Je, Unataka KUJUA Kwanini Mahusiano Mengi Huvunjika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...
Wadau walisema “kila kitu hutokea kutokana na sababu”. Hii ni sawa na kusema kuna kila sababu zinazopelekea kuvunjika kwa mahusiano mengi yanayoanzishwa.
Na, ukweli mchungu hakuna kitu ambacho huuma kama kuvunjika kwa mahusiano yanayohusisha wenzi wawili ambao walipendana kwa dhati, na walikuwa na ndoto za kufika mbali Zaidi!
Hata hivyo katika zama hizi kuvunjika kwa mahusiano halijawa jambo la kushangaza tena, bali limeonekana kama jambo la kawaida tu na watu wanalifurahia na kulishangilia!
Je, kipi hasa ni chanzo cha mahusiano mengi kuvunjika? Fuatana Pamoja nami:
1. Kupuuza Unganiko La Kiroho Kabla Ya Kuanzisha Mahusiano...
Mwanadamu ni roho, nafsi na mwili. Mwili ni kama nyumba tu lakini mwanadamu halisi ni roho.
Ukweli ni kwamba watu wengi wanahusiana kimwili na si kiroho, na ndiyo maana mahusiano hayo yamekuwa yakivunjika kwa sababu hayana unganiko la kiroho.
Hata hivyo watu hawa hata wanapoanzisha mahusiano huwa hawaanzi na Mungu, badala yake huanza kwanza na kutimiza hila za shetani kwa kufanya uasherati na uzinzi.
Na, mara baada ya kufanya hivyo, endapo itatokea mambo yakienda kombo ndipo hurudi na kuanza kumlilia Mungu.
Rafiki, asili ya shetani ni mvurugaji, hii ni sawa na kusema, hatashindwa kuvuruga na kuharibu mahusiano yako ikiwa ndiye umeanza naye!
Hata hivyo waswahili walisema “ukianza na Mungu utamaliza na Mungu”.
Hii ni sawa na kusema “ukianza na shetani utamaliza na shetani”. Sasa kama hukuanza na Mungu inakuwaje umalize na Mungu?
Jaribu kuvuta picha kwenye hayo mahusiano yako kama yana unganiko la kiroho na Mungu, au ulianza pasipo Mungu.
Hata hivyo sipo hapa kukulazmisha kwamba ni lazima ukubaliane na ninachokisema, lakini ninataka utambue kwamba Mungu anakujua vizuri na huenda ungeanza naye, basi angekupa busara na hekima ambazo zingekusaidia umpate huyo aliyeumbwa kwa ajili yako.
Unapopuuza hitaji la kiroho maana yake umefuata hitaji la kimwili, na kwa vile mwili huwa hautosheki, basi ni rahisi kwa mahusiano hayo kufa.
Kumbuka nia ya mwili ni mauti, huku nia roho ya ikiwa ni uzima. Hivyo basi endapo utautii sana mwili ni rahisi kuvunja mahusiano kwa sababu mwili haujawahi kutosheka!
Mpenzi msomaji unatakiwa kujua kuwa, kilichoounganishwa kiroho hakiwezi kutenganishwa bali hudumu hata milele, ikiwa kilichounganishwa kimwili huweza kutengenishwa hasa pale ambapo vitu vya kimwili vilivokuwa vimeunganisha mahusiano hayo kutokuweka.
Kwa mfano baadhi ya vitu ambavyo huwaunganisha watu kimwiili ni kama vile: uzuri, mvuto, umbile na mng’ao ni vitu vya muda tu, kwa hivyo endapo ndivyo vilitumika kama vigezo vya kuingia kwenye mahusiano, basi endapo itatokea vimetoweka thamani ya upendo hushuka matokeo yake mahusiano hayo huvunjika!
Kwa ujumla kupuuza hitaji la kiroho ndiyo imekuwa sababu kuu ya mahusiano mengi kuvunjika. Na, ifahamike kwamba ndoa ni taasisi iliyoasisiwa na Mungu mwenyewe.
Hivyo basi inapotokea tumeanzisha mahusiano pasipo kuanza na chanzo chetu (Mungu) ni rahisi kupoteza dira na uelekeo.
Tumekuwa siyo watu wa kuanza na Mungu tena, bali tunaanza kutimiza tamaa za kimwili kwanza ndiyo maana mahusiano mengi yanayoanzishwa yanakufa!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentaship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0773284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment