Jinsi Ambavyo Jamii Hupelekea Watu Wajifunze Vitu Visivyo Sahihi...

Neno jamii linamaanisha muunganiko wa koo mbalimbali zilizo tofauti zinazokaa katika eneo Fulani la kijiografia, zinazochangia sifa Fulani Fulani hivi fananifu kama vile: lugha, historia moja, uongozi mmoja pamoja na mila na desturi.

Na, kwa vile jamii huchangia sifa Fulani hivi fananifu, hii inamaanisha kwamba hata Imani yake na mitizamo yake huwa inafanana kwa jamii yote!

Na, ndiyo maana ni rahisi sana kuweza kuigundua jamii ya watanzania kwa kuangalia mtindo wao wa kuishi ulivyo.

Na kwa vile jamii hujumuisha watu wengi, maana yake ndani yake kuna mengi ya uozo yanayofanyika. 

Na, ifahamike kwamba suala la kujifunza lipo automatiki, kwa kusema hivyo kupitia jamii tuliyonayo kuna watu wamejifunza vitu visivyo sahihi kama vile vinavyofanywa na baadhi ya wanajamii!

Ukweli ni kwamba chini ya mwamvuli wa jamii kuna watu wamejifunza kuwa, kwa vile wamezaliwa kwenye jamii maskini hawawezi kufanikiwa kifedha na kimaisha kiujumla. 

Kadhalika chini ya mwamvuli wa jamii kuna watu wamejifunza kuwa wanawake hawapaswi kuwa viongozi wakubwa badala yake wawe watiifu tu kwa waume zao, kitu ambacho hakina ukweli wowote ule!

Hata hivyo chini ya jina la jamii kuna watu wamejifunza mwamba ili ufanikiwe kifedha lazima utoke nje ya Tanzania uende mataifa ya ulaya, huku ukweli ukiwa hata utajiri wa mataifa hayo unategemea sana nchi za kiafrika. 

Sambamba na hilo chini ya mwamvuli wa jamii kuna watu wamejifunza kwamba wazungu wana akili kuliko sisi, kwa hiyo ni kawaida sana kwetu kuwa chini yao kitu ambacho siyo sahihi. Kwa maana hata sisi tunaweza tena tu bora kama wao walivyo bora!

Mbali na hilo chini ya jina la jamii kuna watu wamejifunza kuwa mwanamke ni chombo kinachopaswa kikae nyumbani tu, hakitakiwi kuzalisha wala kujihusisha na chochote kile. 

Kitu kisicho na ukweli wowote ule, kwa maana kuwa mwanamke au mwanaume ni kama lebo tu, lakini kila mtu ana uwezo wa kufanya mambo makubwa tu haijalishi ni mwanaume au mwanamke!

Pia chini ya jina la jamii kuna watu wamejifunza kwamba ili ufanikiwe katika maisha ni lazima uroge kwanza. Ilihali mafanikio halisi huja kutoka kwa Mungu mara baada ya kutunza amri zake!

Ukiachilia mbali hilo chini ya mwamvuli wa jamii kuna watu wamejifunza kuwa walevi, wadangaji na makahaba, na hii ni kutokana na baadhi ya wanajamii kuyafanya hayo yote hadharani. 

Vilevile chini ya jina la jamii kuna watu wamejifunza kuwa wezi, waporaji, wanyang’anyi na walevi, kwa sababu ni vitu vinavyofanywa na baadhi ya wanajamii!

Je, hayo yote si yanafanyika kwenye jamii Au Mimi ni mzushi? 

Na kama yanafanyika maana yake kupitia hayo kuna watu wanajifunza mambo yasiyofaa. Hii ni kwa sababu endapo yangekuwa hayafanyiki hakuna mwanajamii hata mmoja ambaye angejifunza! 

Maadamu yanafanyika, na ndiyo maana wanaoyafanya wanaongezeka kadri siku zinavyozidi kusonga mbele!

Ukweli ni kwamba haya yote yanafanyika kwenye jamii yetu, na kwa vile yanafanyika inamaanisha kwamba ubongo wa mwanajamii utayachukua hayo yote na kuanza kumchochoea mwanajamii huyo afanye vivyo hivyo.

Rafiki, wewe pekee siyo jamii yote, lakini u sehemu ya jamii. Na ifahamike kwamba, neno jamii ni wingi wa watu, na umoja wa watu ni mtu.

Kwa kusema hivyo mtu ni jamii. Hivyo basi kama wewe u sehemu ya jamii, huna budi kuachilia baadhi ya mitizamo isiyokuwa na manufaa halafu uanze kubadili maisha yako. 

Na ukishabadili mtizamo wako jamii yote itabadilika, kwa sababu watu watabadilika kupitia wewe! 

Na itapendeza sana endapo jamii yote itatengenezwa upya kimtizamo ili ibadili matokeo itakayoyaleta. 

Kwa sababu huwezi ukabadili matokeo ambayo jamii itakayoyaleta pasipo kuibadili kimtizamo kwanza. 

Na ndiyo maana nimeandika makala hii ili iwe kama chachu itakayoleta mabadiliko kwa jamii.

Nikutakie mapambano mema ndugu Mtanzania!

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!

Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentaship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...