Tahadhari Huwezi Kuelewa Kujifunza Ni Nini Mpaka Usome Kwanza Hii...
Bila shaka ushawahi kusikia neno kujifunza, na huenda hata wewe umeshajifunza vitu kadhaa maishani mwako. Kwa kusema hivyo endapo utaulizwa ufafanue maana ya neno kujifunza, pasi na shaka hutakosa cha kusemea.
Kwa tafsiri nyepesi neno kujifunza linaweza kufafanuliwa kama; kitendo cha kuchukua ujuzi, taarifa, maarifa au wazo kutoka chanzo fulani na kisha kupeleka ubongoni.
Na mara baada ya ubongo kupokea funzo hilo kuna mabadiliko ya haraka sana ambayo hutokea kwenye maisha ya yule aliyejifunza.
Hii ni kwa sababu, kilichoingia kama funzo hubadilisha kile kitakachotoka kama matokeo. Kwa mantiki hiyo, mtu huyo atajikuta akibadilisha hata matokeo anayoweza kuyaleta kwa kutumia maarifa ya kile alichojifunza!
Na ndiyo maana watu wengi hubadili maisha yao mara baada ya kujifunza. Kwa kusema hivyo mtu huyo hujikuta akianza kuratibu matendo yake yalandane na kile alichojifunza.
Kitu unachotakiwa kuzingatia hapa ni kile unachojifunza! Kama utakuwa umejifunza yale yasiyofaa utaanza kufanya yale yasiyofaa! Hata hivyo endapo utakuwa umejifunza yanayofana utaanza kufanya yanayofaa!
Unatakiwa kujua kwamba umeumbwa na ubongo ili ujifunze na ukishajifunza utaulinda ubongo wako.
Na ifahamike kwamba, moja ya mbinu sahihi ya kuulinda ubongo wako ni kupitia kujifunza Vitu sahihi! Na endapo hutajifunza vitu sahihi utaharibu ubongo wako...
Ukweli ni kwamba una wajibu wa kuulinda ubongo wako kwa kuutafutia maarifa sahihi, na usipofanya hivyo hakuna atakayefanya hivyo kwa niaba yako, matokeo yake sasa ubongo wako utaharibiwa!
Hata hivyo ugunduzi mkubwa uliowahi kugunduliwa kuhusu eneo hili la kujifunza, ni kwamba unaweza ukajifunza chochote kile na ukawa yeyote yule, kwa mantiki hiyo huna budi ujifunze kujifunza.
Mbali na hilo, ili mwili wako uweze kukua na kuwa na afya njema unahitaji chakula, vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwenye ubongo, hii ni sawa na kusema kuwa, ili uweze kupata afya ya akili unahitaji kujifunza kila iitwapo leo.
Hoja inayozungumiwa hapa ni kwamba wengi wetu tumeshindwa kuwa akina sisi halisi kwa vile maarifa tuliyonayo, hayajatosha kuthibitisha uhalisia wetu, hata hivyo wengi wetu tumejifunza vitu visivyo sahihi ndiyo maana tumeshindwa kuwa akina sisi halisi!
Jifunze ujijue! Kuna mengi Katika kujifunza, wahenga wana msemo unaosema; "utavuna ulichokipanda".
Hivyo basi endapo utapanda maarifa, ujuzi, taarifa sahihi pamoja na mawazo chanya ni dhahiri utakuja kuvuna mafanikio. Unatakiwa kujua kwamba kama hutojifunza maana yake hakuna utakachokuwa umekipanda hivyo utaambulia patupu.
Vilevile mwandishi nguli wa masuala yahusuyo uchumi na fedha bwana Robert kiyosaki, katika kitabu chake kilichouza zaidi duniani "Rich Dad Poor Dad", aliandika kuwa;
"Maisha ni mwalimu wa yote". Hivyo basi, kama maisha ni mwalimu wa yote, na kazi ya mwalimu huwa ni kufundisha. Basi na wewe hutakiwi kuchoka kujifunza kwa sababu kila siku maisha yatakupa somo na funzo jipya.
Mwisho kabisa hakuna ambaye ameumbwa hana uwezo wa kujifunza na kwa kuwa kujifunza ni hitaji lako la msingi hivyo ukilikosa umekosa vingi.
Fahamu Kuhusu Sehemu Za Ubongo Zinahusika Katika Ujifunzaji…
Wanasayansi wa masuala ya ubongo (neuroscientists) katika kufanya tafiti jinsi gani ubongo wa binadamu unafanya kazi, wamebaini kuwa ubongo una sehemu kuu nne ambazo husaidiana katika utendaji kazi na kumfanya binadamu ajifunze kwa urahisi. Sehemu hizi ni kama zifuatazo:-
Conscious Mind (Akili Fahamu)
Sehemu hii ni sehemu ya ubongo ambayo kazi yake kubwa ni kuchukua wazo, dhana, taarifa, Mawazo, funzo kwa kutumia milango ya fahamu, baada ya hapo hukiamini kwanza kile kilichokuliwa kwanza kuwa ni kweli.
Ukweli ni kwamba hii ni sehemu ya ubongo ambayo ni maalumu kwa ajili ya kujifunza. Hivyo basi hata kujifunza kunakozungumziwa hapa, huanzia kwenye sehemu hii ya ubongo, ambapo mtu atakusanya taarifa kutoka sehemu mbalimbali na kuziingiza ubongoni mwake.
Unatakiwa kujua kwamba kujifunza huku kunaweza kufanyika pasi na hiari, bali ubongo wako ukachukua taarifa kutoka mazingira uliyopo na kuziamini, haijalishi taarifa hizo zipoje!
Basal Ganglia.
Hii ni sehemu ya ubongo ambayo huratibu hisia, kuhifadhi kumbukumbu pamoja na kuhusanisha vitu na matukio mbalimbali.
Kwa mfano kama umeanza kujifunza kila siku kwa kutumia conscious mind basi sehemu hii ya ubongo itahifadhi taarifa hiyo. Hivyo basi kadri ya unavyozidi kurudia kujifunza ndivyo sehemu hii inavyorahisisha na kufanya suala la kujifunza liwe rahisi sana kwako.
Pia sehemu hii ni muhimu kwa sababu itakuwa inakurejeshea kumbukumbu kuhusu yale yote unayojifunza na kufanya kazi ya kujifunza iwe rahisi!
Subjective Mind.
Hii ni sehemu ya ubongo inayoratibu matendo yako na maneno yako yaendane na kile ulichojifunza.
Kwa kusema hivyo sehemu hii itakufanya ubadili vile unavyojiona yaani kujitambua kwako pamoja na hali uliyonayo kwa wakati huo kuanzia: imani yako, hofu na furaha.
Mbali na hilo sehemu hii hutawala jinsi maneno yako na matendo yako yanavyolandana na hali uliyonayo kwa wakati huo.
Ukiachilia hilo, sehemu hii huhusanisha yale mafunzo unayojifunza yaendane na mfumo wa maisha yako.
Superconcsious Mind.
Hii ni sehemu ya ubongo ambayo imeunganika na maarifa yasiyo na ukomo, sehemu hii ya ubongo ina maarifa yote, mbinu, njia na majibu ya maswali ambayo katu hukuwahi kujiuliza.
Mbali na hilo sehemu hii ya ubongo inafanya kazi kwa masaa ishirini na nne (24). Mwisho kabisa sehemu hii ya ubongo ndicho chanzo cha hamasa, tafakuri na uwezo wa kujifunza pasipo chanzo chochote kile (intuition).
Unatakiwa kujua kwamba ukianza kujifunza kuna baadhi ya ufahamu huwa unakuja automatiki tu. Ukweli ni kwamba, sehemu hii ya ubongo ndiyo hukusaidia uweze kupata ufahamu huo.
Je, binadamu huzaliwa akiwa anajua? Je, kuna makundi mangapi ya watu kutokana na vile walivyojifunza?
Haya yote utayajua siku zijazo kwenye mwendelezo wa makala hii...
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentaship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment