Fahamu Ni Namna Gani Malezi Huwafanya Watu Wajifunze Vitu Visivyo Sahihi
Kila mtu aliyezaliwa na anaishi maana yake amelelewa, na hakuna mtu hata mmoja ambaye anaishi na hajawahi kulelewa!
Ukweli ni kwamba eneo la malezi ni eneo la kwanza kabisa katika kumtengeneza mtoto kwa mara ya kwanza, mara baada ya mtoto huyo kuzaliwa na kuanza kuishi.
Hata hivyo kwa mujibu wa tafiti za kisaikolojia zimeonesha kuwa, mtoto akishafikisha umri wa miaka mitatu ubongo wake hugawanyika katika sehemu mbili, baada ya hapo mtoto huyo huanza kujifunza na kuanza kuhifadhi kumbukumbu.
Kwa mantiki hiyo, inapotokea mtoto anafikia kipindi hiki wazazi wanashauriwa kuwa makini, kwa maana ni katika kipindi hiki ndipo mtoto huyo huanza kujifunza vitu vipya!
Unatakiwa kujua kwamba kitendo cha kuchukua taarifa hizo hufanyika pasi na hiari ya mtoto, kwa kusema hivyo chochote kile ambacho mtoto huyo atakiona, ataambiwa, atafanyiwa au atakutana nacho kitamfanya awe mtu wa aina Fulani.
Na ndiyo maana kisaikolojia inaaaminika kuwa; kile ambacho mtoto hukutana nacho wakati wa utotoni mwake ndicho humfanya abaki hivyo hadi utu uzima wake!
Mbali na hilo sote tunafahamu fika kabisa kuwa, hakuna mtu ambaye huzaliwa akiwa anajua, na hii ni kwa mujibu wa nadharia ya blank slate (tabula rasa)
Mbali na kuwa mtoto huyo huzaliwa akiwa hajui, hiki siyo kigezo cha kumfanya aisijifunze kwa sababu ataanza kuiga kile ambacho wazazi/walezi na ndugu ambao wanamzunguka wanakifanya!
Na endapo hao watu watakuwa wanafanya mambo yasiyofaa basi mtoto huyo atajifunza mambo hayo na kuhalalisha kuwa ni halali kwake kuyafanya!
Mbaya Zaidi ni kwamba ubongo wake hufanya kazi pasipo kuuamuru, hii ni sawa kusema kuwa, kila kitu kitakachosemwa au kitakachomzunguka mtoto huyo kitachukuliwa na kuingizwa moja kwa moja kwenye ubongo wake.
Matokeo yake, mtoto huyo hujikuta akiiga na kufanya kila kitu sawa sawa na vile kinavyofanywa na wazazi wake.
Hivyo basi endapo itatokea watu wanaomzunguka mtoto huyo, watakuwa na mtindo mbovu wa kuishi, mtoto huyo hujifunza na kuanza kuishi kama wao kwa sababu ni vitu anavoviiga moja kwa moja kutoka kwao!
Sambamba na hilo hata: kauli, maneno, vitendo na mambo yote ambayo mtoto hufanyiwa huchukuliwa na huaminiwa kuwa ni kweli na kisha huingizwa kwenye ubongo wake na kumtengenezea mtizamo Fulani hivi kumhusu.
Hivyo basi endapo ataambiwa kuwa: yeye ni mpumbavu, mjinga, maskini, hana akili, hajielewi, hatofika popote pale, hana uwezo, hawezi, ni kilema, chizi na maneno mengine mabaya ambayo mtoto huambiwa.
Basi mtoto huyo atakua huku akiwa amejifunza vitu visivyo sahihi, matokeo yake hujikuta akiharibika maishani mwake.
Ukweli ni kwamba kuna baadhi ya watu wamekuwa ni wavivu kupindukia kwa sababu ni kitu walichojifunza kutoka kwa wazazi wao walipokuwa watoto.
Mbali na hilo kuna Watu wamekuwa walevi na Malaya wa kupindukia kwa sababu ni kitu walichojifunza kutoka kwa wazazi wao.
Vilevile kuna watu wamekuwa wagomvi, wambeya wachonganishi kwa sababu ni vitu walivyojifunza kutoka kwa wazazi wao.
Pia kuna watu wamekuwa maskini kwa sababu wanafanya tabia za kimaskini walizojifunza kutoka kwa wazazi wao.
Kadhalika kuna watu wanawanyanyasa wake zao, Watoto wao na familia zao kwa sababu ni vitu walivyojifunza kutoka kwa wazazi wao.
Kuna watu hawajishughulishi na kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili kwa sababu ni kitu walichojifunza kutoka kwa wazazi wao.
Kuna Watu wanakaa tu huku wakiwa hawafanyo chochote kile, wakitegemea mambo yatokee kwa sababu ni tabia walizojifunza kutoka kwa wazazi wao!
Kama ulishawahi kusikia usemi usemao; "kama baba kama mtoto" au "kama mama kama mtoto".
Hii ndiyo maana halisi sasa, kwamba mtoto wa kiume atajifunza na kuchukua tabia za baba, vivyo hivyo na mtoto wa kike atajifunza na kuchukua tabia za mama!
Rafiki, unatakiwa kujua kwamba wengi wetu tumekuwa hivi tulivyo kwa sababu ni matunda ya vile tulivyolelewa.
Huenda umejifunza kuwa huwezi, hustahili na huwezi ukaishi maisha ya hadhi fulani!
Na huenda kupitia hayo umejikuta ukijidunisha na kujidharau, nipo hapa kukuambia kuwa hayo yote siyo kweli kuhusu wewe, bali umejifunza vitu visivyo sahihi. Futa hayo yote baada ya hapo uanze upya!
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!
Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentaship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 444384329/0673184429 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment