Huwezi Kufahamu Uwezo Uliozaliwa Nao Mpaka Usome Kwanza Hii..
Hivi unafahamu kuwa kila mwanadamu ndani yake anamiliki uwezo mkubwa sana aliozaliwa nao, ili umsaidie katika kuishi kwake hapa duniani?
Kwa mujibu wa tafiti za kisaikolojia kuwahi kufanyika zimeonesha kwamba, hakuna binadamu anayezaliwa akiwa hana uwezo fulani ndani yake (hazina), bali kila binadamu huzaliwa na uwezo asilia ambao Mungu alimuumbia ili umsaidie katika kuishi kwake hapa duniani...
Hata hivyo, kinachosikitisha na kushangaza zaidi ni pale unakuta watu wengi ambao wanamiliki uwezo huo ndani yao hawajui kabisa kuhusu hili, huku wengine wakiwa hawajui kabisa kuwa ndani yao kuna hazina kubwa sana ambayo, endapo ingetumika basi ingebadili kabisa hali za maisha yao. (Yaani hali za kiuchumi, kijamii pamoja na kitaifa kwa ujumla wake )
Ukiachilia hilo, moja ya sababu ambayo huwafanya watu hawa washindwe kugundua uwezo wao ni kutokana na mifumo iliyowatengeneza!
Hata hivyo, ukichimba ndani zaidi katika ulimwengu wa saikolojia, mifumo hii hufamika kama archetypes (yaani mifumo tambulishi).
Archetypes ni nini labda! ...Kwa tafsiri nyepesi archetypes huwa ni mifumo fulani inayomfanya mtu awe vile alivyo. Architype ni jumla ya tabia zote ulizonazo yaani utambulisho wako (character yako)
Kama hilo halitoshi, baadhi ya mifumo ambayo humtengeneza mtu na kumfanya awe vile alivyo ni kama vile: mazingira aliyopo, elimu aliyoipata, utamaduni, malezi, jamii inayomzunguka (marafiki, ndugu na jamaa) , uhalisia, jinsia, upekee, mfumo wa elimu pamoja na kuishi kwa mazoea.
Unajua nini hutokea? Mara baada ya kuishi kwa kufuata mifumo hiyo kwa muda mrefu, basi mifumo hiyo hukutengeneza na kukujengea uhalisia fulani usio kweli. Nawe pasipo kujua hujikuta unajikubali na kuridhika na hivyo ulivyo, matokeo yake unaishia kutokugundua uwezo uliozaliwa nao!
Hii ni sawa na kusema, utaanza kujiona kwa kutumia angle ya mifumo iliyokutengeneza, na endapo itatokea uwezo wako utakuwa nje na vile mifumo ilivyokutengeneza basi hutaweza kabisa kuutumia uwezo huo badala yake utakuwa unaishi kimazoea tu!
Ni sawa na shuleni ambapo unakuta mwanafunzi anapimwa kwenye maeneo mawili tu ya uwezo; yaani uwezo wa kuhesabu (Mathematical intelligence) pamoja na uwezo wa kuzungumza (verbal intelligence).
Na, endapo itatokea atafeli ataonekana kama ni mjinga sana na mpumbavu wa mwisho wakati hajapimwa kwenye eneo la uwezo wake!
Hii ni sawa na kumpima samaki kwenye uwezo wa kukwea miti badala ya kumpima mwenye uwezo wake wa kuogolea!
Na, ndiyo maana watu wengi ambao wamefeli shule hujiona wao siyo kitu, na hawawezi wakafanya mambo makubwa kitu ambacho hii kweli kabisa, hali hii imeua kabisa mpaka ule uwezo waliozaliwa nao na hii ni kutokana na dharau walizofanyiwa na wanafunzi wenzao pamoja na kauli walizoambiwa na walimu wao!
Rafiki unatakiwa kujua kwamba shule ilishindwa kutambua uwezo uliopo ndani yako, na kukufanya ujione wewe ni mpumbavu na mjinga kitu ambacho siyo kweli kabisa!
Sijui kwanini unasoma makala hii fupi, lakini ngoja nikuhakikishie kuwa, ndani ya muda mfupi ujao utaenda kugundua uwezo uliolala ndani yako pasipo kutumika.
Unachopaswa kufahamu ni kwamba ndani yako unamiliki uwezo mkubwa sana ambao endapo utaamua kuutumia utavuta mafanikio maishani mwako na utapata kila unachohitaji..
