Jinsi Ambavyo Mazingira Hupelekea Watu Wajifunze Vitu Visivyo Sahihi...

Vitu vingi ambavyo mwanadamu anavifanya vinatokana na msukumo wa mazingira yanayomzunguka mwanadamu huyo! 

Kwa kusema hivyo mtu huyo atajikuta akifanya baadhi ya tabia si kwa sababu anatakiwa afanye tabia hizo bali atajifunza kufanya tabia hizo kama moja ya mbinu ya kuyakabili na kuingiliana na mazingira yanayomzunguka!

Sasa hapa itategemeana na aina mazingira yanatakayokuwa yanamzunguka mtu huyo aidha ni mazingira mazuri au mazingira mabaya!

Na ifahamike kwamba, mazingira ni nguvu isiyoonekana ambayo humtawala mwanadamu kifikra, kimaono, kimatendo, kimtizamo na kimienendo. 

Ukweli ni kwamba kila mtu ni tunda linalotokana na mazingira anayotokea. Hii ni sawa na kusema kuwa, hivyo ulivyo ni kutokana na kile ulichojifunza kutoka kwenye mazingira unayotokea.

Unatakiwa kujua kwamba kuna watu wamekuwa na fikra za uhaba/mgando kwa sababu ni kitu ambacho wamejifunza kutoka kwenye mazingira walimokulia, lakini haimaanishi kwamba walitakiwa wawe hivyo! 

Ukiachilia mbali hilo, kuna watu wamekuwa na fikra zenye ukomo hali ambayo imepelekea washindwe kupiga hatua kimaisha, si kwa sababu wanatakiwa wapige hatua ndogo kimaisha bali ni kwa sababu mazingira yaliyowakuza yamewafanya hivyo.

Na ifahamike kwamba, huwezi ukafanya jambo litakaloenda mbali zaidi ya mazingira uliyopo!

Kadhalika kuna watu wamebaki kuwa na fikra duni, hali ambayo imewafanya wajidumaze na kujilemaza katika kuishi kwao, kwa sababu ni kitu ambacho wamejifunza kwenye mazingira wanamotokea!

Hata hivyo kuna watu wamekuwa: walevi, wapenda anasa na wahuni kwa sababu ni vitu ambavyo wamejifunza kwenye mazingira yanayowazunguka, hususani mazingira yaliyozungukwa na baa pamoja na majumba ya starehe, kwa maana huweza kumchochea na kumfanya mtu ajifunze kuwa mpenda anasa.

Vilevile kuna watu wamejifunza kuwa wazinzi, wadangaji pamoja na kujiuza, kwa sababu ni vitu walivyopo kwenye mazingira yao wanayoishi!

Hususani mazingira yaliyozungukwa na wanawake wanaojiuza na wadangaji humchochea na kumfanya mtu ajifunze kuwa muasherati.

Ukweli ni kwamba mambo yote yanayopatikana kwenye mazingira uliyopo, huchukuliwa kama taarifa au dhana ambazo huingizwa moja kwa moja kwenye ubongo wako. 

Matokeo yake ubongo wako utachakata taarifa hizo na kukuchochea uweze kuenenda na kutenda sawasawa na kile ulichojifunza!

Kinachosikisitisha na kuhuzunisha zaidi ni kwamba, kitendo hiki cha uchukuaji taarifa hufanyika pasipo hiari yako, na kwa vile wengi wetu hatujui jinsi mfumo wa ubongo unavyofanya kazi basi hujikuta tukiwa matatizoni! 

Matokeo yake utajikuta ukianza kubadilika, kimatendo, kimienendo, kimtizamo na kitabia usijue kwanini imekuwa hivyo kumbe ni nguvu ya mazingira inafanya kazi!

Ukitaka kuthibitisha hili, jaribu kuangalia vile wewe mwenyewe huwa unabadilika kimienendo na kitabia pale inapotokea umebadilisha mazingira! 

Jaribu kuvuta picha vile huwa unabadilika kimienendo na kitabia pindi ukiwa; msikitini au kanisani au mahali palipo na hadhi fulani!

Bila shaka umejiona hivyo, na kama umefanya hivyo utakubaliana na mimi kwamba mambo mengi unayoyajua kukuhusu huenda siyo kweli ila mazingira ndiyo yamekufundisha hivyo!

Unatakiwa kujua kwamba hakuna mtu aliyeandika barua azaliwe kwenye mazingira aliyozaliwa, bali kila mtu alijikuta akiwa amezaliwa pale alipozaliwa pasipo hiari. Hii ni sawa na kusema umeweza kupokea athari zote hizo bila hata kujua. 

Ukiachilia mbali hilo hata sasa ubongo wako unaendelea kuchukua na kuchakata baadhi ya taarifa kutegemeana na hapo ulipo! Kwa kusema hivyo kumbe sisi sote ni matunda ya mazingira tunayotokea. 

Kwa maneno mengine twaweza kusema, tumekuwa hivi tulivyo kwa sababu ya kile tulichokipata kwenye mazingira tunayotokea, na pengine labda tungetokea kwenye mazingira mengine huenda tusingekuwa hivi tulivyo.

Na ndiyo maana ukimchukua papa ukamuweka kwenye chumba kidogo hawezi akakua na kuwa mkubwa zaidi ya chumba hicho, kwa sababu atajifunza awe na kimo sawasawa na chumba kinachomzunguka!

Hata hivyo ukimchukua papa huyohuyo ukamuweka baharini atakuwa mkubwa Zaidi kiasi cha kustaajabisha.

Hii ni kwa sababu mazingira ya Bahari hayajampa papa ukomo wa kujifunza, kwa kusema hivyo papa huyo atakuwa mkubwa kwa sababu mazingira yake yamempa mafunzo ya kutosha!

Rafiki, wewe siyo wa viwango hivyo bali mazingira yamekuweka uwe wa viwango hivyo, na hustahili kabisa kuwa wa viwango hivyo! 

Unatakiwa kujua kwamba umejifunza yasiyo na msaada, umejifunza yasiyofaa, umeona yasiyofaa, umejiona huwezi, umejiona hustahili na pengine umejiona wewe siyo kitu, kitu ambacho hakina ukweli wowote ule kuhusu wewe.

Rafiki, usiruhusu mazingira yakufafanue wewe ni nani kwa sababu wewe siyo mazingira bali u sehemu ya mazingira. 

Unatakiwa kujua kwamba mazingira yanakutegemea wewe uyabadilishe. Kwa kusema hivyo badala ya kulaumu kuhusu mazingira tumia busara na hekima zako kubadilisha mazingira yanayokuzunguka.

Unatakiwa utengeneze mazingira yako ya sasa ili kitendo kinachofuatia baadae kifanyike kwa urahisi. 

Ni kweli umejifunza mengi yasiyofaa lakini kuanzia sasa hutakiwi kuchukua kila jambo linalofanyika kwenye mazingira yanayokuzunguka kwa maana umeshaujua ukweli. 

Kumbuka umeumbwa ukiwa na akili na utashi, tafadhali tumia busara na hekima zako vizuri.

Ukiona huwezi kuyakabili mazingira uliyopo, basi hama mazingira hayo, kwa maana wewe siyo mti!

Ndiyo rafiki, wewe siyo mti kwamba ulipandwa umee hapo ulipo, uishi hapo ulipo, ufie hapo ulipo na uzikwe hapo ulipo!

Lahasha! Maadamu wewe siyo mti unaweza ukahama mazingira uliyopo ukaenda kwenye mazingira mengine ukajifunze kilichopo huko!

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!

Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentaship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673185329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...