Pokea Salamu Za Mwaka Mpya 2024 kutoka kwa Emmanuel Samuel…
Awali yeyote natanguliza shukrani kwa Mungu kwa kutulinda, kutusimamia na kutuongoza sote pamoja na kutuvusha kutoka 2023 hadi 2024.
Rafiki, tumia sehemu ya muda wako kumshukuru Mungu haijalishi mwaka uliopita umepitia mangapi, unatakiwa kujua kuwa, ni neema kubwa sana kuweza kuuona na kuufikia mwaka mpya ukiwa hai.
Hebu rudisha sifa na utakufu kwa Mungu wako kwa maana haikuwa rahisi. Natambua kuwa umepitia mengi lakini nipo hapa kukusihi kuwa umshukuru Mungu haijalishi umepitia magumu mangapi!
2 Wathesalonike 5:18 “shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu”.
Pili, natanguliza shukrani zangu za dhati kwako wewe ambaye umekuwa ukiguswa na masomo yangu, ikiwa ni pamoja na kuniunganisha na baadhi ya watu, kunipa fursa za kuwafundisha watu kwenye groups, kufanya mahojiano na mimi kuhusu vipengele kadhaa, kuwa tayari kulipia ili upate huduma zangu, kuthamini huduma yangu ya ushauri pamoja na kukubali kufanyiwa usimamizi na mimi chini ya King Mentaship Program (K.P.M)
King Mentaship inatambua mchango wako, inatambua thamani yako, inatambua uwepo wako na inatambua fika kabisa kwamba pasipo wewe haiwezi ikawepo; kwa maana uwepo wako ndiyo umeifanya King Mentaship iwepo.
Pokea salamu kutoka kwa mtoa huduma ya usimamizi na ushauri, chini ya (King Mentaship Program).
Kuhusu Mwaka 2023…
Mwaka 2023 umekuwa ni mwaka wa baraka na neema sana kwangu, ninamshukuru Mungu kwa kuwa amefungua macho yangu, baada ya macho yangu kufunguliwa nayo yakaona uhitaji mkubwa wa elimu uliopo kwenye jamii yangu.
Mara baada ya macho kufunguka Mungu akafungua fahamu zangu.
Fahamu zangu zilipofunguka nikasikia sauti ikiniambia…
Emmanuel una uwezo wa kuandika na kuelimisha watu hao... nikajiuliza naanzaje?
Ikaniambia; wewe anza kuandika… na endelea kuandika… you just write!
Kweli nikaanza kuandika Makala mbalimbali za kuelimisha jamii katika vipengele mbalimbali, nikawa natuma kwenye WhatsApp groups, WhatsApp status, facebook na kwenye blog yangu, mpaka kufikia sasa nimeweza kujenga familia kubwa tu!
Na nimeweza kutoa huduma ya ushauri na usimamizi, na najivunia kuwa msimamizi kwa watu ambao hata kiumri wamenizidi, lakini bado wananisikiliza ikiwa ni pamoja na kufanyia kazi maarifa ninayowapa!
Funzo kubwa nililojifunza ni hili; “dunia itakupokea vile utakavyokuja” hii ni sawa na kusema kwa chochote kile utakachokianzisha kama ni kizuri wewe anza kukifanya, dunia ipo tayari kukupokea kwa kwa hicho kitu.
Kumbuka dunia ni wewe ulivyo. Unachopaswa kujua ni kwamba dunia itaakisi masuala kadhaa kwako kutegemeana na vile ulivyo, ikiwa ni pamoja na kile unachokifanya!
Wacha nimtukuze Mungu katika hili, kwa maana 2023 umekuwa ni mwaka ambao najivunia kufanya mengi ikiwa ni pamoja na kufanikiwa kukamilisha kuandika vitabu vitabu vitano.
Hata hivyo nina furaha kubwa kwa kuwa nilifanikisha kuchapisha kitabu changu, nilichotoa bure kabisa, kama zawadi kwa wasomaji wangu, nilipokuwa nikifanya kumbukizi ya kuzaliwa kwangu.
Pengine labda wewe ni mwanafamilia mpya, na huenda ulipitwa na ofa ya kitabu hicho, unachotakiwa kufanya ni kuujibu ujumbe huu kwa kuandika neno KITABU, nawe utatumiwa; kwa maana ni haki yako kabisa kukipata na kukisoma.
Ninajivunia kuwa hivi nilivyo, na nina ujasiri wa kumtaja Mungu hadharani kwa sababu ametenda. Najua kuna wengine hamuwezi kumtaja Mungu hadharani, mimi ninamtaja kwa sababu pasipo yeye mimi siyo kitu; na ninayafanya haya yote kwa sifa na utukufu wa jina lake!
Nisipomtukuza Mungu nitakuwa mnyimi wa fadhila, ama hakika sifa zivume zirudi kwake Mumba wetu!
Zaburi 150:2 “Msifuni kwa matendo yake makuu; msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake!”
Mambo Unayapopaswa Uyafahamu Ukiuanza Mwaka Wako 2024…
Rafiki nakupa orodha ya mambo ambayo yafaa uyafahamu ikiwa bado ni mwanzoni sana mwa 2024...
1. Kila Safari Yenye Mafanikio Huanza Na Mungu...
Wahenga walipata kusema kuwa; “ukianza na Mungu utamaliza na Mungu.” Na, safari njema na yenye mafanikio ni ile ambayo inaongozwa na Mungu mwenyewe!
Rafiki, kabla hujaanza kufanya kitu chochote kile mwaka huu anza na Mungu kwanza. Ndiyo bosi, unatakiwa uanze siku mpya, wiki mpya, mwezi mpya pamoja na mwaka mpya na Mungu.
Unatakiwa umpe Mungu nafasi katika maisha yako, kwa maana yeye ndiye anayeujua mwanzo wako na mwisho wako.
Unatakiwa uanze na Mungu kwa sababu yeye ndiye anayejua ni wapi anakokupeleka.
Unatakiwa usijiamini sana wala kuziamini sana akili zako kwa maana zina ukomo, bali muamini Mungu kwa maana njia zake na Mawazo yake siyo sawa na Mawazo yako. Rejea Isaya 55:8
Rafiki, mwaka 2024 mpe Mungu nafasi, labda uwe huamini katika Mungu, na kama huamini katika Mungu nakupa pole!
Unatakiwa utenge angalau saa moja kila siku kwa ajili ya kuzungumza na Mungu wako; ikiwa ni pamoja na kusoma neno lake!
Zaburi 127:1 “Bwana asipoijenga nyumba waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji yeye aulindaye akesha bure.”
Kesho nitakuja na orodha ya mambo matano ya msingi sana ninayotamani uyajue ikiwa ni mwanzoni kabisa mwa mwaka 2024.
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment