeza mahali anataka kila kitu ambacho kitakusaidia utakapokwenda.
✔️ Wana kumbukumbu sana na maeneo mbalimbali na hawapotei kirahisi hata kama walifika mara moja.
✔️Huwa wanakumbuka watu hata kama walikutana na wewe mara moja kwa muda mfupi.
KAZI WANAZOWEZA KUFANYA WATU WANAOMILIKI UWEZO HUU
➡️Mbunifu wa mavazi (designer)
➡️Wachoraji.
➡️Muuzaji nguo.
➡️Muuzaji wa bidhaa za urembo.
➡️Mpiga picha.
➡️Msanifu majengo.
➡️Mpambaji.
➡️Mrembaji wa ndani.
➡️Mpaka rangi.
➡️Mwongoza filamu/muziki.
6. Uwezo Wa Kujijua Kiundani (Intrapersonal Intelligence)/(Self Smart).
Hawa ni wazuri katika kujijua wao wenyewe kiundani, hii ni sawa na kusema watu hawa wanatambua vyema utu wao na thamani yao.
Wanaujua vyema udhaifu na uwezo wao.
Watu hawa mara nyingi wapo kivyao vyao na wako bize na mambo yao..
Mara nyingi siyo waongeaji sana na wanapenda kujifunza kivyao vyao hata kama wangesaidiwa kirahisi na mtu mwingine kirahisi...
SIFA ZAO...
➡️Mara nyingi hupenda kufanya kazi peke yao na watu wengi huwatafsiri kama ni wachoyo..
➡️Wanafanya mambo kwa ubora sana, pale wanapokuwa wanafanya wenyewe.
➡️Wanapenda sana falsafa mbalimbali. Wakiongea utawasikia "kulingana na falsafa fulani"
➡️Wanapenda sana kuzungumza vitu vya kufikirika sana nadharia, ideas n.k
➡️Wanapenda sana mambo ya saikolojia
➡️Wanapenda mambo yao yakamilike ndiyo wafanye kitu (perfectionist).
➡️Ukitaka kufanya jambo wanauliza maswali mengi sana wakati mwingine unaweza kuwaona wasumbufu.
➡️Wanapenda kujiajiri, hawapendi kuajiiriwa hawapendi kuamrishwa , hawapendi kutumwa, hawapendi kupelekeshwa na maagizo.
➡️Wanapenda kuweka diary ya mambo. ➡️Wanaandika tar, matukio na kumbukumbu sana na watu.
➡️Wanapenda kujifunza kuhusu tabia zao.
➡️Wanapenda kufikiri na kuja na mawazo mazuri ya biashara.
KAZI WANAZOWEZA KUFANYA WATU WANAOMILIKI UWEZO HUU.
🔹Mwanasaikolojia
🔹Mwanatheolojia (mhubiri)
🔹Mtoa ushauri mzuri/consultant
🔹Mjasirimali
🔹Mwanafalsafa mzuri
🔹Mwandishi mzuri wa hadithi
NB:
Mimi mwalimu wenu nalimiliki uwezo huu nisiwe muongo!
Hii inamaanisha yule ambaye huwa najiona kabla mtu mtu yeyote yule hajaniona ndiyo mimi halisi.
Kwa hiyo najijua vyema kuliko yeyote yule anavyodhani ananijua!
Kuhusu idea ninazo na ninaendelea kuziandaa zitakazokuja kuibadili jamii yangu ya Tanzania!
7. Uwezo wa ujasiriamali (Entrepreneurial Intelligence)
Huu ni uwezo wa kuwahi kuliona soko na kisha kuandaa rasilimali pamoja na bidhaa utakazouza.
Unatakiwa kujua kwamba Kuna watu huwa wanaishi miaka kumi mbele ijayo.
Watu hawa huona soko litakuwaje na kuandaa bidhaa zitakazohitajika miaka ya huko mbeleni.
Huu ndiyo uwezo unaongoza zaidi kulipa duniani kuliko uwezo wowote ule.
Hata hivyo mabilionea wakubwa duniani kama vile: Elon musk, Michael Dell, bilgates, Michael Zuckerberg wametumia uwezo huu!
Unatakiwa kujua kwamba saa hii kuna mtu anaumiza kichwa huko juu ya dunia ya mwaka 2050 huko...
SIFA ZAO
➡️Wanapenda sana kujifunza...
➡️Wanapenda sana kufanya tafiti mbalimbali.
➡️Wanapenda sana kujaribu vitu..
➡️Wanapenda sana kutaka kujua tabia za watu pamoja na mahitaji yao.
➡️ Wanapenda sana masuala ya ubunifu.
➡️ Wanapenda sana kufanya mambo mapya. N.k
NB: Watu hawa hufanya kazi za biashara pamoja na ujasiramali!
Kutokana na hilo hujikuta wanapata majibu juu ya mahitaji ya watu hao na mwisho wa siku wanaanda bidhaa then boom!
Unatakiwa kujua kwamba kuna mtu yupo anakufikiria wewe hapo kwamba akutengenezee bidhaa gani au huduma gani ili uje uilipie..
Hata mimi ni miongoni mwa watu hao nafikiria namna gani ninaweza nikamfanya mtu atoe pesa mfukoni mwake ili anilipe kutokana na huduma nitakayompa haha 😂
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!
Mwendelezo Wa Somo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 0744284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment