Kama Unataka Kuvuta Fedha Maishani Mwako Nitakuonesha Maeneo 10 Ambayo Fedha Imejificha ....


Ukimuuliza mvuvi ni namna gani ya kunasa Samaki kirahisi atakuambia maeneo yote ya Bahari ambayo Samaki hujificha! 

Na katika kufanya shughuli zake za uvuvi basi huhakikisha, anatega nyavu zake maeneo hayo ili aweze kuwanasa samaki wengi kirahisi. Vivyo hivyo ndivyo ilivyo hata kwenye kuvuta fedha!

Unatakiwa kujua kwamba kuna maeneo ambayo fedha imejificha, kwa kusema hivyo linapokuja suala la kutengeneza na kuvuta fedha maeneo hayo ni lazima yazingatiwe!

Unatakiwa kujua kwamba endapo utakuwa unatafuta fedha pasipo uelewa wowote wa maeneo haya kumi ambayo fedha imejificha, hutokuwa tofauti na mtu anayetafuta bikira ndani ya wodi wazazi! 

Yafuatayo ni maeneo kumi ambayo fedha imejificha, kwa mantiki hiyo katika safari yako ya kutafuta fedha hakikisha unaitafuta katika eneo mojawapo ya haya maeneo kumi!

1. Fedha Imejificha Kwa Watu...

Dunia ya sasa ina watu Zaidi ya bilioni saba, na kila mtu unayemuona ana fedha mfukoni mwake. 

Lakini mtu huyo hawezi kutoa fedha mfukoni mwake ili akupe kama hutampa sababu itakayomfanya afanye hivyo. Kumbuka kila kitu hutokea kutokana na sababu!

Unatakiwa kujua kwamba watu watakuwa tayari kutoa fedha mifukoni mwao/kwenye akaunti za zao na kukulipa, endapo kutakuwa na thamani utakayoitengeneza itakayowasababisha wabadildishane nayo. 

Vilevile watu watakuwa tayari kutoa fedha mifukoni mwao/kwenye akaunti zao na kukulipa endapo utaweza kutatua matatizo wanayokumbana nayo kila iitwapo leo!

Rafiki, unatakiwa kujua kwamba watu wote unaokutana nao hapa duniani wana fedha za kutosha tu, lakini hawawezi wakakupa hizo fedha bila sababu itakayowasababisha wafanye hivyo!

Kwa kusema hivyo ili uweze kuzivuta fedha hizo na kuzifanya zije kwako, huna budi kutafuta sababu itakayowafanya watu hao wanaokuzunguka watoe fedha zao mifukoni mwao ili wakulipe!

2. Fedha imejificha kwenye vipaji na uwezo  uliozaliwa nao...

Hakuna mtu ambaye huzaliwa akiwa mtupu ndani yake. 

Sisi sote ndani yetu tumezaliwa vipaji na uwezo mkubwa tu ambao tunaweza kutumia kutengeneza fedha.

Ukweli ni kwamba kila mtu ni bora katika eneo Fulani, na amezaliwa akiwa na kipaji fulani, lakini kwa sababu ya ujinga pamoja na mifumo iliyotutengeneza wengi wetu hujikuta tukishindwa kugundua vipaji vyetu pamoja na maeneo ya uwezo ambayo tumezaliwa nayo.

Ambapo kupitia vipaji hivyo na maeneo hayo tunaweza kutumia kutengeneza fedha!

Kwa mfano kuna wanamuziki, kuna wanamichezo mbalimbali, kuna wachekeshaji, kuna waandishi, kuna washauri, kuna wahamasishaji, kuna waigizaji pomoja na wengine wengi ambao hutumia vipaji vyao na uwezo wao walizozaliwa nao ili kutengeneza fedha!

Je, unaweza ukazungumza? 

Je, unaweza kuigiza? 

Je, unaweza kupika? 

Je, unaweza kufanya watu wacheke? 

Je, unaweza kuandika? 

Je, unaweza kuona? 

Kama unaweza kufanya hayo yote tambua kwamba kuna watu wanatengeneza fedha kupitia kufanya haya! 
S
Hao wote wanatengeneza fedha kwa kutumia uwezo wao waliozaliwa nao pamoja na vipaji vyao.

Kumbuka Kwamba ukiwa na kipaji Fulani basi ndani yako kuna uwezo uliozaliwa nao ili ukusaidie uweze kukiishi kipaji chako!

Hata hivyo, kama kuna watu wameweza kutengeneza fedha kwa kutumia uwezo wao na vipaji vyao maana yake hata wewe unaweza kufanya kama wao, na ukapata matokeo kama yale ambayo wao wameyapata.

Kumbuka hakuna kitu kizuri kama kufanya kitu ambacho ulizaliwa uje ukifanye!

Hakuna furaha kubwa ambayo mwanadamu huipata kama ile furaha ya kukifanya kitu anachopenda kukifanya.

Rafiki, wewe ni fedha inayotembea, lakini shida ni kwamba hujagundua kipaji chako na uwezo wako uko wapi! Kutokana na hilo, ndiyo maana umeshindwa kuvuta fedha maishani mwako.

Kumbuka hakuna mwanadamu ambaye huzaliwa akiwa tupu, kuanzia leo hii anza kujipa tafakari juu ya kile kitu unachoweza kufanya pasipo kutumia nguvu ili upate kuvuta fedha maishani mwako!

3. Fedha imejificha kwenye matatizo...

Kila palipo na watu pana matatizo. Na matatizo hayo yapo kama fursa ya wewe kutengeneza fedha kwa hiyo usilaumu kuhusu matatizo bali yatatue. 

Rafiki, uliumbwa ili uje utatute matatizo ya watu, na ili watu hao wakulipe kutokana na utatuzi huo! 

Hata hivyo unatakiwa kujua kwamba watu hulipwa kutokana na kutatua matatizo na hakuna mtu ambaye hulipwa kutokana na kulaumu au kugundua tatizo. 

Ngoja nikuoneshe kwa mifano ifuatayo: 

Anayeuza chakula anatengeneza fedha kwa kutatua tatizo la mwenye njaa, 

Anayeuza nguo anatengeneza fedha kwa kutatua tatizo la uchi/utupu, 

Anayefundisha anatengeneza fedha kwa kutatua tatizo la ujinga.

Unaweza ukaendelea na orodha, lakini ni Imani yangu ujumbe umefika! 

Ndugu leo hii ninakupa kazi, orodhesaha matatizo yaliyopo kwenye jamii yako au eneo ulilopo, kisha anza kuyatatua, baada ya hapo fedha itakufuata!

Hata hivyo unaweza ukatatua tatizo la mahitaji muhimu ya binadamu kwa kuwatimizia: chakula, mavazi na malazi.

Rafiki kuna matatizo mengi sana unayoweza kuyatatua, yaani kuanzia matatizo ya kimkoa, kitaifa hadi kimataifa.

Chaguo ni lako! Kumbuka ukubwa wa tatizo utakalolitatua ndilo litakalopima kiwango cha fedha utakachotengeneza!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...