Tahadhari Huwezi Kumuabudu Mungu Katika Roho Na Kweli Mpaka Usome Kwanza Hii…

Hivi unafahamu kwamba siyo kila sehemu ambayo jina la Mungu linatajwa inamtangaza Mungu halisi?

Unatakiwa kujua kwamba, siku hizi kuna ongezeko la manabii wa uongo ambao wanatumia jina la Mungu ndivyo sivyo na kuwaongoza watu nje na ufalme wa Mungu.

2 Wakorintho 10:13-15 Neno la Mungu linasema; “Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.
Wala si ajabu. Maana hata shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawa na kazi zao”

Mpenzi msomaji kutokana na andiko hilo unatakiwa ujifunze kwamba, katika sehemu za ibada kuna watumishi wa shetani ambao wamejigeuza tu lakini kiuhalisia hawamtangazi Mungu wa kweli.

Na, na ndiyo maana katika injili ya Mathayo 7:15 Yesu anasema; “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwamwitu wakali”

Kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri utagundua ukweli wa andiko hili unavyojidhihirisha katika maeneo mbalimbali ambayo ibada zinafanyika.

Unatakiwa kujua kwamba unaposhiriki ibada zinazoongozwa na hawa wachungaji wa shetani, ndivyo unavyojitoa kwenye ile sehemu yako ya ufalme wa mbinguni na kujiunganisha kwenye ufalme wa shetani! 

Ukitaka kuthibitisha hili kasome injili ya Mathayo 23:13, ambapo Neno la Mungu linasema; “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki, kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie”

Hii ni sawa na kusema katika kipindi cha ujio wa Yesu mara ya kwanza wafausi wa Mafarisayo wote walikosa ufalme wa mbinguni kwa sababu ya kuwafuata na kuwasikiliza viongozi vipofu wa vipofu, waliokataa neno la Yesu na kutangaza neno la uongo wa shetani.

Unatakiwa kujua kwamba waamini hao hawakuweza kupima roho za Mafarisayo kama walikuwa ni wafuasi wa kweli wa Mungu na kama walikuwa wakimtangaza Mungu wa kweli!

Na, ndiyo maana katika kitabu cha Hosea 4:6, Neno la Mungu linasema; “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa mimi nami nitakukataa wewe…” 

Unatakiwa kujua kwamba maarifa yanayozungumziwa hapo, ni maarifa ya kulifahamu neno la Mungu kwa usahihi.
Na, endapo utaweza kuwa na maarifa ya Neno la mungu utaweza kupima roho za watu wote  wanaolitangaza jina la Mungu kama wanamtangaza Mungu halisi...

Kutokana na hilo ndiyo maana, 1 yohana 4:1 Neno la Mungu linasema; “Wapenzi msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwani manabii wengi wa uongo wametokea duniani.”

Ukweli ni kwamba utaweza, kuzipima roho za hao manabii kama utakuwa una maarifa ya Neno la Mungu. 

Siku hizi watu wengi wamekosa maarifa ya Neno la Mungu kwa sababu wamekuwa siyo wasomaji na hata hao wanaofundisha neno wamekuwa wakiongeza Mawazo yao binafsi kwenye neno la Mungu, hali ambayo imepelekea watu wengi washindwe kujua maandiko. 

Na, kwa vile hawajui maandiko ndiyo maana imekuwa rahisi sana kuweza kupotezwa na hawa manabii wa uongo.

Mathayo 22:29 “Yesu akajibu, akawaambia, mwapotea kwa vile hamjui maandiko wala uwezo wa Mungu”

Unatakiwa kujua kwamba kama hutojua maandiko utapotea sana…

Kwa kulitambua tatizo lako la kutokujua maandiko kwa usahihi lililokutesa kwa muda mrefu “KITUO CHA UMISHENI CHA SAYUNI, CHUO CHA BIBLIA”, kimekuandalia mafunzo ya biblia bure kabisa.

Katika mafunzo hayo utajifunza mafumbo yote ya biblia kuanzia kitabu cha mwanzo hadi kitabu cha ufunuo, baada ya hapo sasa ndipo utajifunza unabii uliopo kwenye kitabu cha ufunuo Pamoja na utimilifu wake…

Habari njema ni kwamba mafunzo haya yanatolewa bure kabisa. Ufunuo 21:6 “…mimi nitampa yeye mwenye kiu ya chemchemi ya maji ya uzima, bure”

Mafunzo hayo hutolewa kwa siku tatu kwa wiki, kwa njia kuu mbili, aidha kushiriki kwa kuhudhuria moja kwa moja darasani, au kushiriki mtandaoni kupitia zoom meeting.

By the way kama upo tayari kushiriki mafunzo haya, uonapo mwaliko huu, unachopaswa kufanya ni kuujibu kwa kuandika neno BIBLIA.

Au unaweza kuandika neno BIBLIA Kwenda WhatsApp no +255744284329 

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...