Jinsi Ambavyo Walimu Wa uongo Hupelekea Watu Wajifunze Yasiyofaa...


Kitaaluma mimi ni mwalimu mtaalamu. Nikiwa kazini kuna wakati wanafunzi huwa wananiita mwalimu! Mwalimu! Nami huwa naitika kwa kusema; “mwalimu wa pekee na wa kweli alikuwa Yesu Kristo” 

Simaanishi kwamba walimu wengine hawafai lahasha! Tafadhali usinielewe vibaya, walimu wazuri wapo. Hata hivyo uzuri wa mwalimu unapimwa kupitia maarifa anayoyatoa kama yanajenga au yanabomoa. 

Endapo itatokea mwalimu akawa anatoa mafundisho yanayoharibu, kudidimiza na kubomoa badala ya kujenga basi mwalimu huyo hafai, bali anachokifanya ni uharibifu. 

Mwalimu huyu anastahili kupewa jina la mwalimu mharibifu na si jina la mwalimu mjenzi kwa sababu anachokifanya ni kuharibu akili za watu! 

Hawa ndiyo walimu tulionao karne hii, kwa sababu ukichunguza kwa ukaribu utagundua kwamba karibu kila sekta tumezungukwa na walimu, lakini ujinga bado ni mwingi kumbe tatizo siyo ujinga, bali tatizo ni walimu wenyewe kutokana na mafundisho wanayoyatoa!  

Mtu anapobaki kuwa mjinga ilihali anafundishwa ili ujinga umtoke maana yake anafundishwa ujinga! 

Na mtu anaweza akafundishwa ujinga na asijue kama kafundishwa ujinga, kwa sababu mjinga ni mtu ambaye hajui na hajui kama hajui.

Sasa kama umefundishwa na unaendelea kufanya yaliyo ya kijinga hii ina maana gani? Maana yake kilichoingia ndani ya fahamu zako ni ujinga ndiyo maana hata kile unachokifanya nje ya maisha yako ni cha kijinga! 

Ikumbukwe kanuni ya kinachoingia na kinachotoka inasema; "kile kinachoingia hupima kile kinachotoka".

Kwa kusema hivyo siye kila anayefundisha anafaa na siyo kila fundisho linalotolewa lazima likubaliwe, kuna watu wanafundisha watu mafundisho ambayo ni sumu. Ambapo sumu hiyo huenda kuua moja kwa moja ubongo wa yule anayeyapokea! 

Ni ukweli usiokuwa na kipingamizi kwamba hakuna mtu ambaye mwanafunzi humuamini Zaidi ya vile anavyomwamini mwalimu wake. 

Kwa kusema hivyo, kila kitu ambacho mwalimu wake atakisema mwanafunzi huyo atakichukua, na hapa haijalishi umri wa mwanafunzi huyo hata kama ni mtu mzima akifundishwa ujinga na mwalimu wake basi atauchukua ujinga huo na kuamini!

Hata kwenye dini kuna walimu wa uongo, watu ambao hawafundishi kweli ya Mungu badala yake sasa wanafundisha watu uongo  na upotofu na kuwafanya waamini wao wasiishi kiutu!

Kwa mfano kuna watu ambao wamewekwa kuwa Watoto wa madhabahu, ambapo wanafundishwa kuwa wanatakiwa wakae tu kwenye madhabahu ya Bwana, mpaka Mungu atakapowaamuru cha kufanya. 

Cha ajabu hakuna kinachoendelea, badala yake sasa wanapotezewa tu muda wao. Hii ni sawa na kusema watu hawa hubaki na hali dumavu na hushindwa kuchukua hatua maishani mwao kwa sababu ya aina ya mafunzo wanayoyapokea!

Ngoja nikuoneshe ajabu nyingine ya yale yanayoendelea kwenye dini zenu, kuna siku nilikuwa namsilikiza mwalimu mmoja hivi, alikuwa anafundisha kwenye chaneli moja maarufu sana hapa Tanzania, alinishangaza sana kwa upumbavu wa fundisho lake. 

Na kwa sababu chaneli ile ilikuwa maarufu sana, basi kupitia fundisho lake aliweza kuwapoteza watu wengi sana. 

Ubaya unakuja pale ambapo alikuwa ananukuu kutoka kwenye biblia! Nakumbuka aliweza kunukuu kutoka kwenye kitabu cha kumbukumbu la torati, kwa bahati mbaya sikumbuki kifungu…

Lakini katika maelezo yake alisema, nanukuu; “hakuna sehemu inayolindwa na Mungu kweye mwili wa mwanamke kama uke”. Nikashtuka Mungu huyu ninayemjua mimi ndiye anafanya kazi ya kulinda uke? 

Kwa sababu alikuwa amewaokota watu wake akaendelea kusema; “na Mungu huilinda sana sehemu hii kwa sababu ndiyo imebeba nyota, kwa kusema hivyo kila mwanaume hana budi kuhakikisha analala na wanawake wengi ili asafishe nyota yake”

Lakini kuna watu walilikubali fundisho hili la kipumbavu kwa sababu hawajui utu ni nini!

Swali linakuja aliyechafua nyota ya mwanaume ni nani? Na huo usafi wa nyota ya mwanamke unatokana na nini? 

Je, kwa fundisho hilo unahisi wanaume walio role model wake Suleimani waliondoka na picha gani?

Mnalalamika wanaume ni wasaliti kumbe walimu wenu wa mchongo mlionao ndiyo wanawafundisha wanaume wawe wasaliti!

Hata hivyo kwa mujibu wa tafiti binafsi moja ya eneno ambalo limevamiwa na walimu waharibifu ni eneo la mahusiano. 

Hapa kila mtu ana fundisho lake kiasi kwamba hata hao wanaofundishwa wenyewe wameishia kuchanganyikiwa tu.

Kuna walimu wanawafundisha wafuasi wao jinsi ya kuiba na kumteka mke wa mtu bila kukamatwa. 

Kuna walimu wanawafundisha wafuasi wao jinsi ya kumuiba mume wa mtu na kukaa naye kwenye mahusiano bila kukamatwa! 

Hata hivyo kuna walimu wanawafundisha wafuasi wao mbinu za kuishi na michepuka pasipo kukamatwa. 

Mbali na hilo kuna walimu wanafundisha wafuasi wao kuwa, tendo la ndoa ni maalumu kwa ajili ya starehe na ngono tu, kwa hiyo uwe umeoa au hujoa wewe fanya utakavyo, lakini hili likingaliwa kiutu haliko Sawa vilevile lipo kinyume kabisa na amri za Mungu!  

Walimu! Walimu! Walimu! Nimewaita mara tatu! Tafadhali mmepewa neema ya mafunuo ya baadhi ya mambo ambayo wafuasi wenu hawayajui! 

Tafadhali msitumie neema hiyo kuyatukuza yale yasiyo kiutu. Itumieni neema hiyo kwa ajili ya utukufu  Mungu! 

Kama kuna uovu fichua na kama kuna uozo kemea! Huu ndiyo wito mlioitiwa na siyo kuwapotosha watu wa Mungu kwa mafundisho ya uongo!

Najua kuna mwalimu wako unamuamini, leo jipe tathmini juu ya kile anachokufundisha kama kinakujenga kiutu au kinakuza ujinga kwenye fahamu zako!

Ukitaka mwalimu wa uhakika niko hapa, sijisifu ila najikubali na ninayakubali mafundisho yangu!

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!

Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentaship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...