JINSI YA KUFANIKISHA LENGO LA KIFEDHA KWA AJILI YA JAMBO FULANI ILI KUEPUKA MADENI...

Siyo kila njia unayotumia kufanya jambo fulani ni njia sahihi! Na endapo hutatumia njia sahihi huwezi huwezi ukapata matokeo sahihi vilevile!

Kwa kusema hivyo unatakiwa utumie kanuni hizi mbili ili kuepuka kuingia kwenye madeni pamoja na kufanikiwa kifedha!

1. Angalia kiasi cha fedha kinachohitajika. Ni lazima ujue ni kiasi gani cha fedha kinachohitajika kwa ajili ya kufanikisha lengo lako!

Mara baada ya kujua ni kiasi gani kinachohitajika, angalia pato lako huku ukihusisha na muda uliobaki ili kiasi hicho kikamilike!

Baada ya hapo amua kutenga kiasi fulani cha pesa kila baada ya muda Fulani au kila siku.

Mpaka muda uliopanga kufanikisha lengo lako kufika utakuwa tayari una kiasi hicho mkononi mwako! 

Kwa mfano tuchukulie umepanga kufikia mwezi wa 12 mwaka huu 2024 uwe umefanikiwa kuweka angalau 100, 0000,000/= kwa ajili ya mtaji wa kufungua biashara yako!

Unachotakiwa kujiuliza ni hiki; je, umebaki muda gani ufike mwezi wa 12?

Ukishapataa jibu sasa amua kutenga kiasi fulani cha pesa aidha kila baada ya mwezi au kila baada ya wiki ili ufanikishe jambo lako la kuwekeza!

2. Nji ya pili ni kuamua kutenga fedha zako kutegemeana na: kipato chako pamoja na muda unaohitajika ili ukamilishe lengo lako la kifedha!

Kwa mfano Kwa kuangalia kipato chako, unachopaswa kufanya ni kutenga angalau asilimia 10% au 20% ya kipato chako, kama kiasi kitakachokuwezesha kufanikisha lengo lako!

Hata hivyo kwa kutegemeana na muda unaoshusika, tufanye unalipa kodi ya nyumba kiasi cha 50,000/=
Na unapaswa kulipa 150,000/= kwa miezi mitatu...

Sasa basi unaweza kuamua kuweka 5,000/= kila siku, ambapo utajikuta ukikamilisha kodi yako ndani ya mwezi mmoja tu!

Au unaweza ukaamua ukaanza kuweka kila siku 2000/= ndani ya kipindi cha miezi mitatu utakuwa umeweka 180,000/= hivyo utaweza kulipa Kodi bila shida!

Hitimisho kila jambo linalohitaji pesa linakuhusu wewe!

Hivyo basi kama kutakuwa kuna jambo linahitaji kiasi fulani cha pesa huko mbeleni tambua kwamba huo ni wajibu wako, kwa kusema hivyo huna buda kuchagua hizo njia mbili zikusaidie katika kufanikisha jambo hilo!

Pia unatakiwa kujua kwamba endapo utashindwa kutumia mbinu hizi mbili kuna uwezekano wa kuingia kwenye madeni hivyo basi huna budi kuyaepuka kwa kutumia mbinu hizi!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...