HATUA KUU ZA KUPANGA NA KUTIMIZA MALENGO YA KIFEDHA...
Hakuna jambo ambalo hutokea pasipo kuanza ngazi fulani hadi kufikia ngazi fulani!
Na ndiyo maana hata ukuaji wa mtoto huanza hatua ndogo zaidi na kwenda hatua ya juu zaidi!
Na, endapo itatokea kuna hatua imerukwa basi kutakuwa kuna shida ya ukuaji wa mtoto husika!
Kwa kusema hivyo ili ufanikiwe katika kuazimia na kufanikisha malengo ya kifedha unahitaji kuyapanga malengo yako hatua kwa hatua!
Unatakiwa kujua kwamba, hakuna jambo ambalo huwa halitokei pasipo kupitishwa kwenye hatua fulani!
Hii inamaanisha kwamba ili upate matokeo mazuri ya mipango yako ya kifedha ni lazima uzingatie hatua zifuatazo:-
1. Andika Kiasi cha Fedha Unachokitaka Kukipata.
Wengi wanajua wanachokitaka lakini ni wachache tu ndio wanaojua kiasi wanachokitaka kutoka kwenye kile wanachokitaka!
Ukweli ni kwamba moja ya sababu kubwa ambayo imetufanya watu wengi tushindwe kufanikiwa kifedha ni kwa sababu hakuna kiasi cha fedha ambacho tumelenga kukipata..
Unatakiwa kujua kwamba, kwenye maisha usipojua unachokitaka, huwezi kujua kama umekipata, Hata kama utakuwa umekipata tayari.
Kwa kusema hivyo, huna budi kuhakikisha kuwa kwenye Fahamu zako unajua kabisa kwa uwazi ni kiasi gani cha fedha unachokitafuta!
Unachopaswa kufanya ni
Kutaja kiasi hicho, mara baada ya kukitaja kiasi hicho unatakiwa ukiruhusu kiasi hicho kizame akilini mwako..
Hatua hii kitaalamu hufahamika kama kuanza na mwisho wako!
Yaani uone mwisho wa kipato chako cha fedha unachokitaka maishani mwako, ndipo sasa uanze kuchukua hatua za kukitafuta mpaka ukipate...
Kwa mfano unaweza ukasema katika maisha yangu nataka nije nifikie uhuru wa kifedha kwa kumiliki milioni mia moja.
Je wewe ni kiasi gani cha fedha umetajeti kukipata?
2. Andika Ukomo wa Muda Ambao Unataka Lengo Lako La Kifedha Litimie...
Huwezi ukafanikisha lengo lako pasipo kuweka ukomo wa muda ambao unataka lengo lako liweze kutimia!
Pasipo kuweka ukomo wa muda huwezi ukajua ni lini hasa lengo lako la kifedha linatakiwa liwe limekamilika, kwa kusema hivyo utaona muda ukizidi kwenda huku lengo lako likibaki pale pale!
Kumbuka muda ni kipindi fulani ambacho hutumika ili jambo fulani liweze kutokea!
Rafiki ni muhimu kuweka ukomo wa muda ambao utatumika kulichakata na kulifanikisha lengo lako..
Unatakiwa kujua kwamba ukomo wa muda hukufanya uweze kuwa na nidhamu binafsi pamoja na kufanya tathmini juu ya hatua uliyofikia kwenye lengo lako la Fedha!
Kwa mfano unaweza ukasema baada ya mwaka mmoja niwe nimeweka milioni mia tano!
3. Gawanya Pato Lako Katika Vipindi Vifupi Vitakavyokurahisishia Utekelezaji Wake...
Njia ya kumla tembo aliye mkubwa ni kupitia kumkata kata katika vipande vidogovidogo!
Kwa kusema hivyo unatakiwa uligawe lengo lako katika vipindi ili ufakishe lengo lako kirahisi, ikiwa ni pamoja na kuepuka kukata tamaa!
Habari njema ni kwamba, endapo utagawa lengo lako la kifedha katika vipindi vifupi utalifanya liweze kuwa dogo hata kama lilikuwa ni kubwa sana...
Kwa mfano kama una mpango wa kuweka milioni tano kwa mwaka mmoja fanya hivi...
Chukua milioni tano gawanya Kwa miezi kumi na mbili.
5000,000÷12= 416666.66
Hii inamaanisha kila mwezi unatakiwa uweke 416666.66 ili ulifikie lengo lako kuu la kuweka milioni tano kwa mwezi!
Na mara baada ya kufanya hivyo anza kuweka akiba yako kila mwezi, baada ya miezi 12 utakuwa tayari una milioni tano mfukoni mwako!
4. Orodhesha Vyanzo Vya Mapato Utakavyotumia Kupata Pato Hilo...
Hatuna lengo ambalo hujitekeleza lenyewe, bali ni lazima ufanye juhudi Binafsi ili kuhakikisha lengo lako la kifedha linafanikiwa!
Unatakiwa kujua kwamba kuandika kiasi cha fedha unachokitaka siyo guarantee ya kukipata!
Hii ni sawa na kusema kuwa, ili ukifikie kiwango cha fedha unachokitaka, ni lazima uoredheshe vyanzo vya mapato vitakavyoplekea kiasi hicho kipatikane!
Hapa unashauriwa kuwa na vyanzo mbalimbali vya mapato ili kimoja kikifeli kingine kiweze kufidia!
Unatakiwa kujua kwamba sababu kubwa hata maji baharini huwa hayakauki ni kwa sababu bahari inapokea maji kutoka vyanzo mbalimbali...
Kwa mfano unaweza ukaorodhesha vyanzo vya mapato kama ifuatavyo:
✔️Kiasi kadhaa kitatokana na mshahara...
✔️Kiasi kadhaa kitatokana na huduma yangu ya ushauri ambayo huwa naitoa...
✔️Kiasi kadhaa kitatokana na faida ya biashara yangu ninayofanya...
✔️Kiasi fulani kitatokana na uwekezaji wangu niliofanya n.k.
N.b endapo utakuwa na lengo kubwa halafu una chanzo kimoja tu cha mapato fanya yafuatayo:
▪️Punguza matumizi yako ili upate fedha zaidi.
▪️Fikiri namna gani ya kuongeza vyanzo vya mapato yako..
Kumbuka Kama utakuwa na one stream of income utakumbana na multiple streams of sufferings...
5. Panga mkakati wa jinsi ya kutimiza malengo yako ya kifedha...
Kanuni ya kichocheo na matokeo inasema kwamba kila kitu hutokea kutokana na sababu!
Hii ni sawa na kusema kuwa na lengo la kifedha pasipo kuweka mkakati wa kulifanikisha lengo hilo ni kazi bure!
Kwa kusema hivyo huna budi kutengeneza ratiba yako ya majukumu na yale utakayoyafanya ili upate kutimiza malengo yako ya kifedha.
Unatakiwa kuzingatia muda utakaoutumia ili ufanikiwe katika malengo yako kwa kuanzia siku, mwezi, mwaka n.k
Kwa mfano kama unataka kuongeza idadi ya wateja wa huduma yako unaweza kuweka mkakati kwa kusema; "nitatafuta wateja wapya kila siku kwa kulipia matangazo Instagram na Facebook ili nipate wateja wengi...
Nitafundisha kila siku mtandaoni kama nitakuwa natoa biashara ya huduma fulani, n.k.
Unatakiwa kujua kwamba kuna wakati mwingine ili uweze kutekeleza malengo yako unatakiwa uwe mtu ambaye hukuwahi kuwa..
Pia, unapaswa kujua kwamba ili kupata matokeo ambayo hukuwahi kuyapata ni lazima ufanye kitu ambacho hukuwahi kufanya..
Panga mkakati wa kutekeleza malengo yako tena nakusihi uanze leo hii!
6. Anza kufanya kwa vitendo mara.
Hapa unatakiwa kuweka mikakati yako kwenye vitendo...
Kwa mfano Kama umeweka mkakati wa kutafuta wateja wapya anza kutafuta, Kama ni kufanya kazi anza kufanya kazi, Kama ni kuweka akiba anza kuweka akiba na kama nj kulipa madeni anza kulipa madeni.
Hutakiwi kupoteza muda! Kumbuka iii jambo fulani litokee ni lazima kipindi fulani cha muda kipite.
7. Fanya tathmini ili kupima mwenendo wako kama unapiga hatua au laah...
Ni muhimu kufanya tathmini ili ujue umefika wapi na ufanye nini ili ufike kule ulikopanga kufika!
Kumbuka kuwa maisha ambayo hayafanyiwi tathimini hayana maana!
Pia, unatakiwa kufanya tathmini ya kifedha kwa kuzingatia kila kipindi uiichiweka kama tulivyoona kwenye hatua ya nne.
Kwa mfano
fanya tathmini ya lengo la siku ili kujua kama kipato ulichopanga kupata kwa siku kimetimia!
Fanya tathmini ya wiki ili kujua kama Lengo lako la wiki limetimia...
Fanya tathmini ya kila mwezi ili kupima kile Kiasi ulichopanga kuingiza kwa mwezi kimetimia...
Fanya tathmini ya mwaka ili kubaini umefika wapi!
Angalizo: endapo utaona lengo lako halijatimia jiongeze kwa namna yoyote ile. Kwa mfano unaweza kukopa, au kopesha, azima nguvu ya ziada kwa watu, au unaweza kuongeza au kupunguza baadhi ya vitu!
8.Fanya kwa mwendelezo mpaka lengo lako Litimie...
Hakuna kitu ambacho huua ndoto ya watu kama kukosa kwa Sanaa ya mwendelezo...
Kwa mfano Kama umeazimia kuweka 100,000/= basi fanya kwa mwendelezo kwa kuweka kila mwezi kwa miaka yote uliyopanga Lengo Lako Litimie..
Unatakiwa kufanya kila jambo kwa mwendelezo yaani kuanzia tathmini na kila unachopaswa kufanya kifanye kwa mwendelezo..
Ndugu pambana sana ili kutimiza malengo yako ya kifedha.
Unatakiwa ujijengee tabia ya kuwa mchapakazi, tabia ya kuweka akiba, tabia ya kuamka mapema, tabia ya kufungua ofisi mapema, tabia ya kutokughairisha mambo, tabia ya kujifunza pamoja na tabia ya kujiwazia mema muda wote..
Mpaka kufikia hapo utakuwa ni unstoppable!
No one will stop you from going!
Hebu kuwa na mwendelezo katika kutekeleza malengo yako ya kifedha!
Usifanye kwa kudonoadonoa!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment