Kama Unahitaji Fedha Nitakuonesha Mahali Fedha ilipo....
Habari yako mpenzi msomaji, karibu kwenye mwendelezo wa somo letu linaloangazia kuhusu maeneo kumi ambayo fedha Imejificha...
Mpaka sasa tumeangalia maeneo sita!
Kwa leo utaenda kuoneshwa maeneo mengine ambayo fedha Imejificha kama ifuatavyo:-
Maono ni kuwa na picha kamili juu ya jambo Fulani lijalo.
Kwa kusema hivyo linapokuja suala la fedha kila palipo na maono makubwa kuhusu fedha pana mafanikio ya kifedha, na pale ambapo hapana maono kuhusu fedha hapatakuwa na mafanikio ya kifedha.
Unatakiwa kujua kwamba maono huweza kuvuta matukio mazuri katika maisha, na hii ni kwa sababu yale mambo ambayo mtu anakuwa kaona akilini mwake ndiyo anayoyavuta na kuyafanya yawe sehemu ya maisha yake.
Kumbuka unapata kwenye maisha kile unachokitengeneza na kukiona akilini mwako.
Na ndiyo maana kanuni ya msawazo wa akili inasema; “kile unachokipata kwenye maisha ni uakisi wa kile unachokiona kwenye akili zako”
Bila shaka hapo ulipo una wazo Fulani la kutokea muda mrefu sana lakini unasitasita kulifanyia kazi, rafiki hutakiwi kusitasita tena. Hebu anza kuchukua hatua halafu utashangaa fedha itakavyoanza kukufuata.
Kabla sijamaliza kufafanua hoja hii ninakuomba ujiulize hili: je unaona nini mbele yako hasa linapokuja eneo la kifedha?
Ndugu, unatakiwa kujua kwamba kile unachokiona ndicho unachokipata.
Kwa kusema hivyo huna budi kuhakikisha kwamba unaona kiwango kingi cha fedha kwenye akili yako.
Baada ya hapo akili yako itakuletea mbinu utakazozitumia ili kuyafikia maono yako ikiwa ni pamoja na kukuchoea na kukuhamasisha Zaidi ili uweze kuyafikia maono yako!
Siku moja nilimuona mtu akivua Samaki, mara baada ya kuvua alikuwa akilinganisha Samaki hao na kiganja cha mkono wake. Na ilipotokea Samaki kazidi ukubwa kiganja chake alikuwa akimrudishia majini.
Binafsi nilishangazwa sana na kitendo alichokuwa anakifanya. Ikabidi nimuulize wewe kijana mdogo, hii maana yake nini? Akanijibu nina chungu kidogo sana cha kukaangia Samaki, chungu chenyewe ukubwa wake unaaendana na kiganja changu.
Kwa hiyo Samaki ambaye ni mkubwa kuliko kiganja changu, namrudisha mtoni kwa vile sitoweza kumkaanga kwenye chungu changu kidogo.
Huyu kijana alikosa maono, na ndiyo maanaa Samaki walivyonaswa alikuwa akiwarudisha majini! Ningekuwa mimi nikimvua ningemkata vipande viwili/vitatu halafu naenda zangu kumkaanga kwenye chungu changu kidogo!
Huenda hata wewe umekuwa ukinasa samaki wengi sana ukaishia kuwarudisha majini kama alivyofanya huyo kijana mdogo, kwa vile umekosa maono!
Fedha imejificha kwenye maono, pata picha kamili juu ya kile unachokitaka, halafu uanze kupambana hadi ukipate! Kumbuka hakuna kizuizi juu ya kile unachoweza kuishia kukiona na kukikamilisha!
8. Fedha imejificha kwenye Mawazo...
Mawazo ndiyo huendesha na kuitawala dunia. Na ndiyo maana hata Mungu alipoumba ulimwengu pamoja na vyote vilivyomo hakuumba: magari, nyumba, fedha, Barabara, simu, kompyuta, intanenti, n.k. Haya yote yamekuwepo kutokana na ugunduzi unaofanywa na mwanadamu.
Kwa kusema hivyo jambo ambalo lilishindikana jana leo linawezekana na lile ambalo leo haliwezekani kesho litawezekana.
Hata hivyo Muumba alitupa akili ambayo imetusaidia kufanya uvumbuzi wa kina juu ya vile alivyoviumba ili tuvitumie na kutengeneze fedha kupitia hivyo!
Kwa mfano haujaumba ardhi lakini unaweza ukaikatua ardhi ukazalisha mazao ukauza, baada ya hapo ukatengeneza fedha. Haujaumba mti lakini unaweza ukatumia mti kujengea pamoja na kutengeneza fenicha mbalimbali, ukauza ukatengeneza fedha.
Haujamuumba mwanadamu lakini unaweza ukamtumia kutengeneza fedha kwa kumpa kile anachokihitaji.
Rafiki unatakiwa kujua kwamba kutokana na kubadilika kimawazo kunakofanywa na mwanadamu, dunia ya sasa ni tofauti sana na dunia iliyokuwepo kipindi cha nyuma.
Kwa sababu kipindi cha nyuma hakukuwa na nyumba, magari, umeme, intanenti, kompyuta, simu na mwanadamu aliishi maisha kwa namna ya tofauti na vile ambavyo tunaishi sasa!
Kutokana na Mawazo kubadilika, watu wameweza kugundua: simu, magari, kompyuta, umeme, ni kwa mfano tu. Kwa kusema hivyo ugunduzi huo ni matokeo yanayotokana na Mawazo.
Na yule ambaye alipata wazo akatengeneza kifaa kilichorahisisha maisha ya binadamu ameweza kutengeneza kiwango cha kustaajabisha cha fedha!
Hata hivyo kuna Mawazo lukuki ambayo hujitokeza akilini mwa mwanadamu, lakini ni Mawazo yanayofanyiwa kazi tu ndiyo huleta matokeo. Kwa kusema hivyo lazima uwe mtu wa kuangalia mwenendo wa kile kinachoendelea kwenye fahamu zako.
Mbali na hilo kuna makundi ya manne ya watu linapokuja suala la kuengeneza fedha kwa kupitia mawazo: kuna wale ambao wana Mawazo lakini hawana fedha za kulifanya wazo lao lifanikiwe, kuna wale ambao wana wazo na wana fedha, kuna wale ambao wana fedha na hawana wazo la kutengeneza fedha nyingine Zaidi ya zile walizonazo na kuna wale ambao hawana wazo na hawana fedha.
Bila shaka miongoni mwa hayo makundi manne kuna kundi upo! Rafiki unahitaji kufikiria juu ya hili kwa maana fedha imejificha kwenye wazo na kama kuna watu wameweza kutengeneza fedha kupitia Mawazo yao, inamaanisha kwamba hata wewe unaweza ukatengeneza fedha kupitia wazo lako endapo utafanya kwa namna ileile kama wao walivyofanya!
Rafiki sasa hivi kazi timamu zimeweza kubadilisha kazi za kutumia nguvu, na hakuna mtu ambaye ameandikiwa busara bali kila mtu atazipata endapo atazitafuta.
Friend fedha imejificha kwenye wazo, huwezi ukaniambia huna wazo! Wazo unalo sema nini hujui ufanye nini ili utumie wazo lako kutengeneza fedha.
Unatakiwa kujua kwamba kila jambo linawezekana ukijifunza jinsi ya kufanya jambo hilo!
Je, lipi ni wazo lako? Kumbuka wazo lako lafaa liwasaidie watu wengine ikiwa ni pamoja na kurahisisha maisha ya mwanadamu, kwa maana hauwezi kuja na wazo ambalo haliwasaidii watu na ulipwe kupitia hilo!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44285329/0683184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge blogspot.com
Comments
Post a Comment