Je, Unajua ni Sababu Gani ambazo huwafanya watu wengi wajifunze Mambo yasiyofaa maishani mwao? Kama Jibu Lako Ni Hapana, Soma Hii...
Kwa mujibu wa kanuni ya matokeo na kichocheo inasema; “kila kitu hutokea kutokana na sababu”. Hii ni sawa na kusema kuwa, kuna kila sababu ambayo imepelekea watu wengi wajifunze vitu visivyo sahihi.
Na ifahamike kwamba kujifunza ni jambo ambalo linafanyika muda wote pasipo hiari. Hata sasa ubongo wako unaendelea kujifunza vitu vipya nikiwa naandika makala hii!
Kwa kusema hivyo hapo ulipo na vitu vyote vinavyokuzunguka mahali hapo ni vyanzo vinavyotoa taarifa mbalimbali zinazoingia ubongoni mwako!
Na taarifa hizo zikishaingia ubongoni mwako ndizo zitapima kile kitakachoendelea kwenye fahamu zako, yaani kuanzia: hulka, tabia, Imani, matendo pamoja na mitizamo yako, ile hali ya kuona mambo katika maisha!
Hata hivyo hakuna ambaye anaweza akauzuia ubongo wake usichukue taarifa kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vinavyomzunguka, kwa maana ni jambo ambalo haliwezekani!
Lakini kuna yupo mtu mmoja hivi mdadisi ambaye hataamini kila taarifa, huyu ndiye unayepaswa uwe na hiki ndicho ambacho Makala Hii inahusu!
Zifuatazo ni sababu ambazo zimefanya watu wengi waweze kujifunza vitu visivyo sahihi hata kama wamehitimu kutoka ngazi za juu na wana kiwango cha juu cha elimu!
1. Uwepo Wa Vyanzo Mbalimbali Vinavyotoa Taarifa Mbalimbali...
Moja ya kitu ambacho kimepoteza watu wengi katika dunia hii ya leo ni kelele! Unatakiwa kujua kwamba dunia ya sasa ina kelele nyingi sana kiasi kwamba, yule anayezisikia asipokuwa makini na akashindwa kuzichuja basi zitampoteza.
Ukweli ni kwamba kuna vyanzo vingi sana ambavyo vimekuwa vikitoa maarifa na taarifa mbalimbali kwa watu, lakini maarifa hayo na taarifa hizo zimekuwa hazimsaidii yule anayejifunza badala yake sasa zinampotosha na kumfanya ashindwe kusonga mbele!
Unatakiwa kuwa makini na vyanzo hivi ili kuulinda ubongo wako usiathirike, na una wajibu wa kuulinda ubongo wako usidhurike. Hata hivyo usipoulinda ubongo wako kutoka kwenye vyanzo hivi hakuna atakayefanya hivyo kwa ajili yako.
Rafiki unatakiwa kujua kwamba kuna watu wengi sana ambao wanateseka kwenye mahusiano, siyo kwa sababu wanatakiwa kuteseka ila ni kwa sababu wamepata taarifa na maarifa yasiyo sahihi kutoka kwenye vyanzo hivi.
Vilevile kuna watu wanateseka kiroho siyo kwa sababu wanatakiwa kuteseka, ila ni kwa sababu wamepata taarifa zisizo kamili kutoka katika vyanzo hivi!
Hata hivyo kuna watu wanateseka kiuchumi siyo kwa sababu wanatakiwa kuteseka, ila ni kwa sababu wamepokea taarifa zisizo sahihi kutoka kwenye vyanzo hivi!
Swali linakuja ikiwa wengi wao ni wasomi kabisa na bado wanateseka hivyo, je walijifunza nini? Si mnasema elimu ni ukombozi, je, elimu hiyo imewakomboaje hawa watu?
Ukweli ni kwamba vyanzo hivi vinatoa maarifa na taarifa ambazo hazijakamilika na ndiyo maana mbali na kuwa mtu kajifunza bado atajikuta akiendelea kukutana na magumu.
Vifuatavyo ni vyanzo hivyo:-
↪️Elimu/Shuleni
Mfumo wa elimu upo ulimwenguni kote, na ndiyo maana karibu kwenye kila jamii kuna utaratibu wa kupeleka Watoto shule ili wakajifunze.
Na mara baada ya watu hao kupokea mafunzo hutengenezwa na kuwa wasomi na wataalamu katika maeneno kadha wa kadha!
