Fahamu Kuhusu Tabia/Sifa Za Fedha...
Habari rafiki! Ni matumaini yangu u mzima wa afya! Kwa upande wangu namshukuru Mungu, niko mzima wa afya na ninaendelea vyema kabisa!
Karibu sana kwenye mwendelezo wa somo linaloangazia kuhusu elimu ya fedha! Kama unakumbuka makala iliyopita ilishia kudokeza sifa kuu mbili za fedha!
Makala hii ni mwendelezo wa makala iliyopita, kwa leo utaenda kuoneshwa sifa nyingine bainifu za fedha kama zinavyodokezwa hapa chini:-
3. Fedha Huwafuata Watu Wenye Imani Nayo...
Kuamini ni kupokea kuwa jambo fulani ni kweli hata kama jambo hilo siyo kweli!! Hii ni sawa na kusema ili ufanikiwe kifedha unatakiwa upokee kuwa ni kweli unamiliki fedha nyingi hata kama mfukoni mwako hauna fedha kabisa!
Unatakiwa kujua kwamba, imani halisi haiji katika kuona uhalisia wa tukio lenyewe, bali inakuja kwa kuweka tumaini thabiti juu ya kile kilichoaminiwa kuwa kitatokea!
Na ndiyo maana kanuni ya kuamini inasema, "chochote kile utakachokiamini kuhusu wewe na dunia yako kitafanyika kwako pamoja na dunia yako kama ulivyoamini"
Kwa hiyo endapo utaamini kwamba utafanikiwa kifedha na pesa ipo kwa ajili yako, itakuwa hivyo!
Unatakiwa kujua kwamba, imani haijawahi kumsaliti muamini wake! Kumbuka nawe utapokea kwa kadri ya uaminivyo!
Tofauti kubwa kati ya watu wanaofanikiwa kifedha, na wale wasiofanikiwa ipo kwenye imani zao!
Ikiwa wale wanaofanikiwa kifedha wanaamini kwamba waliumbwa wafanikiwe kifedha na fedha ipo kwa ajili yao!
Wale wasiofanikiwa kifedha huamini kwamba wao ni maskini, walizaliwa kwenye familia maskini, wamezaliwa kwenye jamii maskini na nchi maskini hivyo hawawezi kufanikiwa kifedha bali watakufa wakiwa maskini!
Rafiki huhitaji kingine zaidi ya kubadilisha mfumo wako wa kuamini kama kweli unataka kufanikiwa kifedha!
4. Fedha huwa haitafutwi bali huvutwa...
Ukitaka kunasa chuma ni lazima utumie sumaku! Vivyo hivyo ndivyo ilivyo hata kwenye kuinasa/kuvuta pesa!
Unatakiwa kujua kwamba, ni lazima uandae mtego utakaokuwa unainasa fedha na kuivuta ije maishani mwako!
Moja ya mtego sahihi unaoweza kutumia kunasa fedha nyingi ni kupitia kutatua matatizo ya watu!
Kwa mantiki hiyo, badala ya kupambana kutafuta fedha wewe pambana kutafuta matatizo, kisha yatatue ndipo utapata fedha!
Unatakiwa kutatua matatizo hayo, kwa sababu hakuna ambaye hulipwa kwa kugundua tatizo bali watu hulipwa kwa kutoa suluhu ya matatizo!
Rafiki kwenye eneo ulilopo bila shaka kuna matatizo, ninachoweza kukushauri ni hiki: anza kutatua matatizo hayo, hapo ndipo fedha ilipo!
5. Fedha Ina Tabia Ya Kushuka Thamani...
Rafiki fedha huwa haipandi thamani, isipowekezwa! Kwa mfano ukiweka milioni moja kwa miaka kumi itabaki kuwa milioni moja ile ile!
Hata hivyo watu wengi katika kufanya manunuzi huishia kununua liabilities (dhima) ambazo huwa zinapungua thamani kwa kadri ya miaka inavyozidi kwenda mbele!
Unatakiwa kujua kwamba, liability ni kitu chochote kile ambacho hutoa fedha mfukoni mwako! Mfano:Nguo, Simu, Gari, Vifaa Vya Umeme, n.k
Sasa basi ili uweze kupandisha thamani fedha yako, unatakiwa ununue assets (Mali) ambazo huwa zinapanda thamani kadri ya miaka inavyozidi kwenda mbele!
Hii ni sawa na kusema, kwa kadri mali yako inavyozidi kupanda thamani vivyo hivyo na fedha yako itakuwa inapanda thamani!
Unatakiwa kujua kwamba, assets ni kitu chochote kile ambacho huingiza fedha mfukoni! Mfano: Ardhi, Madini, Nyumba za kupangisha, gari kwa ajili ya kutoa huduma ya usafiri, n.k
Rafiki kama kweli unataka kufanikiwa kifedha unatakiwa ufikiri namna gani unaweza ukatengeneza assets nyingi na kupunguza kununua liabilities!
Huna budi kutambua kuwa chochote kile utakachomiliki kama hakiingizi fedha basi moja kwa moja kinapoteza fedha zako!
Jaribu kuchunguza kwenye maisha yako kati ya assets na liabilities kwa kiasi kikubwa unamiliki nini!
6. Fedha Haitaki Ukawaida/(Wastani)...
Kama vile ambavyo hakuna mtu anayependa vitu vya kawaida, vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa fedha!
Unachopaswa kuondoka nacho hapa ni kwamba, endapo utafanya jambo kwa namna ambayo kila mtu hufanya pamoja na kufanya kwa hali ambayo imezoeleka na kila mtu huwezi kutengeneza fedha za kutosha!
Hivyo basi ili uweze kutengeneza fedha katika biashara au ajira yako, lazima ujifunze kuwa mbunifu na wa tofauti Ili uweze kujipatia wateja wengi na wa haraka zaidi.
Kuna msemo mmoja unasema, "kama huwezi kufanya mambo makubwa, basi fanya mambo madogo kwa ukubwa".
Cha kuchukua hapa ni kwamba ili uweze kuongeza thamani kwenye huduma yako nawe utengeneze fedha nyingi unaweza ukafanya yafuatayo: unatakiwa uweze kujitofautisha na washindani wako, fanya kwa namna ya kipekee, fanya kwa sababu una mapenzi na jambo hilo!
Kwa ujumla kwa chochote utachoamua kuuza iwe ni bidhaa au huduma basi hakikisha unatafuta upekee wako uko wapi, ili uepuke kufanya mambo kikawaida!
Kumbuka hakuna anayepnda ukawaida! Hata wewe hupendi vitu vya kawaida!
Na pesa nayo haipendi ukawaida!
7. Fedha Haitaki Mipaka...
Kama unahitaji kutengeneza fedha nyingi kwenye maisha yako basi ondoa mipaka ya muda na eneo katika utoaji wa huduma itakayokusaidia uweze kutengeneza fedha!
Hii ni sawa na kusema endapo katika kazi unayofanya ikifika usiku unafunga duka au ofisi na unahudumia watu wa eneo ulilopo tu, basi huwezi ukatengeneza fedha ya kutosha!
Unatakiwa ufanye mpango wa kupanua biashara yako ili iweze kufika mbali zaidi!
Hivyo basi kama unafanya biashara hakikisha biashara yako inauwezo wa kukuingizia fedha aidha asubuhi, mchana na hata usiku!
Mbali na hilo huna budi kujifunza jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii ili kufikia wateja wengi pamoja na kuwa na Blogu au website!
7. Fedha Inaheshimu Sana Maarifa Na Taarifa...
Kile unachojua ndicho kitapima kiwango cha fedha utakachotengeneza!
Amini usiamini utofauti mkubwa kati ya matajiri na masikini haupo kwenye mali wanazomiliki kwa maana mali hizo zinaweza kutoweka muda wowote, bali upo kwenye vile wanavyovijua.
Unatakiwa kujua kwamba matajiri wanawashinda maskini kwa sababu wanajua mambo mengi ukilinganisha na watu maskini!
Kile kinachoingia kichwani (kama taarifa) hupima kile kitakachotoka (matokeo), hii ni sawa na kusema kama utaingiza taarifa sahihi, utaweza kutengeneza fedha nyingi!
Mpenzi Unatakiwa uweke malengo juu ya kutafuta maarifa katika maeneo kadha wa kadha! Kwa mfano unaweza ukapanga ni vitabu vingapi unataka Usome, ni ujuzi gani unataka ujifunze ambao utakuongezea thamani n.k
Unatakiwa uweke akilini mwako kuwa moja ya eneo nyeti sana, unalopaswa kuliazimia malengo ni eneo la kutafuta ujuzi wa digital marketing skills, ujuzi wa kuwasiliana, pamoja na ujuzi wa kutengeneza mtandao wa watu.
Hata hivyo endapo wewe u mfanya biashara unahitaji ujuzi wa copywriting na closing skills!
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!
Mwendelezo Wa Somo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e, Mwl Mwandishi Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 0744285329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment