Je, Unataka Kujua Maeneo Ya Uwezo Ambao Kila Binadamu Huzaliwa Nao Ili Uliishi Kusudi lako? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...

Ni matumaini yangu u mzima wa afya na unaendelea vyema kabisa...

Karibu kwenye mwendelezo wa somo letu, na kwa siku ya leo tunaenda kumalizia maeneo kumi ya uwezo ambao kila mwanadamu huzaliwa nao na jinsi ya kutumia uwezo huo katika kuliishi kusudi la maisha yako! 

4. Uwezo Wa Kuhesabu: Huu ni uwezo wa kuweza kusoma namba kwa haraka na kujua kile namba zinamaanisha. 

Mbali na hilo eneo hili linahusu uwezo wa kujua na kucheza na namba katika maeneo manne yaani: kujumlisha, kutoa, kugawanya pamoja na kuzidisha! 

Unachopaswa kufahamu ni kwamba siyo kila mtu ni bora katika uwezo huu. Ukweli ni kwamba, kama humiliki uwezo huu ni ngumu sana kufanya vizuri kwenye hesabu. 

Watu wanaomiliki uwezo huu wanaweza kuwa: wahasibu,  madaktari, watafiti, waandishi, wanasheria, wataalamu wa kompyuta, n.k

5. Uwezo Wa Uchoraji: Hawa ni wataalamu katika kuona matukio fulani na kisha kwenda kuyatengenezea picha kwa kuyachora na kuyawasilisha kupitia michoro mbalimbali. 

Wana uwezo mzuri sana wa kuchora picha zinazopendeza na kuvutia!

Watu wanaomiliki uwezo huu, wanaweza kuwa: wabunifu wa mavazi, wauzaji wa nguo, wachoraji, wauzaji wa bidhaa za urembo, wasanifu wa majengo, wapambaji, warembaji wa ndani, wapaka rangi, waongoza filamu, n.k

6. Uwezo Wa Kujijua Kiundani: Hawa ni wazuri katika kujijua wao wenyewe kiundani, hii ni sawa na kusema watu hawa wanatambua vyema utu wao na thamani yao. 

Hata hivyo watu hawa ni wazuri sana katika kuujua vyema udhaifu na uwezo wao.

Ukiachilia hilo watu hawa mara nyingi wapo kivyao vyao na wako bize na mambo yao. Mara nyingi siyo waongeaji sana na wanapenda kujifunza kivyao vyao hata kama wangesaidiwa kirahisi na mtu mwingine kirahisi.

Watu wanaomliki uwezo huu wanaweza kuwa:wanasaikolojia, wahubiri, watoa huduma ya ushauri, wajasiriamali, wanafalsafa, waandishi, n.k

7. Uwezo Wa Ujasiriamali: Huu ni uwezo wa kuwahi kuliona soko na kisha kuandaa rasilimali pamoja na bidhaa utakazouza. 

Unatakiwa kujua kwamba kuna watu huwa wanaishi leo, lakini wako mbele kimiaka na huenda labda wametutangulia mbele kwa miaka kumi hivi!

Watu hawa huona soko litakuwaje na kuandaa bidhaa zitakazohitajika miaka ya huko mbeleni.

Huu ndiyo uwezo unaongoza zaidi kulipa duniani kuliko uwezo wowote ule. Hata hivyo mabilionea wakubwa duniani kama vile: Elon musk, Michael Dell, bilgates, Michael Zuckerberg wametumia uwezo huu!

Unatakiwa kujua kwamba saa hii kuna mtu anaumiza kichwa huko juu ya dunia ya mwaka 2050 huko.

8. Uwezo Wa Ushawishi: Huu ni uwezo wa kushawishi, kuwasiliana, kusihi, kutuliza migogoro pamoja na kuunganisha watu. 

Kuna watu ambao wao wana uwezo mkubwa sana wa kushawishi watu na popote wanapopata kupita huwa wanakubalika sana kutokana na ushawishi wao.

Watu wanaomiliki uwezo huu wanaweza kuwa: wanadiplomasia, viongozi, maafisa ustawi wa jamii, wahudumu kwa wateja, watu wa mauzo, washauri, madalali, walimu wa Watoto, wanasiasa wazuri, n.k

9. Uwezo Wa Kiudadisi: Huu ni ule uwezo wa kujua vitu pasipo kujifunza. Yaani hapa mtu unakuwa una uwezo mkubwa sana wa kudadidisi mambo na kuja na majibu mbalimbali juu ya masuala hayo.

Mbali na hilo uwezo huu humsaidia binadamu kujua mema na mabaya. 

Hata hivyo uwezo huu humsaidia mtu kuwajua watu vizuri pamoja na kuja na majibu kuhusu kwanini watu hao wako hivyo…

Kadhalika, uwezo huu ndiyo huwasaidia sana wanasaikolojia ambao wanaweza kumtambua mtu kwa muda mfupi yaani kuanzia tabia zake mpaka utambulisho wake kwa ujumla.

Watu wanaomiliki uwezo huu wanaweza kuwa: wanafalsafa wazuri, walimu wazuri, washauri, waandishi, wanasaikolojia, n.k

10. Uwezo Wa Kimaono: Huu ni uwezo unaopatikana kupitia maono. Hapa mtu anakuwa anaona jambo fulani lijalo huko mbeleni kupitia maono. 

Hii ni sawa na kusema hata baadhi ya watumishi wa Mungu wanamiliki uwezo huu. Tafadhali usinielewe vibaya nasisitiza tena kuwa (siyo wote)!

Watu hawa wanaweza wakaona jambo fulani kupitia maono halafu jambo hilo likaja kutokea kama lilivyoonwa!

Unatakiwa kujua kwamba vitu vingi hapa duniani huanza kutokea katika ulimwengu wa roho ndipo sasa hudhihirika katika ulimwengu wa kawaida.

Pia, Unatakiwa kujua kwamba karibu kila kinachotokea duniani huanza kama maono kwanza, ndipo sasa huja kutokea kama kitu halisi!

Hii inamaanisha hata wale watabiri wa masuala mbalimbali hutumia uwezo huu. 

Habari njema ni kwamba hata wewe unamiliki uwezo, ndiyo maana unaweza ukaona baadhi ya matukio yajayo kwenye maisha yako na yakaja yakatokea kama ulivyoyaonaa…

Watu wanaomiliki uwezo huu wanaweza kuwa: manabii, watabiri wazuri, waandishi, wahubiri, n.k

Rafiki, hii ni rai yangu kwako tumia muda wako mwingi ujue uwezo wako kwanza, endapo utashindwa kugundua uwezo wako, sehemu ya iliyobaki ya somo hili haitakuwa na msaada kwako, kwa maana ni mwendelezo wa kipi unatakiwa ufanye ili uweze kutumia uwezo wako kutengeneza fedha!

Kwa msaada Zaidi kuhusu kugundua maeneo kumi ya uwezo ambayo kila mwanadamu huzaliwa nayo nakushauri utafute PDF yangu iitwayo; “Mgodi Wenye Hazina Ndani Yake, Uliokosa Wachimbaji". Nina hakika itakusaidia sana! 

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri.

Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho.

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e;  Founder Wa King Mentaship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...