JINSI YA KUTENGENEZA UTAJIRI... HATUA YA 2,3,&4
2. Gundua soko lako...
Ukishagundua uwezo wako lazima ujue soko linalohitaji kile ulichinacho. Unatakiwa kujua kwamba kipaji chako ni kwa ajili ya watu wengine. Ukweli ni kwamba tunaishi kwa ajili ya watu wengine.
Mbali na hilo unatakiwa kujua kwamba siyo kila mtu atahitaji kipaji chako au uwezo wako! Kuna wengine hawatahitaji kabisa chochote kile kutoka kwako, hata usiumie kwa maana hata wao nao wanahitaji kitu kutoka kwa watu wengine.
Kutokana na hilo unahitaji kugundua soko lako liko wapi ili uweze kuuza huduma yako au bidhaa zako.
Kugundua soko lako lilipo kunahusisha vitu kama vile: kuwadokeza wateja wako ni wepi? Jinsia yao ni ipi, umri wao ni upi, hadhi ya maisha yao ni ipi, ikiwa ni pamoja nae neo wanalopatikana.
Ndugu siyo kila mtu anahitaji kipaji chako au uwezo wako, kwa hiyo kugundua uwezo wako siyo kigezo cha kufanikiwa kutengeneza utajiri huo bali lazima uandae orodha ya watu watakaonufaika na uwezo wako.
Kumbuka mtandao wa watu ulionao ndiyo unapima utajiri wako. Kwa kusema hivyo ukubwa wa soko utakaokuwa nao ndiyo utapima kiwango cha fedha utakachotengeneza!
3. Andaa huduma/bidhaa zako
Katika somo la maeneo kumi ambayo fedha imejificha tuliona kuwa fedha imejificha kwenye bidhaa au huduma.
Kwa kusema hivyo ni wale tu watakaokuwa wanatoa huduma Fulani au watakaokuwa wanauza bidhaa Fulani ndiyo hao watakaokuwa wanatengeneza fedha!
Kumbuka fedha hufuata thamani, hii ni sawa na kusema ile thamani utakayoitengeneza kupitia huduma yako au bidhaa yako ndiyo itasababisha fedha iweze kukufuata.
Unatakiwa kujua kwamba ukishagundua kipaji chako au uwezo uliozaliwa nao yafaa utengeneze huduma au bidhaa Fulani kupitia uwezo huo.
Kwa mfano kama umegundua kwamba una uwezo wa kushauri watu unaweza ukaanzisha huduma ya ushauri nasaha.
Umegudua kwamba una uezo wa kuandika unaweza ukaandika vitabu ukawa unauza kupitia hivyo ukatengeneza fedha.
Umegundua kwamba una uwezo wa kupika michanganyo yenye Ladha nzuri unaweza ukabuni mchanganyo Fulani ukaandaa pakeji yake ukawa unauza, kupitia hilo ukatengeneza fedha.
Rafiki angalia fursa zinazoendana na uwezo wako, andaa huduma au bidhaa nenda kauze. Kumbuka huwezi ukapata kitu pasipo kufanya chochote kile.
Hivyo basi ni lazima uandae huduma au bidhaa Fulani za kuuza ili utengeneze utajiri, pasipo kufanya hivyo huwezi ukatengeneza utajiri!
4. Tengeneza upekee wako
Usifanye kitu kwa namna ambayo imezoeleka na kufanywa na kila mtu, kwa sababu endapo utafanya hivyo utaishia kupata matokeo ya kawaida ambayo kila mtu hupata, kutokana na hilo huwezi ukatengeneza utajiri!
Unatakiwa kujua kwamba ukishagundua uwezo wako na soko lako, sasa yafaa utengeneze upekee wako kwenye huduma yako.
Kisaikokolojia inaaminika kuwa, kila mtu ni wa kipekee na ana upekee Fulani. Kwa kusema hivyo lazima ugundue upekee wako ni nini ili uweze kutoa huduma kwa kiwango bora.
Ndugu upekee wako ndiyo utakaokutofautisha na washindani wako pamoja na watu wanaotoa huduma kama yako!
5. Jitangaze
Unatakiwa uwafanye watu watambue kwamba wewe upo na unatoa huduma au unauza bidhaa Fulani.
Ukweli ni kwamba kuna watu ambao hawajui chochote kile kuhusu wewe, kuhusu bidhaa zako na kuhusu huduma yako.
Kwa kusema hivyo unatakiwa ujitangaze ili uwafanye watu watambue kuhusu bidhaa yako, huduma yako na umuhimu wa bidhaa au huduma yako maishani mwao.
Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya watu huwa hawatambui kwamba kuna tatizo, na kwa vile hawajui kuwa kuna tatizo unatakiwa uwafanye watambue kwamba kuna tatizo baada ya hapo sasa unatakiwa upendekeze bidhaa yako ama huduma yako kama mbinu ya kutatua tatizo hilo.
Rafiki unatakiwa kujua kwamba:
Bidhaa nzuri + haifahamiki = mauzo mabaya
Bidhaa mbaya + kufahamika = mauzo ya wastani
Bidhaa nzuri + kufahamika = mauzo ya ajabu.
Una kila sababu ya kuwafanya watu watambue kwamba wewe upo na unatatua tatizo Fulani kwa watu hao ili wafurahie maisha yao.
Comments
Post a Comment