Huwezi Kugundua Uwezo Uliozaliwa Nao Mpaka Usome Kwanza Hii....

Habari yako rafiki! Ni matumaini yangu u mzima wa afya! Kwa upande wangu namshukuru Mungu niko vizuri na ninaendelea vyema kabisa!

Karibu kwenye mwendelezo wa somo letu linaloangazia uwezo wa maeneo kumi ambayo kila binadamu huzaliwa nao! 

Kama unakumbuka vizuri, makala iliyopita ilidokeza hoja moja ya eneo la uwezo! Hii ni sawa na kusema, makala hii ni mwendelezo wa makala iliyopita!

Kwa leo utaenda kuoneshwa uwezo mwingine wa maeneo matatu ambayo kila binadamu huzaliwa nao!
Angalizo: unaposoma maeneo haya ya uwezo, uwe unahusisha na maisha yako ili utambue unamiliki uwezo gani!
Ukishatambua eneo la uwezo wako kwa msaada zaidi nitafute nami nitakupa mawili matatu juu ya kipi unatakiwa ufanye!
Karibu sasa kwenye uchambuzi wa maeneo mengine matatu:-

2. Uwezo Wa Kuchezesha Viungo Vya Mwili (Bodly kinetisthetic)/ (body smart)

Hawa ni watu ambao wana uwezo wa kutumia viungo vya mwili pamoja na mijongeo ya kimadaha...

Bila shaka katika kuishi kwako, umekutana na wanamichezo mbalimbali.
Na, huenda hata wewe ni mwanamichezo na unapenda sana michezo fulani fulani.

Endapo utakuwa unapenda sana michezo, basi yawezekana hata wewe unamiliki uwezo huu kwa sababu hatupendi vitu pasipo sababu!

Kwa ujumla tunaweza kusema kwamba, wanamichezo wote unaowajua wewe wanamiliki uwezo huu!

SIFA ZAO
➡️wanapenda sana michezo, mazoezi na kama ni watoto wanapenda kukimbizana..
➡️Wanapenda sana kutembea tembea huwa hawasimami sehemu moja. Hata akiwa ofisini huwezi kumkuta akiwa ametuliaa..
➡️Wanapenda sana kuzungumza Kwa kutumia ishara mbalimbali...
➡️Akiwa anazungumza utamkuta akiwa anashika vitu vilivyopo eneo hilo...
➡️wanajifunza kwa vitendo na wanapenda kufanya matendo kuliko maneno.
➡️ wanapenda kuchunguza vitu vinafanyeje kazi..
➡️ wanapenda sana kugusa akiongea na wewe lazima akuguse.

KAZI WANAZOWEZA KUFANYA WATU WANAOMILIKI UWEZO HUU
👉 wanamichezo
👉waigizaji
👉madansa
👉kocha wa timu
👉fundi simu
👉mtengeneza vitu vya mikono (msusi, mfumaji n.k)
👉 mfanayakazi mbuga za wanyama n.k

 3. Uwezo wa kimuziki ( Musical Intelligence)

Huu ni uwezo kutunga nyimbo pamoja na kuimba kwa sauti nzuri kama kinanda...

Unatakiwa kujua kwamba siyo kila anayetoa sauti huwa anaimba, kuna watu ambao wako talented kiasi kwamba akiimba hata mbingu zinaweza zikafunguka! 

Endapo una sauti nzuri na unapenda sana kuimba basi huenda unamiliki uwezo huu, ila kutokana na kukosa taarifa sahihi umejikuta ukijiuza kwa hasara na kutokutumia kabisa uwezo huu! 

Hata hivyo, ukichimba ndani zaidi utagundua kwamba karibu kila mtu kaumbwa na uwezo huu ndiyo maana kila mtu ana sauti ya kipekee..

SIFA ZAO
➡️Wanapenda sana kupiga miluzi..
➡️Wanapenda sana muziki kuliko kitu chochote kile...
➡️Wanapenda kuimba imba muda mwingi..
➡️Wanasifia sana muziki na tungo mbalimbali.
➡️Wanaweza kutumia vifaa vya muziki kirahisi..
➡️Wanapenda kujitungia nyimbo wenyewe..
➡️Wanagundua sauti za watu haraka hata kama hawajawaona..
➡️Wanajua sana kugundua waimbaji kwa kupitia sauti zao..
➡️Wanajifunza kwa kusikiliza zaidi kuliko kusoma..
➡️Wanakariri sana mashairii ya nyimbo, na wanaweza kukariri nyimbo kama ilivyo na kuimba nyimbo yote.
➡️ Mwisho na kwa umuhimu mtu anayemiliki uwezo huu, asiposikiliza muziki siku hiyo kwake mambo hayaendi kabisa..

KAZI WANAZOWEZA KUFANYA WATU WANAOMILIKI UWEZO HUU!
▪️Mwimbaji..
▪️Dj mixer
▪️Meneja wa msanii
▪️Muandaa matamasha ya muziki..
▪️Mtunzi wa nyimbo.
▪️Muaandaa muziki (producer)
▪️Mtaalamu wa vyombo vya sauti za muziki..
▪️Mwalimu wa muziki
🔹Promota wa muziki..
▪️muimba kwaya n.k

 4. Uwezo wa kuhesabu (mathematical intelligence)

Huu ni uwezo wa kuweza kusoma namba kwa haraka na kujua kile namba zinamaanisha...

Mbali na hilo eneo hili linahusu uwezo wa kujua na kucheza na namba katika maeneo manne yaani: kujumlisha, kutoa, kugawanya pamoja na kuzidisha! 
Unachopaswa kufahamu ni kwamba siyo kila mtu ni bora katika uwezo huu.

Ukweli ni kwamba, kama humiliki uwezo huu ni ngumu sana kufanya vizuri kwenye hesabu.
Na, ndiyo maana watu wengi hawafanyi vizuri kwenye Somo la hesabu. 
Unatakiwa kujua kwamba, watu hao siyo wajinga au wapumbavu kwa kuwa wanafanya vibaya, bali wanafanya vibaya kwa sababu hawajazaliwa na uwezo huu!

SIFA ZAO 
➡️Wanapenda sana hesabu..
➡️Wana uwezo wa kufanya hesabu kichwa kichwa na kupata majibu sahihi..
➡️Wanapenda kuweka vitu katika makundi makundi.
➡️Wanapenda zaidi kutumia data zinazoambatana na maelezo ya kisayansi..
➡️Huongozwa zaidi na akili kuliko hisia.
➡️Wengi wao huwa hawapendi kufanya vitu mpaka pale watakapojiridhisha kwamba sasa naweza kufanya (perfectionist)
 ➡️Wanapenda kutumia muda mwingi wakiwa pekee yao pamoja na kujiuliza maswali mbalimbali..

KAZI WANAZOWEZA KUFANYA WATU WANAOMILIKI UWEZO HUU!
🔹Mhasibu.
🔹Daktari
🔹Mtafiti.
🔹Mwandishi 
🔹Mwanasheria.
🔹IT/ mtaalamu wa kompyuta. N.k

Bila shaka kati ya maeneo hayo matatu ya uwezo wa kuzaliwa nao, kuna eneo la uwezo upo!
Endapo ushaligundua eneo lako la uwezo unachopaswa kufanya ni kutafuta taarifa sahihi pamoja na maarifa ya kutosha ili uweze kutumia uwezo huo ukunufaishe!

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!
Mwendelezo Wa Somo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant! 

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No +255744284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com 

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...