Jinsi Ambavyo Marafiki Hupelekea Watu Wajifunze Vitu Visivyo Sahihi...
Mtu mmoja mwenye busara aliwahi kusema kuwa; “vile utakuwa miaka mitano ijayao itategemeana na marafiki ulionao pamoja na vitabu unavyosoma”.
Sote tumeona kwenye hiyo nukuu kuna neno marafiki. Huenda ukawa unajiuliza kwanini marafiki?
Unatakiwa kujua kwamba akili yako inajua jinsi ya kuendana na wengine, kwa mantiki hiyo unapochangamana na marafiki fulani Fulani hivi maana yake akili yako itakusukuma na wewe uenende kama wao wanavyoendana, kwa sababu ni vitu ukavyojifunza kutoka kwao.
Unaweza ukawa unajiuliza kwanini akili yangu hujifunza kutoka kwa marafiki zangu?
Jibu ni jepesi tu, jambo hili la kujifunza hufanyika ili kukuwezesha ukubalike kwenye kundi la marafiki unalohusiana nalo.
Kwa kusema hivyo, endapo marafiki zako watakuwa ni watu wenye mitizamo hasi, ni watu wenye mienendo mibovu, ni watu wasiojali kesho zao hata wewe utajifunza na kuwa kama wao walivyo!
Ukweli ni kwamba kuna baadhi ya watu ambao kabla hawajawa na aina fulani hivi za marafiki, walikuwa ni watu wema, wazuri, na wenye malengo ya kuona mbele maishani mwao.
Lakini mara baada ya kuanza kuchangamana na baadhi ya marafiki wamejikuta wakipoteza uelekeo maishani mwao kwa kujifunza, yasiyofaa.
Unatakiwa kujua kwamba chini ya jina marafiki kuna watu wamejifunza kuwa walevi, na wanalewa kila muda, na kila ukiwakuta wananuka pombe utafikiri wanamiliki kiwanda cha kutengeneza pombe mwilini mwao!
Hata hivyo chini ya jina la kutunza marafiki kuna watu wamejifunza kuwa wazinzi na waasherati. Na ndiyo maana uzinzi na uasherati unashangiliwa sana siku hizi!
Mbali na hilo chini ya mwamvuli wa marafiki kuna watu wamejifunza kutokuwa waaminifu. Ndiyo maana siku hizi imekuwa ni ngumu sana kumpata mtu aliye muaminifu!
Ukiachilia mbali hilo chini ya jina marafiki kuna watu wamejifunza kuwa wavivu. Na ndiyo maana kizazi hiki hakipendi kazi zaidi ya kutafuta ishara na miujiza isiyowezekana!
Kama hilo halitoshi chini ya mwamvuli wa marafiki kuna watu wamejifunza kuwa hawawezi kubadili maisha yao. Na ndiyo maana kuna watu utawakuta wakikaa wakisubiri mambo yatokee badala ya kufanya mambo yatokee!
Kwa kuongezea chini ya mwamvuli wa marafiki kuna watu wamejifunza kuwa wadangaji. Bila shaka hapo ulipo kuna wadangaji wengi tu, na huu ndiyo ukweli wa Mambo!
Kadhalika chini ya mwamvuli wa marafiki kuna watu wamejifunza kutokujali chochote kile maishani mwao. Hawa ndiyo waumini wakubwa wa ile falsafa inayosema; "liwalo na liwe"
Si hivyo tu lakini pia chini ya mwamvuli wa marafiki kuna watu wamejifunza kutokuwa watu wa mipango maishani mwao. Watu hawa hawajui kwamba kushindwa kupanga ni kupanga kushindwa!
Hata hivyo chini ya mwamvuli wa marafiki kuna watu wamejifunza kutumia muda wao vibaya na kutokuthamini kabisa muda walionao. Ubaya ni kwamba watu hawa hawajui kuwa, muda uliochezewa ni maisha yaliyochezewa!
Ukiachilia hilo chini ya mwamvuli wa marafiki kuna watu wamejifunza kuwa waghairishaji wa mambo. Wasijue kuwa kughairisha mambo huwa hakufanyi jambo lililoghairishwa lijitekeleze lenyewe!
Mbali na hilo chini ya mwamvuli wa marafiki kuna watu wamejifunza kuwa maisha yao yatabadilishwa na mifumo itokayo nje. Wasijue kuwa mifumo ya nje haijatengenezwa iwanufaishe zaidi ya kuwanyonya!
Vilevile chini ya mwamvuli wa marafiki kuna watu wamejifunza kuwa wao siyo kitu hivyo hawawezi kufanya mambo yatokee, badala yake sasa wanatakiwa wakae tu wakisubiri mambo yatokee, ilihali mambo hayawezi kutokea pasipo kuyafanya kwanza yatokee.
Kadhalika chini ya mwamvuli ya marafiki kuna watu wamejifunza kuwa hawawezi kufanikiwa kifedha. Wasijue kuwa kila jambo linawezekana endapo utaamua!
Hata hivyo chini ya mwamvuli wa marafiki kuna watu wamejifunza kuwa hawawezi kupata mahusiano sahihi na yatakayodumu. Wasijue kuwa tatizo siyo mtu sahihi bali tatizo ni fikra hasi zilizopo kwenye fahamu zao!
Pia chini ya jina la marafiki kuna watu wamejifunza tabia za unayanyasaji kwa wake zao, familia zao na Watoto wao! Wasijue kuwa busara imetufundisha kwamba familia ndicho kiwe kipaumbele chako!
Rafiki, kila mtu wako wa karibu ana ushawishi kwako, na ushawishi huo unaweza kuwa mbaya au mzuri.
Lakini kwa vile wengi wetu marafiki zetu ni watu wa kawaida tu, ndiyo maana huwa tunaishia kuharibikiwa maishani.
Unatakiwa kujua kuwa urafiki unaweza ukaleta ulemavu kwenye akili yako, si haba endapo utajikuta ukilemaa na kujikuta; ukizungumza kama marafiki zako wanavyozungumza, ukihofia wanachokihofia, ukila wanachokula, ukifanya wanachokifanya, ukiwaza wanachokiwaza, ukiamini wanachokiamini, ukiona wanachokiona na ukifanya kila kitu maishani mwako kama vile ambavyo wao wanakifanya!
Kumbe sasa wengi wetu ni matunda ya marafiki zetu. Na ndiyo maana wahenga walisema; “ndege wanaofanana huruka pamoja”.
Kwa kusema hivyo wale unaoshinda nao ndio watakaokufanya uwe kama wao.
Hitimisho; kukutana na watu ni jambo lisiloepukika, lakini kumruhusu yupi abaki kwenye maisha yako ni jambo linalohitaji utumie utashi wako.
Daima kuwa makini kwa maana kila mtu unayeshinda naye anaweza kukufanya ujifunze vitu Visivyo Sahihi...
Ahsante Sana Kwa kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri.
Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentaship Program, Mwl, Mwandishi Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284339/0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment