JINSI YA KUPANGA MALENGO KWA KUTUMIA NENO SMART..._____________________________


Neno smart ni kifupisho cha maneno matano, ambayo yanatoa sifa nzuri za lengo lililoazimiwa!

Lengo lolote lile litakaloazimiwa kwa kutumia mbinu hii ni lazima litafanikiwa!

Ufuatao ni ufafanuzi mfupi wa Mbinu hii:-

S=Specific
M=Measurable
A=Attainable 
R=Realistic 
T=Time

1. Specific (lengo lako liwe Mahususi)

Lengo lazima liwe na sifa ya umahususi! Ni lazima useme kwa uwazi ni kipi unachokitaka!

Kwa mfano huwezi ukasema ninataka nitengeneze kiasi kingi cha fedha!

Kingi ni nini labda? Je unaweza ukafafanua maana ya kingi ukaeleweka kwa watu?

Rafiki hakikisha unaazimia lengo ambalo ni mahususi ili iwe rahisi kufuatilia maendeleo yake pamoja na kujua kuwa umepata kile ulichokuwa unakitaka!

Kwa mfano unaweza ukasema ninataka nitengeneze kiasi cha fedha taslimu 300,000/= kila mwezi!

2. Measurable (Lengo lako liwe linapimika)

Lazima uazimie lengo linalopimika ili iwe rahisi kulitekeleza!

Kwa mfano ukisema nataka niwe tajiri unamaanisha nini?

Je, unataka uwe tajiri wa nini?
Je, unataka uwe tajiri utakayemilili kiasi gani cha fedha?

Rafiki hakikisha lengo linapimika ili iwe rahisi kufuatilia maendeleo yako!

Kwa mfano unaweza kusema, nitakuwa tajiri wa milioni kumi miaka kadhaa ijayo!

3. Attainable (lengo lako linatakiwa lifanikiwe)

Huwezi ukapata mimba leo ukategemea uzae baada ya miezi mitano, haitawezekana!

Kwa mantiki hiyo lengo lako haliwezi likafanikiwa!

Lazima uazimie lengo ambalo lipo ndani ya uwezo wako!

Rafiki epuka kujidinganya, angalia una uwezo gani ili uweke lengo lililopo ndani ya uwezo!

Epuka kuweka Lengo lililopo nje ya uwezo wako kwa maana utaishia kukata tamaa!

4. Realistic (lengo lako liwe halisi)
Huwezi ukasema nataka niwe raisi wa Korea Wakati upo Tanzania na wewe ni Mtanzania!

Inafaa uweke lengo halisi kwa kuhusisha hadhi yako, mahali ulipo na uwezo wako!

Huwezi ukasema unataka uwe msanii maarufu kuwapita wasanii wote, ndani ya mwaka mmoja ilihali hata singo moja hujatoa!

Rafiki Weka Lengo ambalo ni halisi hasa ukihusisha na uwezo wako!

5. Time (ukomo wa muda)
Huwezi ukasema lengo hili nitalikamilisha hivi karibuni!

Hivi karibuni ni nini labda?
Je unaweza ukafafanua Hivi karibuni kwa watu na ukaeleweka? 

Lazima uweke ukomo wa muda ambao unaeleweka ili uwe rahisi kwako katika kufuatilia maendeleo yako, ikiwa ni pamoja na kujua muda uliobaki ili lengo lako liweze kutimia!

Kwa mfano, unaweza kusema, baada ya miaka saba ijayo nitakuwa mwandishi mkubwa, nitakayeandika katika eneo la mahusiano na ndoa ili niweze kuhuisha mahusiano yaliyokufa!

Ndugu, endapo utafanikiwa kuweka malengo yako kwa kutumia mbinu ya SMART utashangaa kila kitu kinaenda vizuri na lazima utaweza kufanikisha lengo lako!

Hivyo ndivyo unavyotakiwa uwe unaazimia malengo yako!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo, Binafsi Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...