Hata katika jamii yetu wazazi wengi wameonesha mwitikio mzuri wa kupeleka Watoto shuleni lakini hakuna anayeuliza kwanini nimpleke mtoto shule.
Tafadhali Usinielewe vibaya sina maana kwamba kumpeleka mtoto shule ni kitu kibaya lahasha! Shida ipo kwenye kile anachofundishwa!
Kwa maana wanafunzi wengi wanajifunza maudhui ambayo hayawasaidii kwa sasa, na hata kwa maisha ya kesho zao zijazo!
Ubaya ni kwamba watoto hawa wamekuwa wakitumia muda mrefu sana katika kujifunza, ni Zaidi ya miaka 15.
Lakini cha kustaajabisha zaidi ni kwamba, mbali na kutumia muda wote huo, wengi wao huishia kujifunza mambo yasiyo na Msaada! Kwa kusema hivyo mara baada ya kuhitimu hujikuta wakitakiwa waanze upya!
Pasipo kulijua hili wazazi nao wamekuwa wakiwataka Watoto wao wasome kwa bidi wafaulu kwa kupata alama za juu, lakini hakuna anayedadisi huo ufaulu wa alama za juu utamsaidia nini huyo mtoto kwa hapo badae.
Hata hivyo mfumo huu umekuwa ukitengeneza watu wanaofaa kuajiriwa na siyo kuandaa watu watakaotengeneza kazi!
Ubaya ni kwamba ajira zenye zimekuwa hazitolewi hali ambayo imepelekea wengi washindwe kujikwamua kimaisha.
Hata hivyo mbali na kuwa watu hawa huwa ni wasomi lakini bado hawajui mambo mengi sana kuhusu maisha yao!
Na ndiyo maana sasa hivi kumekuwa na wimbi la wasomi wengi wasioweza kujimudu kimaisha kutokana na kujifunza vitu visivyo sahihi.
Ukija kuangalia hata katika nchi yetu tuna wasomi wa kutosha ambao wamejifunza vitu visivyo sahihi. Suala hili limechangiwa na kuwapitisha wasomi hao kwenye mfumo mmoja huku wakiwa wana vipaji tofuati, uwezo tofauti, karama tofauti, ndoto na malengo tofauti.
Hii inamaanisha kwamba kumfundisha mtu kitu kisichomsaidia kutimiza malengo yake, ni kumfundisha kitu kisicho sahihi na kumpotezea wakati.
Na ndiyo maana kuna muda utafika atatenga muda mwingine ili ajifunze kitu kingine kwa gharama nyingine. Swali linakuja vipi kama angefundishwa mapema?
Kitu kingine cha kuongezea hapa ni kwamba, shida imekuja hata kwa mwalimu anayewafundisha kwa maana hajui awaandaaje hao wajifunzaji, na hii ni kwa sababu jukumu alilopewa ni kufundisha tu lakini hajui anamfundisha nani.
Kwa kusema hivyo ni ngumu sana kwa mwanafunzi huyo kupokea maarifa na taarifa muafaka zitakazoendana na mapenzi yake.
Mbali na hilo mfumo wa elimu umekuwa ukiwapitisha wanafunzi kwenye mitaala iliyopitwa na wakati.
Kutokana na hilo mhitimu anahitimu akiwa na maarifa ya zamani hali ambayo inamfanya ashindwe kukabili uliwengu huu wa kisasa hasa ukihusisha na maarifa anayokuwa nayo kichwani mwake!
Ikumbukwe kilichoingia kama maarifa ndicho hupima kinachotoka yaani matokeo.
Kwa ujmla wengi wanasoma lakini kile wanachojifunza hakiwasaidii, kingekuwa kinawasaidia basi wangetumia huo usomi kutatua tatizo la ajira.
Sasa kama wasomi wenyewe wameshindwa kutatua tatizo hili ni nani atatatua, na je walijifunza ili waje wawe waajiriwa tu?
Ndugu mzazi, kabla hujampeleka mtoto shule tafadhali fanya upembuzi wa kina asije mtoto wako akaishia kujifunza vitu visivyo sahihi akaishia kukulaumu pamoja na kupotezewa muda.
Yafaa elimu itolewe kulingana na mapenzi ya mtoto hasa ukihusisha na uwezo wake pamoja na ndoto zake.
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!
Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentaship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0773284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment