Sababu Kuu Tatu Kwanini Unatakiwa Usome Ujumbe Huu...

 
Habari yako rafiki! Ni matumaini yangu u mzima wa afya! Kwa upande wangu namshukuru Mungu niko vizuri na ninaendelea vyema kabisa!

Karibu kwenye mwendelezo wa somo letu linaloangazia uwezo wa maeneo kumi ambayo kila binadamu huzaliwa nao! 

Kama unakumbuka vizuri, makala iliyopita ilidokeza hoja tatu za maeneo uwezo! Hii ni sawa na kusema, makala hii ni mwendelezo wa makala iliyopita!

Kwa leo utaenda kuoneshwa uwezo mwingine wa maeneo matatu ambayo kila binadamu huzaliwa nao! Na huu ndiyo utakuwa mwisho wa maeneo yote kumi!

Karibu sasa kwenye uchambuzi wa uwezo wa maeneo matatu ya mwisho kabisa:-

 8. Uwezo wa ushawishi (interpersonal Intelligence)...

Huu ni uwezo wa kushawishi, kuwasiliana, kusihi, kutuliza migogoro pamoja na kuunganisha watu.

Kuna watu ambao wao wana uwezo mkubwa sana wa kushawishi watu na popote wanapopata kupita huwa wanakubalika sana kutokana na ushawishi wao..

SIFA ZAO.
➡️Wanapenda sana kuzungumza...
➡️Wanatengeneza marafiki kirahisi sana.
➡️Wanajali sana hisia za wengine..
➡️Ni wahudhuriaji wazuri wa semina  na kila tukio...
➡️Wanapenda sana kufundisha watu... 
➡️Wakipata maarifa kidogo tu huwa wanatafuta sababu ya kuwafundisha wengine..
➡️ Wanapenda sana kupatanisha watu pamoja na kuhamasisha umoja.

KAZI WANAZOWEZA KUFANYA WATU WANAOMILIKI UWEZO HUU!

🔹Mwanadiplomasia
🔹Kiongozi/meneja
🔹Afisa ustawi wa jamii
🔹Mhudumu kwa wateja
🔹Mtu wa mauzo
🔹Mshauri
🔹Dalali
🔹Kufundisha watoto
🔹Mwanasiasa mzuri

 9. Uwezo Wa Kiudadisi (Intuitive intelligence)

Huu ni ule uwezo wa kujua vitu pasipo kujifunza..
Yaani hapa mtu unakuwa una uwezo mkubwa sana wa kudadidisi mambo na kuja na majibu mbalimbali juu ya masuala hayo..

Mbali na hilo uwezo huu humsaidia binadamu kujua mema na mabaya..

Hata hivyo uwezo huu humsaidia mtu kuwajua watu vizuri pamoja na kuja na majibu kuhusu Kwanini watu hao wako hivyo..

Kadhalika, uwezo huu ndiyo huwasaidia sana wanasaikokolojia ambao wanaweza kumtambua mtu kwa muda mfupi yaani kuanzia tabia zake mpaka utambulisho wake kwa ujumla...

Actually huu uwezo huwa nautumia sana nikiwa natafuta majibu ya baadhi ya maswali kuhusu vitu mbalimbali.

Kwa mfano naweza kujiuliza; hivi hapa duniani kama tusingeishi kutafuta pesa tungeishi kutafuta nini?

Au naweza kujiuliza, "Kwanini Mungu alitupa mamlaka ya kuitawala dunia lakini kuna watu wanatawala watu wengine/nchi zinatawala nchi nyingine?"

Au naweza kujiuliza, hivi maisha yetu yako wapi labda, na kwanini tupo tunaishi hapa duniani tukiwa huru tu, huku tukiwa tunafurahia maisha...

Uwezo huu umeniwezesha kuanza kutengeneza falsafa zangu, siku moja nitakuja na orodha ya falsafa hizo! 

KAZI WANAZOWEZA KUFANYA WATU WANAOMILIKI UWEZO HUU.

➡️Mwanafalsafa mzuri.
➡️Mwalimu mzuri.
➡️Mshauri.
➡️Mwandishi mzuri
➡️Mwanasaikolojia mzuri.

 10.Uwezo Wa Kimaono (Abstract Intelligence)

Huu ni uwezo unaopatikana kupitia maono. Hapa mtu anakuwa anaona jambo fulani lijalo huko mbeleni kupitia maono..

Kwa mfano wanasayansi wengi walitumia uwezo huu na bado wanaendelea kuutumia katika kufanya ugunduzi wa kisayansi.. 

Hii ni sawa na kusema, wakilala usiku huweza kuletewa majibu ya formula mbalimbali zilizokuwa zinawapasua vichwa, kwa hiyo akiamka asubuhi anarekodi halafu ugunduzi unakuwa umekamilika!

Mbali na hilo baadhi ya viongozi wa dini wanamiliki uwezo huu (siyo wote)!

Wanaweza wakaona jambo fulani kupitia maono halafu jambo hilo likaja kutokea kama lilivyoonwa!

Unatakiwa kujua kwamba vitu vingi hapa duniani huanza kutokea katika ulimwengu wa roho ndipo sasa hudhihirika katika ulimwengu wa kawaida..

Pia, Unatakiwa kujua kwamba Kwamba karibu kila kinachotokea duniani huanza kama maono kwanza, ndipo sasa huja kutokea kama kitu halisi! 
Hii inamaanisha hata wale watabiri wa masuala mbalimbali hutumia uwezo huu.

Habari njema ni kwamba hata wewe unamiliki uwezo, ndiyo maana unaweza ukaona baadhi ya matukio yajayo kwenye maisha yako na yakaja yakatokea kama ulivyoyaonaa..

Hii ni sawa na kusema akili yako inaijua kesho yako endapo utaamua kuwekeza katika kutumia uwezo huu...

KAZI WANAZOWEZA KUFANYA WATU WANAOMILIKI UWEZO HUU!
➡️Nabii
➡️Mtabiri mzuri
➡️ Mwandishi
➡️ Mhubiri n.k

Kwa ujumla, ni vyema ukafahamu uwezo wako uko wapi ili uweze kutumia uwezo huo katika kuishi kwako hapa duniani!

Unatakiwa kujua kwamba endapo hutajua eneo la uwezo wako, utakuwa ni kama mtumwa kwa sababu utakuwa unafanya mambo nje na eneo la uwezo wako!

Unachopaswa kufanya mara baada ya kugundua uwezo wako ni kutafuta taarifa sahihi, maarifa na mbinu zitakokusaidia uweze kuuishi uwezo wako pamoja na kunufaika nao!

Ikumbukwe wajibu wangu mimi ni kukuonesha tu ila sikuamuru ufanye nini!

Kwa sababu hayo ni maisha yako na wewe ndiyo kifaa cha uzalishaji wa maisha yako! 
Hii ni sawa na kusema, unaamua! Unachagua!

Kwa ushauri zaidi karibu inbox, tuzungumze mawili matatu kuhusu wewe!

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No +255744284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com 

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...