Je, Unataka Kujenga Mahusiano Sahihi Yatakayodumu? Kama jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...

Bila shaka ulishawahi kupenda/kupendwa mpaka ukaona dunia imekuwa ndogo kiasi kwamba ukatamani kama kungekuwa na uwezekano, mngeongezewa nafasi nyingine ya dunia, au mngepewa dunia yenu ambayo mngeishi ninyi mkiwa wawili tu! 

Na, huenda ulishaweka mpaka ahadi ya kumpenda mwenzi wako maisha yako yote. 

Au, huenda mwenzi wako naye aliweka ahadi ya kukupenda maisha yake yote! Lakini mwisho wa siku upendo wenu haupo tena na ahadi zenu zote mlizoweka ziliishia njiani!

Hivi ushawahi kujiuliza ni kipi kilichopelekea safari yenu iishie njiani mbali na kuwa ilianza kwa mbwembwe kama zote? 

Unatakiwa kujua kuwa, mahusiano mengi hufa kwa sababu wanaoyaanzisha wanakuwa hawajui wanakoyapeleka ni wapi, na kwa vile huwezi ukajua kama umefika ikiwa huijui hatima unayotaka kuifikia, basi hiki ndicho hutokea kwenye mahusiano ya wapenzi hao! 

Hii ni sawa na kusema kwa vile hawajui hatima kamili ya mahusiano waliyoyaanzisha basi hujikuta wakishindwa Kwenda nayo mbali, matokeo yake mahusiano hayo hufa!

Na, ndiyo maana asilimia kubwa ya mahusiano mengi yanayoanzishwa hufa ukilinganisha na yale ambayo hudumu pasipo kuvunjika! Mwanzo wa mahusiano hayo huwa mzuri lakini mwisho wake huwa mbaya!

Huenda hata wewe ni miongoni mwa wale watu ambao wameweza kupitia hali ya sintofahamu kwenye mahusiano kiasi kwamba umeshalia sana, umeshaumia, umeshaumiza sana na huna tumaini lolote lile lililo jema kuhusu kumpata mwenzi sahihi Pamoja na mahusiano yatakayodumu.

Unatakiwa kujua kwamba kosa siyo kuumizwa wala kuachwa bali kosa ni kuingia kwenye mahusiano yasiyo sahihi. 

Ukweli ni kwamba kuna watu mpaka saa hii wapo kwenye mahusiano, lakini wao wenyewe siyo watu sahihi ijapokuwa wanahusiana, ubaya Zaidi ni kwamba wanahusiana na watu wasio sahihi, na, kwa wakati usio sahihi, hali hii imepelekea mahusiano mengi kutokuwa sahihi matokeo yake mahusiano hayo huvunjika. 

Rafiki, unatakiwa kujua kwamba siku hizi wimbo wa mahusiano umekuwa ukiimbwa sana, huku kila mtu akiwa anasema lake na walimu wa mahusiano wamekuwa wengi sana, huku kila mtu akiwa ana fundisho lake la kipekee, kutokana na hilo ukweli umepotoshwa na uongo ndiyo umepewa kipaumbele, hali ambayo imepotosha watu wengi katika sekta hii ya mahusiano.

Wahenga walisema “miluzi mingi humpoteza mbwa”, ukweli ni kwamba mafundisho mengi yamekuwa yakitolewa, lakini hayajamsaidia yule anayefundishwa na ndiyo maana mbali na kuwa na walimu wengi na maandiko mengi katika eneo hili la mahusiano lakini bado vilio, maumivu, mateso, malalamiko Pamoja na majuto vinazidi kushamiri kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele!

Hali hii imefanya watu wengi wawezebkuwa mtizamo potofu kuhusu mahusiano. Kwa mantiki hiyo watu wengi wanayaona mahusiano kama ni kitu kibaya! 

Unachopaswa kujua ni kwamba, endapo utaona hakuna mahusiano yanayodumu, huwezi kumpata mwenzi sahihi, mahusiano hayana maana yoyote ile, hutofurahia mahusiano maisha yako yote. Kitachotokea hapo ni kwamba utaishia kuvuta matukio hasi kwenye mahusiano yako Pamoja na kuvuta watu wa muda (wapitaji)!

Ukweli ni kwamba maisha yetu yanaongozwa kwa kanuni, na moja ya kanuni ambayo haijawahi kudanganya katika eneo lolote lile ni kanuni ya uvutano, ambayo inasema; “wewe ni kama sumaku inayoishi kwa hiyo unaweza ukavuta watu, matukio, pamoja na hali mbalimbali ambazo zinaendana na fikra kuu inayoongoza na kutawala maisha yako!

Hii ni sawa na kusema kwamba, kama fikra zako kuhusu mahusiano ni fikra hasi, basi fikra hizo ndizo zitavuta matukio hasi ya mahusiano maishani mwako.

Kwa mfano endapo umeona kwamba hakuna mtu sahihi, hakuna mahusiano yanayodumu, huwezi ukafurahia mahusiano, uliumbwa uteseke kwenye mahusiano, huna nyota ya kupendwa, mapenzi hayapo kwa ajili yako, wewe ni fungu la kukosa na mambo mengi kama hayo ndivyo utakavyovuta matukio hayo na kuyasogeza kwenye maisha yako yako. Kwa mantiki hiyo kwenye mahusiano yako utapokea matukio yanayoakisi kile ulichokiwasilisha.

Rafiki, unapowaza na kuona jambo Fulani liko hivi ama vile ubongo wako hulipokea kama ombi na kuanza kulichakata ambapo mwisho wa siku utakupa matukio yanayoakisi lile ombi ulilolipeleka. 

Haijalishi jambo hilo litakuwa baya zuri au zuri ili mradi wewe mwenyewe ndiye umelipeleka basi litapokelewa kama lilivyowasilishwa! 

Mpenzi msomaji, unatakiwa kujua kwamba hatua ya kwanza itakayokusaidia ili uweze kujenga mahusiano sahihi ni kubadilisha mitizamo yako Pamoja na mtindo wako wa kufikiri kwanza, endapo utaweza kufanya hivyo utaanza kuona upande wa pili wa sarafu, ambapo mwisho wa siku utagundua kwamba mahusiano sahihi yapo, na una haki ya kumpata mtu sahihi na unastahili kufurahia mahusiano maisha yako yote!

Hiki ndicho kitabu hiki kinaenda kufanya kwenye maisha yako, kwani kinaenda kukupa sura mpya kuhusu mahusiano hali itakayopelekea ubadili mitizamo yako, ambapo mwisho wa siku utagundua kwamba ni haki yako kufurahia maisha ukiwa na mwenzi wako.

Ikumbukwe ukipanda fikra utavuna kitendo, ukipanda kitendo utavuna tabia, ukipanda tabia utavuna utambulisho na ukipanda utambulisho utavuna hatima. 

Hii ni sawa na kusema endapo utapanda fikra nzuri kuhusu mahusiano utaanza kumtendea mema mwenzi wako, unavyomtendea mema utakuwa unajitengeneza kuwa na tabia njema kwake, unavyojitengeneza kuwa na tabia njema, ndivyo unavyomfanya akuone wewe ni mume/mke bora (mwenzi bora) na unavyozidi kuonekana kuwa ni mwenzi bora kwake ndivyo unavyotengeneza hatima ye penzi lenu kufika mbali.

Kumbe sasa matukio yoyote yale katika maisha yetu huanza kama fikra lakini mwisho wa siku huishia kututengeneza hatima Fulani kutegemeana na fikra tulizoziwasilisha! 

Nilikuwa nakuonjesha sehemu ndogo tu ya utangulizi wa kitabu changu!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e, Founder Wa King Mentaship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/ 0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...