Jinsi Ambayo Shauku Ya Kuwa Na Maisha Mazuri Hupelekea Watu Wajifunze Vitu Visivyo Sahihi i...

Hivi unafahamu kwamba asilimia kubwa ya watu duniani kote wana shauku ya kuwa na maisha mazuri yaliyojaa furaha, amani, mafanikio na utele?

Ukweli ni kwamba mbali na kuwa watu wengi wana mitizamo hasi kuhusu maisha yao na kesho zao, lakini hakuna mtu hata mmoja ambaye huwa yupo tayari kutokuwa na maisha mazuri. 

Kwa mujibu wa tafiti Binafsi nilizobaini mara baada ya kufanya matembezi sehemu tofauti tofauti duniani, basi kila nilipopita niliwaona watu wakiwa bize sana huku wakifanya mambo mbalimbali wakilenga kutimiza Shauku zao za kuwa na maisha mazuri!

Hii ni sawa na kusema chini ya mwamvuli wa kuwa na maisha mazuri kuna watu wamejifunza kufanya kila linalowezekana hata kama halifai, kwa madai ya kutimiza shauku zao...

Unaweza ukawa unajiuliza kufanya kila linalowezekana maana yake nini? Unatakiwa kujua kwamba, watu hawa wamejifunza kufanya mambo hata yasiyo ya kiutu, ili tu kutimiza shauku yao ya kuwa na maisha mazuri!

Ngoja twende kwa mifano dhahiri upate kuujua uhalisia wa hoja inayojengwa hapa:-

Chini ya mwamvuli wa kuwa na maisha mazuri, kuna watu wamejifunza kutapeli watu na kuibia watu kwa kutumia teknolojia na ujuzi wa kiwango cha hali ya juu. 

Ni kweli wanafanya hivyo na hawakamatwi na ndoto yao ya kufikia maisha mazuri inafikiwa japo kwa kufanya yasiyo ya haki. Watu hawa wanatakiwa kujua kwamba, "anayekula cha mwenzake na chake huliwa pia".

Mbali na hilo chini ya mwamvuli wa kuwa na maisha mazuri, kuna watu wamejifunza jinsi ya kufanya biashara haramu, kwa mfano uuzaji wa madawa ya kulevya, usafirishaji haramu wa binadamu, uuzaji wa viungo vya binadamu hali ambayo hupelekea mauaji ya jamaa ndugu na rafiki ili viungo vyao vichomelewe na Kwenda kuuzwa. 

Unatakiwa kujua kwamba kuna watu wamejifunza haya yote na wanafanya haya yote na huenda wakawa hawakamatwi na pengine labda kupitia kufanya haya yote wamefanikiwa kuwa na maisha mazuri. 

Lakini jambo hili likiangaliwa kiutu siyo sahihi, huu ni unyama kabisa, kwa maana siyo vema kuharibu au kuhatarisha uhai wa mtu ili uwe na maisha mazuri, ilihali hata huyo unayemfamyia hivyo anasatahili na ana ndoto za kuwa na maisha mazuri kama wewe!

Hata hivyo chini ya tamaa ya kuwa na maisha mazuri kuna wanaume wamejifunza kuwa mashoga na wanafanya ushoga, ili wafanikiwe kifedha, na huenda wamefanikiwa kuzimilki hizo fedha na mali nyingine nyingi, kama vile; nyumba na gari, wakasahau kuwa utu wao ni muhimu zaidi kuliko hata hizo Mali!

Amelaaniwa mtu yule abadilishaye matumizi asili ya mwili wake...

Vilevile chini ya mwamvuli wa kuwa na maisha mazuri, kuna watu wenye mamlaka fulani fulani hivi kwenye sekta za umma au sekta binafsi, ambao wamejifunza jinsi ya kuwaibia walio chini yao kwa ulaghai wa madaraka yao pamoja na kutumia mbinu za kisayansi na kiteknolokia.

Ni kweli wanafanya hivyo na hawakamatwi na wanafanikiwa kuwa na maisha mazuri sawa, huku wakiwatesa wale walio chini yao! Watu hawa wanatakiwa kujua kwamba kila mtu atalipwa sawa sawa na matendo yake.

Hata hivyo chini ya mwamvuli wa kuwa na maisha mazuri kuna watu wamejifunza kufanya biashara za ngono na ndiyo maana sasa hivi ngono imekuwa ikishangaliwa sana na watu wanauza na kununua.

Ukweli ni kwamba, ukienda karibu kila kona ya mtaa utakutana na makahaba, wadangaji na wengine wengi wafanyao kila aina ya machukizo wamejiweka tayari kwa kufanya biashara zao haramu!

Haya yote ni mambo ambayo yapo na watu wanayafanya tena kwa ustadi mkubwa sana, kwa sababu wamejifunza jinsi ya kufanya biashara hizo za kuuza utu wao kwa thamani ndogo!

Swali linakuja; kama kila mtu kaumbwa na karama, kipaji au uwezo Fulani ambao endapo angeutumia, angaweza kutengenenza fedha za kutosha na kuishi maisha mazuri, je, ni kwamba hawa wanawake wana kipaji na karama ya kutumikia ngono hapa duniani?

Na kama jibu ni Hapana kwanini wafanye hivyo? Lakini na ninyi wanaume huwa mnazidi sana, ama hakika sijivunii kabisa kuwa mwana! Yaani unatumia hela zako ulizotafuta kwa shida kununua: shida,  matatizo, balaa, UTI SUGU, nuksi na laana?

Poleni sana Ndugu wanaume, hawa watu huwa wanapata soko kwa ajili ya uhitaji wenu, siku mtakapoacha kuwanunua ndipo watakosa soko na huo ndiyo utakuwa mwisho wa biashara zao! 

Amini nawaambieni, siku inakuja, tena imefika, nitakapoitisha kikao na wanaume wenzangu, niaminini mimi, tukishamaliza hiko kikao hakutakuwa na kununua tena wanawake wanaojiuza... hahahaha 😂😂😂

Hata hivyo chini ya mwamvuli wa kuwa na maisha mazuri kuna watu wamejifunza ushetani wa kulala na mama zao wa kuwazaa, kulala na Watoto wao wa kuwazaa, kulala na ndugu zao wa damu, ikiwa ni kama sharti la kufanikiwa na kuwa na maisha mazuri. Je hili nalo ni uzushi, kama mimi ni mzushi niko hapa mje mnipige!

Kadhalika chini ya mwamvuli wa kuwa na maisha na mazuri kuna watu wanalala na viumbe vya ajabu, kama vile nyoka, majini na vingine vingi kwa madai ya kufanikiwa kifedha!

Hebu vuta picha vile kuna watu wanaishi kwa shida chini ya mwamvuli wa kuwa na maisha mazuri! Yaani unakosa uhuru wa kuishi kiutu hapa duniani kisa uwe na maisha mazuri?

Ni kweli una shauku ya kuwa na maisha mazuri, hata mimi pia ninayo, lakini lazima ujiulize ni kipi unafanya ili uwe na maisha mazuri! 

Rafiki, shauku yako ya kuwa na maisha mazuri isikufanye uache yaliyo ya kiutu, ukawa kikwazo kwa watu wengine!
 
Unatakiwa ujifunze kuwa daraja na siyo kuwa kikwazo kwa wengine, kufanikiwa huku ukiacha maumivu kwa ndugu zako haina maana yoyote ile...

Na ndiyo maana katika kitabu cha Matthayo 7:12 neno la Mungu linasema; "Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii".

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!

Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho.

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentaship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...