FAIDA KUU ZA KUWA NA MALENGO YA KIFEDHA...

Hivi unafahamu kwamba huwezi ukafanikiwa katika jambo fulani kama hujaazimia kulifanikisha jambo hilo?

Hata hivyo kabla hujafanya kitu chochote tafakari mambo haya haya:
1. Faida za kufanya kitu hicho
2. Hasara za kutokufanya kitu hicho.

Zifuatazo ni faida kadhaa za kuwa na malengo ya kifedha!

1. Malengo ya kifedha yanakufanya usiangalie muda uliotumia kufanya kazi bali matokeo uliyoyapata ndani ndani ya muda uliofanywa kazi!

Hii inamaanisha kwamba ukiwa na lengo hutokuwa bize kuangalia muda unaotumia bali utakuwa unaangalia umefikia wapi kwenye lengo lako...

Pia unatakiwa kujua kwamba watu waliofanikiwa sana kifedha siyo watumwa wa muda bali ni watumwa wa malengo.

2. Malengo ya kifedha yatakufanya uwe na nidhamu ya fedha.

Huwezi ukatumia pesa hovyo wakati umelenga kutengeneza milioni 100 mwaka huu.

Kwa mantiki hiyo malengo ya kifedha yatakufanya uwe na nidhamu ya fedha. 

Kutokana na hilo, utajikuta ukiheshimu kila kiasi cha fedha utakachoingiza haijalishi ni kiasi gani...

3. Malengo ya kifedha yatakufanya uweze kujifanyia tathmini binafsi juu ya pale ulipofikia kimafanikio...

Ukiwa na malengo yanayopimika ni rahisi kujifanyia tathmini...

Kwa mfano unaweza ukajifanyia tathmini ya siku, mwezi na mwaka.

Unatakiwa kujua kwamba pasipo malengo huwezi kupoteza muda wako kufanya tathmini...

4. Pia malengo ni hatua ya kwanza ya kufanya mambo yasiyoonekana yaonekane...

Kuna uumbaji wa aina mbili, kuna uumbaji unaoanzia akilini na kuna uumbaji wa pili ambao unakuja kuwa kama kitu halisi!

Kwa mfano unapoazimia kuwa unataka Kupata milioni 100 maana yake umefanya kitu ambacho kilikuwa hakionekani kionekane kwenye Fahamu zako.

Kwa kusema hivyo baada ya mwaka huu kile ulichokiumba akilini kitakuja kutokea kama kitu halisi!

5. Mbali na hilo malengo ya kifedha huongeza hamasa ya mafanikio. 

Hebu jaribu kuvuta picha picha furaha utakayokuwa nayo endapo utafanikisha lengo lako la kutengeneza milioni 100 Mwaka huu!

Hii ni sawa na kusema furaha utakayoipata itakuwa ni hamasa itakayokusukuma ili upambane zaidi kufanikisha lengo lako!

6. Malengo ya kifedha hutusaidia kufanya maamuzi sahihi kuhusu fedha:

Kila mtu ni mtumwa wa maamuzi yake mwenyewe!
Kwa kusema hivyo endapo utatumia Fedha vibaya utakuwa mtumwa wa matokeo hayo!

Lakini ukiwa na malengo ya kifedha utajikuta ukifanya maamuzi sahihi kwa sababu kuna matokeo ya maana umelenga kuyafanikisha!

7. Malengo ya kifedha hukufanya uwe makini na muda wako.

Kwa mfano kuanzia muda wa kuamka, muda wa kufanya kazi pamoja na muda kutafuta wateja.
Pia unatakiwa kujua kwamba muda ni mali, hii inamaanisha muda uliopotezwa ni fedha iliyopotezwa!

Kwa ujumla kuweka malengo ya kifedha ni jambo la msingi sana!
Hivyo ninakualika sana ulifuatilie somo hili kwa makini! 

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...