Je, Wewe Ni Mjifunzaji Mzuri Lakini Umeishia Kujifunza Vitu Visivyo Sahihi? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...

Hivi unafahamu kwamba Zaidi ya asilimia 80 ya watu wametumia muda wao mwingi kujifunza lakini wameishia kujifunza vitu visivyo sahihi? 

Ukweli ni kwamba watu wengi chini ya mwamvuli wa elimu na mafunzo wameishia kujifunza vitu visivyo na msaada, na ndiyo maana mwisho wao umekuwa ni: mateso, shida, taabu, magumu na mapambano kwa sababu kile walichojifunza hakijaweza kuwarahishia maisha!

Lengo kuu la kujifunza ni kutumia kile ulichojifunza ili kurahisisha maisha yako, kwa hiyo inapotokea umejifunza lakini bado hujaweza kuyarahishisha maisha yako kupitia kile ulichojifunza, maana yake huenda kile ulichojifunza hakijakusaidia katika lolote lile.

Unachopaswa kujua ni kwamba, siyo kila kinachofundishwa kinafaa kulishwa kwenye ubongo wako. Hata hivyo, huna budi kufahamu kuwa, kama vile unavyokuwa kimwili kutokana na kile unachokula, vilevile unakuwa kimaisha kulingana na kile unachoulisha ubongo wako.

Ukweli ni kwamba siyo kila funzo linafaa na siye kila anayefundisha anafaa. Kabla hujaruhusu jambo Fulani lizame akilini mwako yafaa ujiulize hili; je, jambo hilo ni nini na huyo anayefundisha ni nani, anakufundisha nini na ili iwe nini?

Kinachonistaajabisha Zaidi ni kuwa, dunia ya sasa ina wasomi, wabobevu na wataalamu katika maeneo mengi lakini bado ina ujinga mwingi!

Kadhalika, mbali na dunia ya sasa kuwa na wigo mpana wa kupata maarifa na taarifa za kila eneo linalohusu maisha ya mwanadamu lakini bado ina wajinga wa kupindukia.

Kutokana na hilo, siyo kila chanzo kinachotoa maarifa kinatoa maarifa sahihi, kuna vingine vinatoa maarifa yanayoangamiza na kukua kabisa fahamu za wengi!

Na ndiyo maana sasa hivi limekuwa ni jambo la kawaida kukutana na msomi ambaye hawezi akazungumza jambo lenye mantiki, suala hili limechangiwa na mtu huyo kufundishwa mambo yasiyo sahihi. Kwa kusema hivyo kumbe tatizo siyo usomi wake bali tatizo ni kile alichojifunza kwenye huo usomi wake!

Kuna baadhi ya watu wanafanya mambo ya ovyo siyo kwa sababu wanatakiwa kufanya mambo ya ovyo ila ni kwa sababu wamejifunza masuala ya ovyo na ndiyo maana mwisho wao umekuwa ni kuwa watu wa ovyo vilevile!

Kuna baadhi ya watu wanajiona hawawezi siyo kwa sababu hawawezi ila ni kwa sababu wamefundishwa na wamejifunza kwamba wao hawawezi, lakini haimaanishi kuwa hawawezi kweli.

Kuna baadhi ya watu wanaona hawastahili kuwa watu wa hadhi Fulani siyo kwamba hawastahili kweli, ila ni kwa sababu wamefundishwa na wamejifunza hivyo, lakini haina maana kuwa hawastahili.

Rafiki unatakiwa kujua kwamba mafunzo unayoyapokea huenda kuathiri moja kwa moja mfumo wako wa Imani ikiwa ni pamoja na mitizamo yako.

Kutokana na hilo ndiyo maana ni ngumu sana kumpata mtu ambaye huwa kinyume na kile ambacho amejifunza/amefundishwa. Kwa kusema hivyo wengi ni matunda ya kile walichojifunza. 

Na ndiyo maana watu wengi huwa hawaamini wanachokiona, bali hukiamini kile walichoaminishwa kupitia mafunzo waliyoyapokea!

Mbali na hilo kanuni ya kinachotoka na kinachoingia inasema; “kile kilichoingia ndicho hupima kinachotoka”, kwa kusema hivyo hakuna mtu ambaye huenda Zaidi ya pale alipoishia kujifunza. 

Na ndiyo maana kuna usemi maarufu usemao; “kile unachokijua ndicho ambacho hupima umbali unaoweza Kwenda kimaisha”. 

Hata hivyo katika hali ya kawaida, mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu wake maarifa endapo hataenda Zaidi ya pale mwalimu wake atakapoishia kumfundisha, na hii ni kwa sababu pale mwalimu wake alipoishia ndiyo ukomo wa maarifa kwa mwanafunzi wake.

Kwa kusema hivyo, maarifa tunayoyapata yana ukomo, na kwa vile yana ukomo inamaanisha kwamba tunafika sehemu tunashindwa kuendelea Zaidi, kwa sababu kile kilichomo kwenye fahamu zetu hakituruhusu Kwenda mbele Zaidi. 

Kumbe sasa ili ufanikiwe unatakiwa ukachimbe Zaidi ya pale ulipoishia kufundishwa.
Ukweli ni kwamba dunia ya sasa ina watu wengi ambao wamejifunza mambo yasiyo sahihi, yasiyoendana na wao walivyo kiuwezo pamoja na kujifunza mambo ambayo yamepitwa na wakati hasa ukilinganisha na dunia tuliyo nayo sasa!

Kumbe kwenye kujifunza kuna kuchanganywa, hali hii hutokea pale ambapo mjifunzaji hajafundishwa mambo sahihi, kutokana na hilo huishia kuwa mtu wa kawaida tu kwa sababu amepewa mafunzo yaliyomfanya aishie kuwa mtu wa kawaida lakini huenda yeye siyo mtu wa kawaida kabisa, kwa sababu wengi wetu ndani yetu tunamiliki vitu visivyokuwa vya kawaida kabisa!

Bila shaka hata wewe umeweza kujifunza na huenda hata sasa unajifunza, kwa maana hatutakiwi kuacha kujifunza, kwa sababu maisha hayaachi kutufundisha na ifahamike kwamba, maisha ni mwalimu wa yote.

Kumbe hatupaswi kuacha kujifunza, lakini yafaa tujipe tathimini kuwa tunajifunza nini na iwe nini baada ya kujifunza!

Sijui kwanini unasoma makala hii,  lakini uamuzi ulioufanya wa kusoma makala hii ni uamuzi mzuri sana kuwahi kuufanya, na hii ni kwa sababu uamuzi huo unaenda kukufanya upokee nuru mpya ambayo inaenda kukupeleka kwenye kweli yote kuhusu kujifunza, na ndani ya muda mfupi utaenda kujifunza vitu vitakavyobadili maisha yako.

Katika somo hili utaenda kujifunza maana halisi ya kujifunza, kwanini watu wengi hujifunza vitu visivyo sahihi, ni nini athari ya kujifunza vitu visivyo sahihi na nini kifanyike ili uweze kujifunza vitu sahihi.

NB: Nitakuwa natoa hili somo kwa mwendelezo mpaka pale utakaporidhika!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentaship Program, Mwl, mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...