Kama Unatafuta Fedha Nitakuonesha Maeneo Kumi Ambayo Fedha Imejificha..
Habari yako rafiki yangu! Ni matumaini yangu u mzima wa afya!
Karibu kwenye mwendelezo wa somo letu linaloangazia kuhusu maeneo kumi ambayo fedha Imejificha!
Kwa leo utaoneshwa maeneo mawili ya mwisho ambayo fedha Imejificha kama ifuatavyo:-
Nimesoma maandiko, lakini sijaona andiko linaloonesha kuwa Muumba aliumba fedha!
Kwa kusema hivyo, haijalishi kama Mungu aliziumba fedha au laah lakini ni yeye ndiye kampa mwanadamu akili, maarifa na nguvu ya kufanya uvumbuzi ili aweze kufanya mabadilishano!
Hata hivyo mbali na Muumba kutokuumba fedha haimaanishi kwamba alikuwa kafirisika lahasha! Unatakiwa kujua kwamba Mungu hakutengeneza fedha, lakini akiamua fedha zije kwako zitakufuata!
Kitu unachotakiwa kuchukua hapa ni kwamba, Mungu akikubariki hakuna atakayezizuia baraka zako!
Je, unajua utajiri alioupata Ibrahimu mara baada ya kuitii sauti ya Mungu?
Je, unajua utajiri alioupata Mfalme Sulemani mara baada ya kufanya maombi yaliyompendeza Mungu?
Je, unajua baraka ambazo Mungu aliziahidi kwa taifa la Israeli katika kumbukumbu la torati 28:1-14 endapo wangeitii sauti yake na kufanya maagizo yake awaagizayo kwa bidii?
Rafiki unatakiwa kujua kila kwenye agano ni lazima kuna maudhui ya kutunzwa! Kwa kusema hivyo ni lazima uweze kumjua Mungu ni nani kwanza, na kama hujui neno la Mungu basi humjui Mungu kwa sababu Mungu ni neno!
Na, kama humjui Mungu ni ngumu sana kufanikiwa kifedha kupitia yeye.
Wengi huwa wanaomba kwa kufunga, kulia na kwa kuombeleza, wengi wanatoa hadi sadaka, wengi wanatoa hadi fungu la kumi lakini mambo hayabadiliki.
Wasijue shida nini, kumbe hawajui mfumo wa Mungu anavyofanya kazi, huku wengine wakitoa mahali pasipo sahihi na pengine labda kwa mtumishi ambaye hamtangazi Mungu halisi!
Hivi unajua kwamba sadaka ya mtu mwovu ni chukizo mbele za Mungu? Mithali 15:8 inasema hivyo!
Hivi unajua kwamba Mungu yuko mbali na wasio haki bali huwasikia wenye haki tu? Nenda kasome Mithali 15:29 na 1 Petro 3:12
Wengi wanadhani wanampenda Mungu na wamejitoa kwa ajili yake kumbe siyo. Unatakiwa kujua kwamba kumpenda Mungu ni kushika amri zake. Yohana 14:22, 23.
Kwa kusema hivyo wale wanaoshika amri za Mungu ndio hao ambao Mungu anawabariki kwa sababu wanatunza agano lililopo kati ya Mungu na wanadamu.
Hata hivyo Mungu huweka agano na watu wake ili awabariki, endapo watatunza agano na endapo hawatatunza Mungu huwalaani watu hao!
Hii ni sawa na kusema kwamba, kuna baadhi ya watu wanafanya maisha ya Imani lakini wamelaaniwa kwa sababu hawajatii sauti ya Mungu. Kutokana na hilo kila wanachokifanya kinagoma kwa sababu hawatimizi mapenzi ya Mungu.
Rafiki, Mungu yupo na anabariki lakini sharti ili ubarikiwe ni lazima ujikabidhi kwenye amri zake kwanza!
Nakukumbusha tena wewe zishikie amri zake na uziishi halafu yeye atakubariki, kwa maana anatambua wajibu wake kwako mara baada ya kutunza agano, yaani kukubariki!
Sunajua kilichomkuta Adamu mara baada ya kuasi? Alipoteza kila kitu akaanza kuishi maisha magumu pamoja na kukutana na mateso mengi kwa sababu ya kuasi sheria ya Mungu!
Rafiki Mungu anakupenda na anakutaka ufanikiwe, kwa kusema hivyo unatakiwa uache mwenendo mbovu halafu ushike neno lake pamoja na amri zake! Baada ya hapo yeye atakubariki na lolote ambalo mkono wako utafanya litafanikiwa! Zaburi 1:3
Najua kuna watu hawaamini katika nguvu za Mungu. Hivi unajua maji yaliingiaje kwenye nazi?
Hivi unajua, ni kwa namna gani shahawa iliyo kimininika humtoa mtoto aliye siye kimiminika? Je, unajua ni nini huzuia anga lisidondoke?
Je, unaijua nguvu inayosimamisha maji ya Bahari inatoka wapi?
Ukweli ni kwamba sisi kama wanadamu kuna maeneo hatuwezi kitu, kwa kusema hivyo ni lazima tujiunganishe kwake halafu yeye atatutendea mambo makuu! Kasome Isaya 55:8 na Yeremia 33:3.
Kumbuka utajiunganisha kwa Muumba mazima pale ambapo utashika amri zake. Uzuri ni kwamba amri zake siyo mzigo bali ni nyepesi mno, ni suala la kuamua tu.
Rafiki, unasubiri nini? Ishi maisha ya kitauwa halafu Mungu atakujazi baraka!
10. Fedha imejificha kwenye kazi
Neno kazi limeonekana kama kitu cha ajabu kwa watu wengi, na ndiyo maana kuna wengine huwa hawapo radhi kufanya kazi wenyewe pasipo kusukumwa au kuamrishwa!
Unajua kile biblia imesema? “asiyefayanya kazi na asile” 2 Wathesalonike 3:10. Kwa kusema hivyo kama hakuna kazi hakuna malipo!
Rafiki, ili ufanikiwe kifedha ni lazima kuwe kuna kazi unayoifanya. Unatakiwa kujua kwamba kazi itakuwa kama nyenzo itakayokusaidia uweze kutengeneza fedha!
Hata hivyo wapo watu wengi ambao wanadhani wapo kazini na wanafanya kazi kumbe wapo vibaruani.
Na hii ni kwa sababu maana halisi ya kazi ni kutengeneza pato kwa kufanya kile ambacho uliumbiwa uje ukifanye, na kama unafanya kazi kwa sababu ya kutengeneza fedha tu, hiyo siyo kazi na hauna tofauti na kibarua!
Rafiki unatakiwa kujua kwamba kazi haitakiwi kuwa ni mateso kwako. Bali kiwe ni kile kitu ambacho unafurahia kukifanya, na endapo unafanya kazi ambayo kwako unaiona kama ni mateso, maana yake hauwezi ukatengeneza fedha za kutosha kwa sababu kile ambacho unakifanya hukipendi.
Ndugu, unatakiwa kujua kwamba kufanikiwa kifedha unahitaji ufanye kazi haijalishi ni kazi unayoipenda au laah!
Hata hivyo unaweza ukaanza na kazi ambayo huipendi, baada ya hapo tengeneza kiasi kadhaa cha fedha, halafu tumia kiasi hicho kama kianzio cha kuanza kufanya kazi unayoipenda!
Ukweli ni kwamba kuna baadhi ya watu wanafanya baadhi ya kazi siyo kwa sababu wanatakiwa wafanye ila ni kwa sababu wametengenezwa kupitia mifumo Fulani ili waweze kufanya kazi hizo.
Watu hawa huwa hawafanikiwi kutengeneza fedha za kutosha kwa sababu cha kwanza wanafanya kitu ambacho hawakuumbwa waje wakifanye na pili hawafanyi kwa moyo wao wote.
Kumbuka hauwezi ukapambana kula labda uumwe, hauwezi kupambana kuongea labda uumwe, hauwezi kupambana kukimbia labda uumwe.
Ukimchukua ndege ukamweka kwenye maji lazima atapambana Zaidi ili apate kuishi mle. Hata hivyo ukimchukua Samaki ukamtoa nje ya maji lazima atapambana ili apate kuishi.
Ukweli ni kwamba watu wengi wanadai wapo kazini kumbe wanapambana ili waishi lakini hawafanyia kazi zao ili wafurahie maisha.
Unatakiwa kujua kwamba ndege huwa hatumii nguvu kupaa, Samaki huwa hatumii nguvu kuogelea, nyani huwa hatumii nguvu kukwea kwenye miti.
Kwa kusema hivyo hata wewe unatakiwa kufanya kazi ambayo hutumii nguvu kwa sababu, tafsiri nzuri ya kazi ni ile inayosema “kufanya kile kitu ambacho unapenda kukifanya na pengine labda uliumbwa kwa ajili ya kufanya kitu hicho”
Unatakiwa kujua kwamba matajiri wanafanya kazi kidogo sana ukilinganisha na watu wa kawaida lakini wanatengeneza fedha za kutosha kwa sababu wanafanya kile walichoumbwa waje wakifanye.
Rafiki fedha imejificha kwenye kazi! Je una kazi gani? Je, unafanya kile ambacho uliumbwa uje ukifanye?
Kama jibu ni Hapana basi ni ngumu sana kuweza kufanikiwa kifedha kwa sababu ni kupitia kazi ndipo mtu anaweza akatengeneza pato la kutosha!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44285329/0683184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge blogspot.com
Comments
Post a Comment