JINSI YA KUTUMIA KANUNI YA VISACO KUFANIKISHA MALENGO YAKO YA KIFEDHA!


Kila kitu hapa duniani huendeshwa na kanuni! Na ili mafanikio yapatikane kuhusu kitu hicho utatakiwa kufanya kama vile kanuni inavyokutaka!
Uzuri ni kwamba kanuni hufanya kazi kwa mtu yeyote yule na akiwa mahali popote pale!

Habari njema nyingine ni kwamba kanuni hazina upendeleo bali humpa kila mtu matokeo sawa sawa na alivyotumia kanuni hiyo!

Hio ni sawa na kusema endapo utafanya kile kanuni inakutaka ufanye, utapata matokeo Mazuri, na endapo utafanya kinyume na kanuni yako utapata matokeo mabaya!

Hivyo basi ili ufanikiwe katika kuweka malengo ya kifedha, unatakiwa utumie kanuni ifuatayo:-

Kanuni ya VISACO ni kifupisho cha maneno matatu ambayo ni: vision, sacrifice na consistence.

VI= VISION
SA= SACRIFICE
CO= CONSISTENCE.

wengi wetu huwa tunashindwa kufanikiwa katika mambo yetu kutokana na kushindwa kutumia kanuni hii!
Unatakiwa kujua kwamba kuna uwezekano wa kufanikiwa katika jambo lolote lile endapo utatumia kanuni hii!

Mambo MATATU kuhusu kanuni hii ya visaco...

1. Vision
Maono ni picha kamili ya maisha ya mtu yajayo! Unatakiwa kujua kwamba mtu ambaye hana maono hajaanza bado kuishi ila ataanza kuishi pindi akipata maono.

Mbali na hilo huwa tunapanga malengo fulani kulingana na maono tuliyonayo!
Je unaona nini kuhusu kesho ya maisha yako?
Je unaona nini kuhusu kipato chako cha fedha siku zako zijazo?

Unaalikwa utengeneze malengo makubwa kwani ndiyo yatachochea hamasa na nguvu za kupambana zaidi!

2. Kuwa tayari kulipa gharama (sacrifice)
Kwa chochote kile kizuri utakachokuwa unakitaka katika maisha yako tambua kuna gharama utapaswa kulipa!

Unatakiwa kujua kwamba kuna gharama za aina mbalimbali, kama vile: gharama ya muda, nguvu, pesa, maarifa, hisia n.k.

Jambo moja unalopaswa kujua ni kwamba ukiona kuna matokeo mazuri juu ya jambo fulani jua kuna mtu alikubali kuingia gharama ili kupata matokeo hayo!

Pia, usiogope maumivu unayoyapata bali ogopa kukwepa maumivu yaliyobeba mafanikio yako!

Kumbuka ni kheri kuumia leo ili ufurahie kesho kuliko kufurahia leo na kuja kuumia kesho.
Hebu jisacrifice kulipa gharama my mentees!

3. Fanya kwa mwendelezo (consistence)

Hapa unapaswa kujenga nidhamu ya hali ya juu ili ufanye masuala yote unayopaswa kuyafanya kwa mwendelezo.
Kuna watu ambao huanza kufanya jambo fulani kwa moyo wao wote lakini hujikuta wakiishia njiani!

Watu hawa hukosa sanaa ya mwendelezo katika mambo yao ambapo mwisho wa siku hujikuta wakiishia njiani.

Unatakiwa kujua kwamba dakika moja ya uzembe wa kutokufanya jambo fulani inaweza kuharibu kabisa matokeo makubwa ambayo umeyahangaikia kwa muda mrefu!

Linda sana kila ulichonacho, huku ukifanya juhudi zaidi kutafuta kile usichonacho!

Hivyo ndiyo unavyoaswa utumie Kanuni ya visaco kubadili maisha yako!

Yaani pata maono makubwa
Halafu jitoe sadaka kukamilisha maono hayo,
Mwishowe kuwa tayari kufanya kila siku ili upate matokeo unayoyataka (yaani fanya jambo fulani kila siku)

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...