Akipandacho Mtu Ndicho Akivunacho...

Hivi unafahamu kwamba hivyo ulivyo pamoja na hapo ulipo ni mavuno uliyoyapata kutokana ya kile ulichokipanda katika maisha yako?

Huenda hata wewe umekuwa ni miongoni mwa wale watu ambao wamekuwa wakilaumu kuhusu hali ngumu wanazokumbana nazo kila leo, wasijue chanzo ni nini, kumbe chanzo ni wao wenyewe!

Unatakiwa kujua kwamba kile unachokifanya (kupanda) ndicho kinapima matokeo (mavuno) unayoyapata!

Kwa mantiki hiyo kama utapanda upepo utavuna upepo, kwa maana katika hali ya kawaida huwezi ukapanda mchele halafu ukavuna mahindi!

Ukweli ni kwamba kila mtu ana hulka ya kuwa na mafanikio pamoja na kuishi maisha yaliyojaa furaha, lakini ni watu wachache sana ambao huwa na utaratibu wa kupanda mbegu ambazo hupelekea mafanikio hayo!

Kutokana na hilo, ni watu wachache tu ndiyo hupata mafanikio, kwa sababu walipanda mbegu zilizopelekea mafanikio hayo, huku wanaosalia wakibaki kulalama na wengine wakijisemea ipo siku mambo yatakuwa sawa. Wasijue kwamba Mambo hayawezi kuwa sawa bila kuwekwa sawa!

Rafiki, wahenga walisema "utavuna ulichokipanda" kwa mantiki hiyo, usipopanda huwezi kuvuna kwa maana sharti la kuvuna ni lazima upande kwanza.

Sasa unapolia kuwa hali ngumu, sasa  unapolaumu kuhusu umaskini wako unataka kumaanisha kuna mtu alipanda mbegu zilizopelekea hali hizo maishani mwako?

Ukweli ni kwamba maisha yako ni juu yako na kila kinachotokea katika maisha yako ni juu yako na wewe mwenyewe ndiye umechangia kwa asilimia mia moja katika kutokea kwake, aidha kwa kujua au kutokujua au kwa kutaka ama kutokutaka!

Na, kama hujachangia basi kuna mtu alikuamlia nawe ukakosa chaguo, au kuna mazingira yamechagia hali hizo. Japo mazingira pamoja na msukumo wa nje huchangia kwa asilimia chache sana. Asilimia kubwa zipo kwako kwa maana ulipewa akili na uwezo wa kuitawala dunia yako!

Sasa basi badala ya kulaumu unatakiwa ukae kwanza chini na kujiuliza ni aina gani ya mbegu ulizipanda na umevuna nini! Na ni aina gani ya mbegu unazopaswa uzipande ili zikuletee matokeo tofauti na hayo uliyoyapata.

Kumbuka hakuna kitu ambacho hutokea pasipo kuwa na kisababishi! Kwa mantiki hiyo ni lazima utafute vichocheo vitakavyopelekea matokeo unayoyataka. Kumbuka kila kitu hutokea kutokana na sababu!

Hii ni sawa na kusema, kuna sababu ambazo zimepelekea kila kitu kinachotokea katika maisha yako haijalishi ni umaskini, hali ngumu, maradhi, magonjwa, mateso, n.k

Rafiki, unatakiwa kujua kwamba kile unachokifanya ndicho hupima kile unachokipata (your input determines your output)

No input no output! And if there is no output it means you will be reluctant!

Na, kama unataka ubadlishe matokeo unatakiwa ubadili kile unachokifanya kwanza. Kwa maana ili upate matokeo ambayo hujawahi kuyapata ni lazima ufanye kitu ambacho hujawahi kukifanya!

Hata hivyo moja ya kitu ambacho kimechangia kuharibu maisha ya wengi ni ile hali ya mtu kukaaa tu, huku akiwa hafanyi chochote kile na akiwa na tarajio kuwa, ipo siku mambo yatajipa naye atabadili maisha yake!

Asijue kwamba anapanda upepo kwa hiyo ataishia kuvuna upepo!

Rafiki, hakuna namna utabadili maisha yako pasipo kuanza kwanza kupanda mapando mapya!

Sikatai, huenda ukawa unapitia umaskini, huenda ukawa unapitia hali ngumu, huenda ukawa umesongwa na magumu mengi mpaka huoni ugeukie wapi!

Unachotakiwa kufanya hapo ni kuanza kupanda mbegu mpya zitakazoondoa hali hizo, kwa maana ukikaa tu pasipo kufanya juhudi za kuondokana nazo, basi hali hizo zitabaki kama zilivyo katika maisha yako.

Na, kama wewe hutashiriki katika kuziondoa hali hizo kwenye maisha yako, hakuna atakayekuja kuziondoa kwa niaba yako!

Kumbuka kanuni ya inertia inasema kwamba "Mambo yaliyotulia yatabaki katika hali ya utulivu mpaka pale yatakaposukumwa na fosi itokayo nje"

Kwa ufupi tuseme, umaskini, hali ngumu, mateso, magumu, manyanyaso na mahangaiko yako yote yatabaki kama yalivyo kama hutothubutu kuyaondoa!

Rafiki, kuanzia saa hii jaribu kuvuta picha kuhusu hali zote unazozipitia, halafu jiulize haya: 
Mimi nilichangia kwa kiasi gani katika kutokea kwake?
Ni nini ulikuwa wajibu wangu? 
Na nifanye nini ili niziondoe hali hizi maishani mwangu?

Usiwe miongoni mwa wa wale watu wanaopata matokeo makubwa kwenye madogo na kupata matokeo Madogo kwenye mambo makubwa!

Kumbuka juhudi yako ndiyo itapima matokeo utakayoyapata! 
Hivyo basi ili ubadili maisha yako unatakiwa uanze kwanza kubadilisha mapando yako ili yakuleletee aina ya matokeo unayoyataka!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogsopt.com


Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...