Onyo! Hata Usifikirie Kuhusu Kubadli Hali Yako Ya Kifedha Mpaka Usome Kwanza Hii...
Hivi unafahamu kwamba mafanikio katika eneo lolote lile maishani mwa binadamu huanzia kichwani mwake?
Katika hali ya kawaida huwezi ukapata kitu ambacho kichwani mwako hujakiwazia au hata kufikiria kwamba utakipata!
Hii ni sawa na kusema, watu wengi hatufanikiwi KIFEDHA kwa sababu hatuna fikra za uwezekezaji!
Ukichimba kwa undani utagundua kwamba, kitu kilichopo vichwani mwetu ni ile dhana ya kudhani, fedha ilitengenezwa ili ije itumike tu!
Huku ukweli kuhusu fedha ukiwa ni ule unaodai kuwa, fedha ilitengenezwa ili ije iwekezwe au izalishwe!
Kwa mantiki hiyo endapo itatokea huizungushi fedha yako au hujaiwekeza huwezi kutengeneza fedha nyingine hali ambayo itakufanya ushindwe kufanikiwa kufedha!
Siyo kwamba watu wote wanapenda kutokuwekeza fedha zao ili zijilizalishe, bali wengi wetu tumejikuta tukifanya hivyo kutokana na sababu mbalimbali, huku sababu yenye mashiko zaidi ikiwa ni athari ya malezi tuliyokutana nayo.
Tafiti za kisaikolojia kuwahi kufanyika zimeonesha kwamba, mwanadamu hukua kwa kuiga kile ambacho watu wanaomzunguka wanakifanya.
Hii ni sawa na kusema wengi wetu tumeathirika katika eneo la fedha kutokana na aina ya malezi tuliyofanyiwa.
Kwa mfano wengi wetu tunatokea kwenye zile familia ambazo wazazi wetu hawakuwa wawekezaji au wafanya biashara!
Kutokana na hilo inakuwa ngumu kuwa na maamuzi sahihi kuhusu fedha pamoja na kutokuelewa tabia halisi za fedha!
Unatakiwa kujua kwamba moja ya eneo nyeti sana ambalo mtoto huanza kujifunza kuhusu fedha ni katika ngazi ya familia, kwa hiyo endapo msingi wake hautakuwa imara itakuwa ngumu sana kwa mtoto huyo kukua akiwa na uelewa mpana kuhusu fedha!
Wengi tumejitengenezea ile mentality ya kuona kuwa, fedha ilitengenezwa ili ije itumike tu, kwa sababu wazazi walitufundisha hivyo na walikuwa wanafanya hivyo!
Hebu jaribu kurudisha kumbukumbu nyuma enzi za utoto wako. Kwa mfano ilikuwa ikitokea umepewa fedha aidha na ndugu au jirani kitu cha kwanza kilichokujia akilini mwako kilikuwa ni kuwaza ukanunue nini kutokana na ile fedha ulopewa!
Matokeo yake ukajikuta ukikua hivyo. Hii ni sawa na kusema kila pesa uloshika uliwaza ukanunue kitu gani. Mpaka sasa huwa unafanya hivyo!
Kwamba ikitokea tu umetengeneza pato lako, huwazi ni kiasi gani cha fedha niwekeze bali unawaza namna utakavyoweza kutumia fedha yako!
Kitu kingine cha kuongezea hapa ni kwamba, ukitaka kuthibitisha kwamba wengi tunajua kuwa fedha ilitengenezwa ili itumike, jaribu kumpa mtoto mdogo fedha halafu angalia mwititikio wake, bila shaka atarudi kanunua something sweet sweet eee 🤣😂...
Mbaya zaidi ni kwamba umeendelea kukua kwa namna hiyo mpaka sasa unajikuta tu ukipata fedha, akili yako inakuletea orodha ya vitu pesa yako inaweza kununua, lakini haikuletei orodha ya miradi ambayo fedha yako inaweza kuwekeza!
Kutokana na hilo utajikuta unaitikia automatic katika kufanya manunuzi ambayo hukupanga kabisaa...
Ndugu hauhitaji KITU kingine zaidi ya kubadilisha FIKRA zako!
Unatakiwa ubadilishe fikra za kuona fedha kama kifaa cha kutumika tu na kuona FEDHA kama kifaa kinachopaswa kiwekezwe ili kikuzalishie fedha nyingine!
Katika makala hii fupi utajifunza jinsi ya kutengeneza FIKRA ZA UWEZEKAJI!
Fikra za uwezekezaji ni nini labda?
Kwa tafsiri nyepesi fikra za uwekezaji ni zile fikra ambazo zinalenga zaidi katika kuwezekeza fedha ili ijizalishe zaidi!
Unatakiwa kujua kuwa, mtu mwenye fikra za uwekezaji akishapata tu fedha wazo la kwanza linalomjia akilini mwake ni kuwaza miradi ambayo fedha yake inaweza kuwekeza, huku yule asiye na fikra za uwekezaji akiwaza ni namna gani ataenda kutumia fedha yake!
Hata hivyo huna budi kufahamu kwamba, endapo utaweza kutengeneza fikra za uwezekezaji utaweza kubadili kabisa hali yako ya kifedha!
Je nifanye nini ili niweze kutengeneza fikra za uwekezaji?
...usijalii makala hii imeandikwa kwa ajili ya hilo! Ili uweze kutengeneza fikra za uwezekezaji unatakiwa kufuta fikra Hatarishi kama zifuatazo:
1. Futa Fikra Za Kuhamahama (Nomadic Mentality)
Fikra za kuhamahama ni aina ya zile fikra ambazo hazijatulia! Yaani hapa unakuta mtu ukipata tu fedha unaanza kuwekeza kwenye miradi tofauti tofauti kwa kuhamahama.
Kwa mfano leo mradi huu, kesho mradi ule, keshokutwa mradi ule, pasipo hata kufanya tathmini maendeleo ya mradi uliopita mwisho wa siku utajikuta ukishindwa, hali ambayo itapelekea upotevu wa fedha yako!
Unatakiwa kujua kwamba, kufanikiwa kwenye uwekezaji kunakutaka uweze kuchagua eneo moja halafu ulitengenezee mfumo mzuri wa kuitawala fedha, kwani fedha hufuata mfumo ulioandaliwa kwa ajili yake!
Kitu unachopaswa kuondoka nacho hapa ni hiki; hukuumbwa uje ufanye miradi yote inayokuja mbele yako, na ukitaka kuwekeza kwenye kila mradi unaokuja mbele yako, utaishia kutokuwekeza chochote kile!
NB: kufanikiwa katika uwekezaji unatakiwa utulize akili zako katika eneo moja ulilochagua mpaka ufanikiwe!
You have to eradicate nomadic mentality!
2. Futa Fikra Za Matumizi (Consumer Mentality)
Hizi ni zile fikra ambazo hukuletea maeneo unayoweza kutumia fedha zako pindi tu ukitengeneza pato fulani!
Hii ni sawa na kusema endapo utatengeneza fedha mawazo yako yanakusukuma uzitumie zote mpaka ziishe, kwa kukuletea orodha kibao ya matumizi!
Kwa mfano kwa wale waajiriwa wenzangu unakuta hata mshahara wa mwezi huu haukutani na mshahara wa mwezi ujao! Huyo mtu anakuwa kazidisha matumizi kuliko pato analolitengeneza!
Na, endapo utamuuliza kama kuna cha maana alichofanyia fedha hizo hana, na huenda hana kumbukumbu yoyote juu ya namna alivyoitumia fedha yake!
Unatakiwa kujua kwamba, chanzo kinachopelekea hali hii ni fikra za matumizi (consumer mentality)
Ndugu unatakiwa ufute fikra za matumizi kichwani mwako! Na endapo utabaki nazo zitakuweka kwenye umaskini!
3. Futa Fikra Za Kuweka Visingizio!
Kuna watu ni wataalamu wa kuweka vizingizio, utafikiri wamehitimu shahada ya kwanza katika kitengo cha kuweka visingizio!
Unatakiwa kujua, endapo utakuwa ni mtu wa kuweka sana visingizio, kitakachotokea hapo ni kwamba vizingizio hivyo vitakupa haki na kukufanya ujione upo sahihi tu kutokufanya uwekezaji!
Kinachomaanishwa hapa ni hiki, hapa unakuta mtu anaweka visingizio vingi vinavyompa haki ya yeye kutokufanya uwekezaji!
Kwa mfano utamsikia mtu akisema, "sijawekeza kwa sababu mahitaji ya kifamilia yanaongezeka kila siku"
Mwingine anaweza kusema "Mimi sijaumbiwa kufanikiwa katika biashara"!
Huku mwingine akisema "sina muda wa kufanya biashara" n.k.
Ndugu Unapaswa kujua kwamba visingizio ni lugha ya kujifajiri na vitakufanya ujihesabie haki huku ukiharibu kesho yako!
4. Futa Fikra Za Kuwaza Kuhusu Mshahara (Salary Mentality)
Moja ya fikra hatari sana ambayo hutufanya wengi wetu tushindwe kutengeneza fikra za uwekezaji ni fikra kuwaza kuhusu mshahara!
Kitachotokea hapa ni kwamba, fikra hizi zitakupa ile hali ya kutokujali chochote kile kuhusu kufanya uwekezaji kwa sababu mshahara upo!
Utamsikia mtu akisema "kwanini nijitese wakati mwisho wa mwezi upo na nitapokea mshahara?"
Rafiki unatakiwa kujua kwamba, hizi ni moja fikra hatari sana ambazo humnasa mtu kwenye mtego!
Matokeo yake mtu huyo hujikuta akiingia kwenye mlolongo wa kuhesabia siku!
Na hapa ndipo utamsikia mtu akisema, "bado siku ngapi ili mwezi uishe?"
Kutokana na hilo atajikuta hawazi kabisa kuhusu kuwekeza bali atajikuta akiwaza apate mshahara ili aendelee kuutumia tena na tena na Tena.
Hii ni sawa na kusema maisha yake yote yanakuwa yanategemea mshahara!
NB: hakuna kitu kibaya kuhusu mshahara! Unatakiwa kujua kwamba mshahara hautakufanya ufanikiwe kifedha bali ni rasilimali unayopaswa kuwekeza ili uzalishe pesa nyingine zaidi.
5. Futa Fikra Za Uhaba (Scarcity Mentality)
Hizi ni fikra hatari sana, hapa mtu anaamini duniani hakuna fedha ya kumtosha kila mtu na kwamba siyo kila mtu kaumbwa kufanikiwa kifedha!
Awali nilishasema kwamba mafanikio huanzia kichwani! Hivyo basi endapo utakuwa na fikra za mtindo huu hutajishughulisha kabisa katika kuwezekeza!
Pia Unatakiwa kujua kwamba huwezi ukakipata au ukakivuta kitu unachokilaani/kukitaa kiwe sehemu ya maisha yako!
NB: Ili Ufanikiwe Kifedha unatakiwa ufute kabisa FIKRA ZA uhaba na kuona kila mtu anaweza kufanikiwa kifedha hata wewe hapo.
Ahsante Sana Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!
Mwendelezo Wa Somo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi, Muelimishaji, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No +255744284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment