Fahamu Kuhusu Fikra Ambazo Humuendesha Mwanadamu Aidha Afuje Fedha Zake Au Awekeze Pindi Akitengeneza Pato...


Jambo la kwanza unalopaswa kujua ni kwamba hakuna binadamu ambaye huzaliwa akiwa na Fikra fulani, bali kila mtu amekuwa na mtizamo wa kuona mambo kwa namna fulani kutokana na yeye alivyo pamoja na namna alivyozoeshwa!

Mbali na hilo unatakiwa kujua kwamba hivyo ulivyo, hapo ulipo pamoja na hali uliyonayo kiuchumi ni kutokana na wewe mwenyewe!

Hivyo basi kabla sijaenda mbali zaidi somo la leo ngoja tufafanue vipengele vifuatavyo, ni matumaini yangu kwamba vitapanua uelewa wako...

 Fikra: ni ile namna ya kufikiri,  hali ya kutizama na kuyaona mambo kwa namna fulani fulani hivi pamoja na kuyapa tafsiri kutegemeana na vile ulivyoyaona...

Uwekezaji: ni mfumo utakaokusaidia uweze kuzalisha pesa zako na kuzifanya ziwe nyingi zaidi!

 Aseti (Mali): ni kile kitu ambacho thamani yake inazidi kuongezeka kadri muda unavyozidi kusonga mbele... 
Au
 Aseti: ni kitu ambacho kinaingiza pesa mfukoni mwako! Hii inamaanisha aseti inafanya pesa iendelee kuongezeka mfukoni mwako!

 Liability (dhima): ni kile kitu ambacho thamani yake inazidi kushuka kadri miaka inavyozidi kuongezeka!
Au
 Liability: ni kile kitu ambacho kinatoa fedha mfukoni mwako kila iitwapo leo!

Hii inamaanisha  endapo utakuwa ni muumini wa kununua liability utakuwa ni sawa na kuufanya utajiri uote mabawa na kukukimbia huku ukiukaribisha umaskini maishani mwako!

Je mpaka hapa wewe ni mfuasi wa kununua aseti au liability!

Tuendelee na somo kwa kuangalia mambo matatu ambayo watu hufanya wakipata fedha!

Tumia mambo haya kujipima kama una fikra za uwezekezaji au una fikra ufujaji...

1. Fikra  Za Ufujaji Pesa!

Ni jambo ambalo hufanywa na watu wengi wasio na busara!
Hapa mtu anakuwa hana mpangilio wa manunuzi bali ananunua kila anachokiona...
Hawa ndiyo wale watu ambao wakishika pesa huwa zinakuwa ni kama zinawawasha!

Yaani wanakuwa wanaendeshwa na pesa mwisho wa siku wanajikuta hawafanyi kitu cha maana kwenye pato walilotengeneza..

Je wewe ni mfujaji? Je ukipata fedha kitu cha kwanza huwa unawaza ufanyie nini?
Ndugu Unapaswa kujua kwamba kuna kesho inakuja ambayo huijui!

Kuna kesho inakuja ambayo hata uwezo wa kufanya kazi hutakuwa nao!

Kuna kesho inakuja ambayo uwezekano wa kutengeneza fedha kama leo hautakuwa nao!

Je unajipangaje kwa ajili ya kesho yako?

Tambua kwamba fedha unayoingiza leo ndiyo mbegu yako ya kesho!
Ndiyo maana wahenga walisema akipandacho mtu ndicho akivunacho!

Je unapanda nini kwa ajili ya kesho yako?

2.  Fikra Za Kutumia Pesa!

Hapa ni pale mtu anapotumia fedha zake zote kwenye masuala ambayo huonekana ni ya msingi kwa upande wake huku akiathiri kesho yake!

Watu wanaondondokea kwenye kufanya tabia hii ni wafanyakazi! 
Watu hawa hujikuta wakitumia pato lao lote kwa kulipa Kodi, kulipa ada, bili pamoja na matumizi mengine, na pengine labda huona kufanya hivyo ni sahihi, vilevile watu hawa ni waamini wazuri wa ule usemi usemao; "fedha ilitengenezwa ili itumike" 

Hata hivyo mbali na kuwa hufanya matumizi sahihi lakini kosa lao ni moja tu, huwa wanatumia fedha zote pasipo kuwekeza hata shilingi mia!

Ndugu mtu mwenye busara anajua kwamba kuna kesho inakuja!

Je wewe nawe upo kwenye kundi la kutumia tu pasipo kuwekeza?

Huna budi kujiandaa na kujipanga kwa ajili ya kesho yako!

Rafiki, nimalize kwa kusema; "jiandae kwa wakati ulio mbaya, nawe daima utakuwa na wakati ulio mzuri"

Kaa ukiwa umejiandaa kwani muda wowote ule lolote lile linaweza kutokea! 

3. Fikra Za Kuwekeza Pesa!

Hii ni tabia ambayo hufanywa na watu wachache sana!

Hapa mtu anakuwa ametambua kwamba kuna kesho inakuja!

Hivyo basi anaamua kuchukua sehemu ya pato lake na kuiwekeza kama mbegu ya kesho yake iliyo njema! 

Unatakiwa kujua kwamba hakuna atakayekupangia kesho yako pasipo uhusika wako mwenyewe!

Ndugu unatakiwa kujua kwamba kitengo cha uchumi katika maisha yako kinakutegemea wewe!

Hivyo ukishindwa kuwekeza utakifanya kitengo hiki adimu kife!

Wekeza pesa zako!

Hautakiwi kuishia tu kuwa mfujaji au mtumiaji bali kuwa mwekezaji!

Mtu mwenye busara huwekeza PESA zake kwa sababu anatambua kwamba kuna Kesho inakuja!

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e: Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No  +255744284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com 

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...