Fahamu Kuhusu Sehemu Mbili Za Akili Na Jinsi Utendaji Kazi Wake Unavyopima Kila Kinachotokea Maishani Mwako…

Hivi unafahamu kuwa unamiliki akili moja ambayo hufanya kazi kwa kutumia sehemu kuu mbili tofauti za akili, huku utendaji kazi huo ukiwa ndiyo hupima kila kinachotokea maishani mwako?

Ukweli ni kwamba, watu wote wanamiliki akili, lakini ni watu wachache sana kati ya hao ndiyo wanajua jinsi gani akili zao zinafanya kazi! 

Laiti kama kila mtu angejua jinsi gani akili yake inavyofanya kazi, huenda tusingekuwa na dunia hii tuliyonayo sasa na huenda tungeishi maisha ya hadhi nyingine kabisa!

Makala hii fupi itaenda kudokeza jinsi akili yako hufanya kazi, na jinsi gani utendaji kazi huo huathiri kila kibnachotokea maishani mwako, ikumbukwe karibu kila kitu kinachotokea maishani mwako huanzia akilini mwako!

Mpenzi msomaji unatakiwa kujua kwamba unamiliki akili moja ambayo hufanya kazi kwa kuhusisha sehemu mbili tofauti za akili, na ufanyakazi wa sehemu hizo mbili huongozwa na kanuni ya kuamini.

Sehemu ya kwanza inaitwa Conscious Mind; hii ni sehemu ya akili ambayo huchukua dhana, wazo, fikra, taarifa au jambo lolote lile kisha huliamini kuwa lipo hivi ama vile, mara baada kuliamini, basi jambo hilo huchukuliwa kama ombi kisha hutumwa kwenye sehemu ya pili ya akili!

Hata hivyo, sehemu hii ya akili hutumia milango ya fahamu katika uchukuaji wa taarifa hizo.

Kwa mfano tufanye unaambiwa: huwezi ukapona ugonjwa wako, unaumwa kwa sababu wewe ni mdhambi, huo ugonjwa ni wa Mungu mwenyewe hakuna wa kukuponya, utaishia kuwa maskini, huwezi kufanikiwa, hutopata kazi, N.k.

Basi kitakachofanyika hapo, akili yako itazichukua taarifa hizo na kuziamini. (kwa mfano unaweza ukaamini kuwa, ni kweli mimi nitaishia kuwa maskini)

Baada ya hapo, taarifa hizo zitapelekwa sehemu ya pili ya akili iitwayo Subconscious Mind!

Nini maana ya Subconscious mind; hii ni sehemu ya akili ambayo hupokea taarifa zitokazo kwenye conscious mind na kisha kuanza kuzichakata hadi kuleta Matokeo yanayoakisi kile kilichoaminiwa kuhusu taarifa hizo!

Unatakiwa kujua kwamba jambo lolote, au kitu chochote kile utakachokiwaza/kukifikiria kupitia conscious mind, basi subconscious mind hukipokea kama ombi na kuanza kuchakata na kukuletea matokeo yanayolandana na kile ulichoamini kuhusu jambo hilo

Ukweli ni kwamba subconscious mind ni sehemu ya akili ambayo huna mamlaka nayo, na hufanya kazi kwa kuongozwa na kanuni ya kuamini, haijalishi jambo hilo utakaloliamini litakuwa kweli au si kweli, itakakachofanya sehemu ya akili ni kulipokea jambo hilo kama ombi na kulichakata mpaka upate matokeo yanayoakisi kile ulichoamini kuhusu jambo hilo! 

Hata hivyo unatakiwa kujua kwamba utendaji kazi wa wa sehemu hizi mbili huongozwa na kanuni ya akili inayosema;
 “Subconscious mind itachakata oda, komandi, taarifa, na mawazo kama zilivyowasilishwa na kuaminiwa na conscious mind”

Msisitizo mkubwa upo kwenye conscious mind, kwamba unatakiwa kuwa makini na kile unachokiamini kwa sababu ukiliamini jambo kuwa lipo hivi, hata kama jambo hilo halipo hivyo, basi jambo hilo litawasilishwa kwenye subconscious nayo italichakata na kukupa matokeo yanayolandana na kile ulichoamini kuhusu jambo hilo!

Kumbuka kuamini ni kupokea kuwa jambo Fulani ni kweli hata kama jambo hilo halipo hivyo…

Na, ndiyo maana kanuni ya kuamini inasema kwamba; “chochote utakakachokiamini kuhusu wewe na dunia yako kitafanyika kwako na dunia yako kama uaminivyo”

Hii ni sawa na kusema, endapo utaaminishwa kwamba ugonjwa wako hautapona bali utateseka maisha yako yote, nawe ukaamini hivyo, basi subconscious mind itaruhusu na kukuletea matokeo yanayolandana na kile ulichokiwasilisha.  Mwisho wa siku hutapona, kwani umeamini kwamba hutopona.

Rafiki unatakiwa kuwa makini sana kwani kile unachofikiri na kukiamini, ndicho kitakachokutokea, kumbuka imani haijawahi kumsaliti muamini wake…

Ukweli ni kwamba hata uponyaji mwingi ambao watu hufanyiwa, hufanyika kwa kubadili mfumo wa imani wa subconscious mind!

Hii ni sawa na kusema hata wewe unaweza kutumia subconscious mind kujiponya au kutatua tatizo fulani!

Angalia mfano ufuatao wa mtu, niliyemhudumia mimi mwenyewe!

Jinsi Alivyojiponya Kwa Kutumia Conscious Mind Na Subconscious Mind…

Siku moja katika huduma yangu nilipata kumhudumia mzee mmoja ambaye alikuwa ameteseka kwa muda mrefu sana na ugonjwa, mzee huyo alikuwa amelazwa kwa muda mrefu sana na katika fahamu zake hakuwa na tumaini la kupona tena.

Nilipomuuliza kuhusu eneo la kiroho akanijibu kuwa yupo vizuri na anamjua Mungu vizuri tu, na huwa anasoma biblia kila siku.

Nilipoendelea kumuuliza maswali zaidi ndipo sasa nikagundua kwamba tatizo siyo ugonjwa bali tatizo ni kile anachokiamini kuhusu maradhi yanayomkabili…

Mzee huyo alikuwa ameiingiza imani potofu kwenye subconscious mind kuhusu maradhi yake, kwani aliamini kwamba hawezi kupona na anachosubiri yeye ni kifo tu, na aliona kama kifo chenyewe ni kama kinachelewa kuja kwani alikuwa ameteseka kwa muda mrefu sana na maradhi hayo. 
Akaona ni bora afe tu ili aepuke maumivu, ikumbukwe alikuwa akihisi maumivu makali mno. 

Jinsi Nilivotoa Fikra Hasi Iliyopo Kichwani Mwake Iliyopelekea Uponywaji Wake…

Kwanza nilianza kufafanua kuhusu uhusiano uliyopo kati ya conscious mind na subconscious mind na jinsi gani uhusiano huo hupima kila kinachotokea katika maisha yake.

Nilimwambia kwa kutumia conscious mind amejikuta akiamini katika imani potofu pasipo kujua kwamba kile anachokiamini kinawasilishwa kama ombi kwenye subconscious mind, na kwa sababu subconscious yenyewe huchakata na kuleta matokeo yanayolandana na kile kilichowasilishwa ndiyo maana hapokei uponyaji.

Yaani mbali na kuwa alikuwa anasali pamoja kusoma biblia, hakuweza kupokea uponyaji kwa sababu imani yake ilikuwa kwenye kutokupona na  si kupona tena!

Ikumbukwe alikuwa kaamini kwamba hawezi kupona, bali ataishia kuteseka maisha yake yote na hakuna kingine alichokuwa anakingoja zaidi ya kifo tu!

Hii inamaanisha kwamba kupitia kuamini hivyo, taarifa hizo ziliwasilishwa kwenye subconscious mind, mara baada ya kupokelewa subconscious mind ilichakata na kumletea matokeo yaliyosadifu imani yake, kwa hiyo akajikuta kadri siku zinavyozidi kwenda mbele hali yake inakuwa mbaya zaidi, ijapokuwa anasali sana pamoja na kusoma biblia!

Mzee huyu alijiadhibu mwenyewe kwa kuamini katika imani potofu…

Nini Nilimumbia Afanye?...
Nilimuambia kwamba hatua ya kwanza anayopaswa kufanya ni kubadilisha imani yake kwanza, kwani shida haikuwa ugonjwa, bali shida ilikuwa ni Mental Block ambayo aliiweka akilini mwake kutokana na kuamini katika imani potofu, kwa hiyo nilimuambia abadilishe kwanza imani yake pamoja na kuwasilisha picha nzuri akilini mwake ambazo zitaachilia uponyaji mwilini mwake…

Alipoelewa tu jinsi mfumo wake wa akili unavyofanya kazi akaamua kuachilia fikra potofu kichwani mwake na hiyo ndiyo ikawa pona yake. 

Kumbuka kile kilichojadiliwa kwenye Mathayo 18:19, kwamba wawili kati yenu lazima wapatane katika jambo hilo…

Hivyo basi aliamua kujipa uhuru kwa kuachilia fikra potofu na akajaza conscious mind na fikra chanya, nzuri, zilizomfanya ajione anastahili kupona na kuishi tena, na si kusubiri kifo kama alivyokuwa akidhani hapo awali.

Nikaumueleza kuwa kila siku asubuhi ahakikishe anatengeneza picha akilini mwake ikimuonesha yeye akiwa mzima tena, huku akiwa na afya njema na mwenye furaha na matumaini mapya…

Baada ya miezi mitatu alinijulisha kuwa kuna muujiza umetokea, nikamuuliza ni kipi hasa kimetokea akasema, kwamba ameshapona tayari na anajuta sana kwanini alikuwa anajiadhibu kwa kuamini katika imani potofu…

Nikamueleza kwamba kila siku aendelee kushikilia picha ikimuonesha yeye akiwa mzima, maisha yake yote.

Hivyo ndivyo hata wewe unaweza ukatumia conscious na subconscious mind kujiponya dhidi ya ugonjwa, au shida yoyote ile…

Toa imani potofu zote ulizoweka kichwani mwako kisha ujione ukiwa unaendelea vyema, kama ulikuwa umelazwa jione ukiwa unatembea, kumbuka hakuna kitu chenye nguvu kama picha hasa linapokuja suala la uchakataji. 

Unatakiwa kujua kwamba yule unayemuona ndiye utakayekuwa, hii inamaanisha ukijiona upo mzima nawe utakuwa mzima kwa sababu umejiona hivyo…
 
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant! 

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com 

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...