Katika sehemu hii utajifunza kuhusu uwezo mkubwa sana unaoumiliki ndani yako, lakini umebaki umelala tu bila kutumika..
Nimekuombea kwa Mungu ili ukimaliza kusoma makala hii ugundue uwezo wako, hata hivyo sitapendezwa kuona ukiiishia tu kugundua uwezo wako lakini nitapendezwa zaidi endapo utatumia uwezo huo utakaougundua.
FAHAMU KUHUSU TAFITI ZILIZOFANYIKA KUHUSU MAENEO KUMI YA UWEZO AMBAO KILA BINADAMU HUZALIWA NAO
Charles handy pamoja na Howard Gardner mwaka 2012, walifanya utafiti uliolenga kuchunguza uwezo ambao kila mwanadamu huzaliwa nao...
Kwa mujibu wa utafiti huo, maeneo kumi ya uwezo ambao kila binadamu huzaliwa nayo yalipatikana...
Sijajua kama tayari unautambua uwezo uliopo ndani Yako, lakini kwa leo nitachambua uwezo wa eneo moja tu, halafu maeneo mengine tutakutana kwenye makala zijazo Mungu akijaalia!
1. UWEZO WA KUZUNGUMZA (Verbal Intelligence)
Hawa ni watu ambao huwa ni wazuri sana katika kuzungumza na wanajua kutumia lugha kimamlaka.
SIFA ZAO...
➡️wanaelezea mambo kwa kina sana, wanapenda sana kufundisha, wanapenda sana kuandika mada mbalimbali na wana uwezo mkubwa wa kugundua makosa katika maandishi,
wanapenda sana kusoma, kuandika pamoja na kujifunza,
➡️ vilevile watu hawa, wanapenda sana kusimulia mambo, hupenda kusimulia stori mbalimbali kwa undani na kwa mpangilio mzuri yaani kuanzia mwanzo wa kisa hadi mwisho wa kisa..
➡️kama hilo halitoshi watu wanaomiliki uwezo huu, hupenda kusimulia vitu walivyosoma kwa undani na kama ameshiriki katika tukio fulani basi atakusimulia kwa ufasaha mpaka utajihisi kama umelishiriki tukio hilo.
➡️mwisho na kwa umuhimu, watu hawa ni wazuri sana katika kutumia: methali, nahau, maneno mbalimbali pamoja nukuu zilizosemwa na watu mbalimbali.
Na, Wanaamini kwamba kadri unavyojua maneno mengi ndivyo unavyozidi kuongeza ulinzi kwako kwani kwao maneno yao mengi ndiyo silaha yao.
Hata katika jamii utagundua kwamba watu hawa huwa wanatumia maneno yao kuweza kuchochea na kuhamasisha umma ufanye jambo fulani..
KAZI WANAZOWEZA KUFANYA WATU WANAOMILIKI UWEZO HUU!
✔️ Uanasiasa
✔️ Uandishi
✔️Utangazaji
✔️ Huduma kwa wateja (customer Care)
✔️Mwalimu
✔️Mwigizaji
✔️Mshehereshaji
✔️ Mhubiri
✔️Mhariri. N.k
NB: niliyeandika ujumbe huu ninamiliki uwezo huu! Sunaona ulivyoshuka na makala hii mwanzo Mpaka mwisho, mpaka ukatamani niendelee!
Mimi naishia hapa buana! Kesho tutaendelea na eneo la pili la uwezo Mwenyezi Mungu akijaalia!
Hata hivyo endapo unajiona unamiliki uwezo huu, hapo juu nimekutajia na kazi unazoweza kuzifanya!
Kwa msaada zaidi nitext inbox, kwa maana nipo hapa kwa ajili Yako!
Na, kabla hujaweka simu yako chini jaribu kuvuta picha kiwango cha fedha kinachotengenezwa na hawa watu wanaouishi uwezo wao yaani: waandishi, walimu, wanasiasa, waigizaji, washehereshaji pamoja na watoa huduma kwa wateja!
Bila shaka ni kiasi kingi ee... hata wewe unaweza kuwa kama wao endapo utagundua uwezo wako!
Kwani kipimo halisi kwamba unaweza ukafanya jambo fulani ni kwa sababu wengine wameweza kufanya jambo hilo!
Ahsante Sana Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No +255744284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment