Namna Ya Kuharibu Tabia Yoyote ILe Kwa Kutumia Kanuni Kuu Tatu Za Kubadili Tabia ...
Habari yako rafiki yangu, ni matumaini yangu u mzima wa afya!
Karibu kwenye mwendelezo wa somo letu linaloangazia kuhusu namna ya kuharibu na kujenga tabia mpya na zenye tija!
Makala iliyopita ilidokeza kanuni kuu tatu zinazoonesha jinsi zambavyo tabia yoyote ile hupitia hadi kujengwa kwake.
Kwa leo utaoneshwa jinsi ya kutumia kanuni hiyo katika kuharibu tabia yoyote ile.
Songa nayo...
1. Vichocheo Vya Tabia Hiyo (Cues)
➡️Ondoa Vichocheo Vyote Kwa Kuvifanya Visionekane Kabisa Katika Mazingira Uliyopo…
Hakuna tabia ambayo haiendeshwi na kichocheo Fulani. Kila tabia unayoifanya tambua kwamba kuna vichocheo vinavyokusukuma ili uifanye na endapo pasingekuwepo na vichocheo hivyo kusingekuwa na sababu ya wewe kufanya tabia hiyo.
Kwa mfano unatumia muda wako vibaya kwa sababu kuna cues zinazochukua sehemu ya muda wako. Cues hizo zaweza kuwa: simu, tv, marafiki pamoja na mazingira ya starehe.
Sasa basi kanuni hii inakutaka utoe vichocheo vyote vinavyokusukuma ufanye baadhi ya tabia, ili visionekane katika mazingira uliyopo!
Kwa mfano kama unataka uharibu tabia ya kutumia muda vibaya huna budi uvitoe Vichocheo vyote vinavyokuchukulia muda wako, kama ni simu au tv unaweza ukazifungia chumba kingine halafu ukampa mtu funguo aondoke nazo ili kwa muda huo uweze kufanya ratiba yako kwa usahihi!
Unatakiwa uondoe Vichocheo vyote vinavyokufanya utumie muda wako vibaya kwa sababu endapo vitakuwepo katika mazingira yanayokuzunguka kila siku, itakuwa ni ngumu sana kwako kuweza kutumia muda wako vizuri.
Ukweli ni kwamba ukishatoa vichocheo vyote vilivyokusukuma ufanye tabia Fulani, hakutakuwa na sababu tena ya wewe kufanya tabia hizo, na hii ni kwa sababu ubongo wako hautachochewa tena ili ukuchochee wewe hapo ufanye tabia hizo!
Kanuni hii ni rahisi sana na imesaidia maelfu ya watu. Unatakiwa kujua kwamba ukishatoa vichocheo vyote ambavyo hukuchochea wewe ufanye tabia Fulani ni ngumu sana kwako kufanya tabia hizo tena.
Angalizo: ukitaka kubadili tabia yoyote ile zingatia kanuni hii kwanza!
2. Mwitikio Wa Tabia Hiyo (Response)
➡️Weka Ukinzani Wa Kuitikia Kufanya Tabia Hiyo...
Unachopaswa kufanya katika kutumia kanuni hii ni kuweka ukinzani katika kuitikia kufanya tabia fulani ambazo hazikupendezi wala kukuvutia!
Kwa mfano badala ya kutumia muda wako kuperuzi, kuangalia tv, kuzurura na marafiki zako, pamoja na kupenda usingizi. Utatakiwa uweke ukinzani kuitikia kufanya tabia hizo na kutumia muda wako kwa kuzingatia vipaumbele vyako ambavyo unataka uvikamilishe, kwa kipindi cha muda Fulani kwa mfano: kwa wiki, mwezi, mwaka na miaka!
Rafiki, unatakiwa kujua kwamba kadri ukinzani unavyokuwa mkubwa ndivyo na ufanywaji wa tabia unavyopungua. Futa baadhi ya namba za simu za marafiki zako, sitisha urafiki na baadhi ya mashoga zako ili ubaki salama!
Unatakiwa ufanye hivyo kwa sababu, karibu kila tabia unayoifanya inatawaliwa na mazingira. Hivyo basi endapo utaweza kutengeneza mazingira yenye ukinzani utafanikiwa katika hilo.
Hata hivyo unaweza ukatumia muda wako kujiuliza ni namna gani unaweza ukatengeneza mazingira yatakayokufanya uweze kutumia muda wako vizuri...
Kwa mfano ili uweze kutumia muda wako vizuri kuwa na utaratibu wa kuandaa daily routine.
Unatakiwa kujua kwamba una wajibu wa kujitengenezea mazingira yatakayokufanya uweze kuwa na mwitikio mzuri wa kufanya tabia nzuri na zenye tija maishani mwako.
Kwa mantiki hiyo badala ya kuitikia kwenda kuwatembelea rafiki zako unaweza ukajitengenezea mazingira yatakayokufanya uwe unajisomea vitabu ili kujiongezea maarifa kwa kuulisha ubongo wako taarifa nzuri.
Endapo utaanza kutengeneza mazingira yanayoendana na upekee wako basi utajikuta ukiweka ukinzani kutumia muda wako vibaya na kuitikia kufanya tabia inayoakisi mazingira uliyoyatengeneza.
3. Matokeo Ya Tabia Hiyo (Reward)
➡️Fanya Matokeo Ya Tabia Hiyo Yasiridhishe (Yafanye Yawe Dhoofu)...
Kwa mfano kama unataka kuharibu tabia ya kutumia muda vibaya pamoja na tabia ya kughairisha mambo, unatakiwa kufanya matokeo yatakayopatikana mara baada ya wewe kutumia muda vibaya pamoja na kughairisha mambo yasikuridhishe kabisa.
Kumbuka kile ambacho hakiridhishwi kimatokeo hakiwezi kurudiwa tena kufanywa. Kwa mantiki hiyo endapo utaifanya tabia ya kutumia muda vibaya pamoja na kughairisha mambo isiwe na matokeo mazuri huwezi kupata motisha na hamasa ya kuendelea kufanya tabia hizo tena.
Pia, unatakiwa kujifunza kwamba gharama za tabia yako ya kutumia muda vibaya pamoja na tabia ya kughairisha mambo zipo miaka ya mbeleni na siyo sasa.
Hii ni sawa na kusema kwamba huko mbeleni kuna gharama zimejificha kwenye tabia yako ya kutumia muda vibaya na tabia ya kughairisha mambo.
Kwa mfano unaweza ukajikumbusha madhara yanayotokana na kughairisha mambo. Na moja ya madhara hayo ni kama vile kupoteza fursa nzuri maishani mwako.
Vilevile kutokana na kutumia muda wako vibaya umeshindwa kupiga hatua kimaisha, hasa ukilinganisha na umri wako. hii ni sawa kusema kuwa kiumri umeenda lakini kimafanikio bado upo nyuma.
Unatakiwa kujua kwamba inahitaji moyo mgumu sana kufanya jambo ambalo unajua fika kabisa litakuletea matokeo mabaya.
Na, ndiyo maana kanuni hii unakutana uweze kutengeneza mwisho mbaya utakaopatikana mara baada ya kufanya tabia fulani, ili uepuke kuifanya tabia hiyo tena na tena!
Je, nifanye nini ili nijenge tabia mpya na zenye tija?
Usijalii fuatana nami kwenye mwendelezo wa somo hili!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi l, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.bogspot.com
Comments
Post a Comment