Kama Umechoka Kujifunza Vitu Visivyo Na Msaada Maishani Mwako Unatakiwa Ufanye Uamuzi Huu...
Kila matokeo yoyote yale yaliyo ya maana ambayo mwanadamu huyapata hutegemeana sana na aina ya maamuzi aliyoyafanya!
Na ifahamike kwamba kila mtu ni matokeo ya maamuzi aliyowahi kuyafanya huko nyuma aidha kwa kutaka ama kutokutaka au kwa kujua ama kutokujua!
Kwa mantiki hiyo, hata wewe umekuwa hivyo ulivyo na umefika hapo ulipo kutokana na aina ya maamuzi uliyowahi kuyafanya!
Kwa kusema hivyo ili uweze kujifunza vitu sahihi huna budi kufanya aina ya maamuzi ambayo hujawahi kuyafanya kabisa hapo awali.
Kumbuka moja ya dalili ya uwendazimu ni ile hali ya kuendelea kufanya kitu kilekile na kwa namna ileile huku ukitegemea matokeo ya tofauti!
Na hauwezi ukatatua tatizo kwa kutumia njia ileile iliyopelekea kutokea kwa tatizo hilo, kwa kusema hivyo unatakiwa uende mbele zaidi!
Hata hivyo unatakiwa kujua kwamba ili upate matokeo ambayo hujawahi kuyapata, ni lazima ukubali uwe mtu ambaye hujawahi kuwa pamoja na kufanya kitu ambacho hujawahi kukifanya.
Rafiki, unatakiwa kujua umefika hapo ulipo na kuwa hivyo ulivyo kutokana na kile ulichojifunza.
Na hii ni kwa sababu kile kilichoingia kama mafunzo kimepima kile kilichotoka, na hayo ndiyo matokeo mbalimbali maishani mwako pamoja na hapo ulipofika!
Na ndiyo maana kanuni ya kinachotoka na kuingia inasema kuwa; “kinachoingia hupima kile kinachotoka”.
Kwa kusema hivyo ili uweze kupata matokeo mapya ni lazima uweze kuingiza kitu kipya kitakacholeta matokeo hayo. Na hiki ndicho makala hii inahususu!
Kwa ujumla ili ujifunze vitu vipya pamoja na kubadili matokeo na hali mbalimbali maishani mwako huna budi ufanye yafuatayo:-
1. Futa Masuala Yote Uliyojifunza Ambayo Hayakusaidii...
Bila shaka ushawahi kutumia memori kadi na ikajaa kiasi kwamba ikawa haina uwezo wa kutunza faili lingine lolote lile.
Je, ni nini ulifanya ili memori kadi hiyo iweze kupokea na kutunza faili jipya?
Bila shaka uliifomati ee… …Ndiyo utakuwa uliifomati kwa kufuta kila kitu na kuifanya iwe kama mpya vile…
Vivyo hivyo ndivyo unavyotakiwa ufanye kwenye ubongo wako kwa kufuta kila kitu na kuanza upya huku ukiwa mpya kabisa, sawasawa na vile ulivyokuwa siku uliyokuja hapa duniani!
Unatakiwa kujua kwamba hukuzaliwa ukiwa na uelewa ulionao sasa! Na umekuwa hivyo ulivyo kutokana na kuingiza taarifa zisizo sahihi, kuamini yasiyofaa, pamoja na kuona yasiyofaa na kupitia kwa hayo ukafanyiwa uharibifu!
Hivyo basi unachopaswa kufanya kwenye hatua hii ni kusafisha ubongo wako, kwa kusafisha takataka zote zilizojaa kwenye ubongo wako. Bila shaka unakumbuka vizuri nadharia ya blank slate yaani tabura lasa...
Unachopaswa katika hatua hii ni kuirudia ile hali ya utabura lasa na kuanza upya kama mtoto mchanga aliyezaliwa sasa...
Rafiki, hakikisha unasitisha uhusiano na vyanzo vyote vinavyoangaza mafunzo yoyote yale yasiyo na msaada, baada ya hapo sasa unatakiwa ufute mafaili yote yaliyomo kichwani mwako ambayo yameonekana kutokukusaidia!
Kitu kingine cha kuongezea hapa katika hatua hii, hakikisha kuwa haunywi maji machafu tena, ukauchafua ubongo wako, kwa kusema hivyo huna budi kuanza kuchuja taarifa unazokutana nazo kutoka vyanzo mbalimbali vinavyoangaza maarifa kabla hazijaingia ubongoni mwako!
Rafiki unatakiwa ufute mafundisho yote uliyojifunza haijalishi ulijifunza wapi na katika ngazi gani na kwa kiwango kipi, maadamu hayajakusaidia huna budi uyafute.
Hata hivyo unatakiwa ufute kila kitu ambacho jamii yako imekufunza haijalishi ni kipi maadamu hakijakusaidia huna budi kukifuta.
Vilevile unatakiwa ufute yale yote uliyojifunza kutoka kwa walimu mbalimbali na watu wote wenye ushawishi, maadamu hayajakusaidia huna budi uyafute.
Pia unatakiwa unatakiwa ufute mambo yote uliyojifunza kutoka kwa rafiki zako ambayo hayajaonekana kuwa na msaada kwako, maadamu hayajakusaidia huna budi kuyafuta!
Kwa ujumla unatakiwa uruhusu kila kitu kiende, kwa kusahau kila kitu kuhusu wewe zamani.
Baada ya hapo ndipo unatakiwa uanze upya ukiwa mpya kiakili na kimitizamo.
Rafiki, huenda ulienda mpaka mia, usiogope kurudi na kuanza tena kwenye moja ambayo ina uhakika wa kukufikisha mbali Zaidi.
Endapo utaweza kufuta kila kitu bila shaka utapoteza mpaka utambulisho wako, kwa hiyo basi unapopoteza utambulisho wako maana yake utashindwa kujijua wewe ni nani...
Ukishindwa kujijua wewe ni nani kama matokeo ya kufuta Utambulisho bandia uliokuwa nao, ndipo sasa utakaribishwa kwenye hatua ya pili ambayo itakusaidia kugundua kile kilicholala ndani yako!
Na hatua hii itaendelea kwenye somo lijalo...
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!
Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho...
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentaship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment