SIFA KUU ZA MALENGO YA KIFEDHA...
Siyo kila jambo linalowekwa, linaloazimiwa au linalopangwa kufanyika hapo baadae linafaa kuitwa lengo!
Ili Lengo lolote lile liweze kuitwa lengo lazima liweze kuwa na sifa hizi zifuatazo!
NB: haijalishi litakuwa ni lengo la kifedha, kiafya, kimaisha au lengo lolote lile endapo litakosa sifa hisi basi hilo halitakuwa lengo bali litakuwa ni tamanio tu!
1. Malengo ya kifedha lazima yawe mahususi...
Ili lengo la kifedha lihesabike kama lengo lazima liwe mahususi!
Hii inamaanisha kuwa kile kiasi cha fedha kinachoazimiwa lazima kielezwe kwa uwazi!
Epuka kusema nataka kufanikiwa tu kifedha, sema unataka kufanikiwa kwa Kiasi gani.
Unatakiwa kujua kwamba sababu kubwa wengi huwa hatufanikiwi katika maisha ni kwamba hatujaweka wazi kile tunachotaka tukikamilishe!
Ndugu Unapaswa uepuke matarajio yenye ujumla bali kuwa na matarajio yenye ubayana.
Kwa mfano ninaazimia kufikia mwezi wa 12 mwaka huu 2024 niweze kuweka akiba ya shilingi 1,000,000/=
NB hii siyo motivation bali ni elimu unayopaswa kuwa nayo!
Weka wazi kiasi cha fedha unachokitaka maishani mwako! Ndipo sasa utaweza kutimiza lengo lako!
2. Malengo lazima yapimike, ili kukupa wepesi wa kufanya tathmini...
Ili lengo la kifedha lionekane kama ni lengo sharti lake liweze kupimika!
Huenda ukawa unajiuliza utalipimaje? Ukweli ni kwamba utalipima lengo lako la kifedha kwa kuangalia hatua uliyoifikia katika utekelezaji wake!
Ukiona umeweka Lengo la kifedha, lakini huwezi kulipima kwamba umefikia wapi katika kulitekeleza basi hapo lengo lako siyo halisi..
Hapa unashauriwa kutaja namba, kiasi au idadi ili uweze kubaini kama namba ulizozitaja unaweza kuzipima au laah!
Kwa mfano nitaweka akiba ya milioni moja kila mwezi, n.k.
NB: usifosi mambo angalia uwezo wako, usije ukaweka lengo la laki ili hali kwa mwezi uwezo wako ni kuingiza 50,000/=
Unatakiwa kujua kwamba utashindwa kupima lengo lako kwa sababu namba uliyoisema haiendani na uwezo wako!
3. Malengo Ya Kifedha lazima yawe yanatekelezeka...*
Ili lengo la kifedha lionekane kama ni lengo ni lazima liweze kutekelezeka...
Usiweke lengo la kifedha ambalo huwezi kulitekeleza.
Kwa mfano huwezi kusema unataka uweke milioni moja kwa mwezi, ilihali pato unalotengeneza kwa mwezi ni laki moja!
Je, sijui hiyo laki tisa hiyo utaitoa wapi?
Kwanini ujibebeshe msalaba mzito sana ambao huwezi kuubeba?
Unatakiwa kupanga malengo yanayoendana na uwezo wako my friend!
Kwa mfano kupanga kuwa baada ya miaka mitano uwe milionea ilihali bado unahangaika na mahitaji ya msingi ni malengo yasiyowezekana!
Unapaswa kujua kwamba kuweka lengo ambalo ni kubwa kuliko uhalisia litakukatisha tamaa!
NB, hii siyo motivation bali ni elimu unayopaswa kuwa nayo linapokuja suala la kufanikiwa kifedha!
4. Malengo lazima yawe na uhalisia...
Lengo lako la kifedha litaitwa lengo endapo litakuwa halisi...
Usiweke lengo la kifedha ambalo halina uhalisia hasa ukihusisha na pale ulipofikia kimaisha!
Kwa mfano unapata mshahara 200,000/= kwa mwezi na hauna chanzo kingine cha mapato halafu unaazimia kwamba utakuwa unaweka 500,000/= kila mwezi.
Hivi unamaanisha kwamba hizo hela nyingine utazipata wapi? Dear mentee kwa nini utafute msongo wa mawazo kinguvu?
Hii inamaanisha kwamba lengo lako halina uhalisia...
NB: unatakiwa kuwa na elimu hii ili uweze kufanikiwa kifedha
*5. Lengo la kifedha lazima liwe na ukomo wa Muda...
Ni muhimu kueleza ukomo wa muda ambao utatumika ili lengo lako la kifedha liweze kutimia.
Jaribu kufikiri umeweka lengo lakini hakuna ukomo wa muda ulioweka, kwa hiyo unamaanisha kwamba lengo lako ni la maisha au?
Je unataka lengo lako lifanikiwe baada ya muda gani?
Ndugu, unatakiwa kujua kwamba ukomo wa muda unaweza kuwa ndani ya muda wa masaa kadhaa, ndani ya siku kadhaa, ndani ya miezi kadhaa, ndani ya miaka kadhaa..
Unatakiwa ueleze ni muda gani hasa utakaohitajika ili lengo lako la kifedha liweze kutimia..
Usifanye lengo liwe la maisha kwani hakuna anayejua salio la maisha yake..
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e: Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Comments
Post a Comment