Kama Unataka Kugundua Soko Linalohitaji Huduma/Bidhaa Inayotokana Na Kuusihi Uwezo Wako Soma Hii...
Kila uwezo fulani alionao mtu, basi nyuma yake kuna soko kubwa sana linalouhitaji uwezo huo ili lirahisishiwe maisha pamoja na mahitaji yao.
Na huenda mtu huyo asipouishi uwezo huo, hilo soko linalotegemea uwezo wake linaweza kuishia kuishi kwa taabu na mateso mengi, kwa sababu Yule anayepaswa kuja na ufumbuzi wa kuondoa adha hizo hajaanza bado.
Pia kugundua uwezo na kuanza kuuishi pasipo kujua ni aina gani ya watu watakaonufaika na uwezo wako hiyo nayo ni kazi bure.
Na endapo utaanza kuuishi uwezo wako pasipo kujua ni watu gani wanaohitaji uwezo wako unaweza ukaishia kujifurahisha mwenyewe.
Na ifahamike kwamba, huo uwezo siyo kwa ajili yako bali ni kwa ajili ya watu wengine kwa maana tunaishi kwa ajili ya watu wengine.
Hata hivyo unatakiwa kujua kwamba siyo watu wote watahitaji uwezo wako, kwa sababu uwezo wako siyo kwa ajili ya kila mtu bali ni kwa ajili ya kundi Fulani hivi la watu mahususi.
Hivyo basi kuwagundua watu hao ni jambo la msingi sana kwa maana ni hao tu ndiyo watakaohitaji uwezo wako!
Kwanini unatakiwa ugundue watu wanaokuhitaji? Ni kwa sababu ni kupitia hao tu ndipo kusudi lako na uwezo wako utakamilishwa.
Kwa hiyo kugundua watu hawa ni muhimu kwa sababu huwezi ukakubalika na kila mtu, unatakiwa kujua kwamba kuna watu wengine hawatahitaji kabisa chochote kile kutoka kwako.
Hivyo basi ili kuepuka maumivu ya kuona kama unafanya juhudi sana na unapambana sana lakini huoni matokeo, unatakiwa kubaini ni kundi gani linalotakiwa lije linufaike na uwezo wako.
Kugundua soko lako lilipo kunahusisha vitu kama vile: kubainisha aina ya wateja unaowahudumia kwa mfano; Jinsia yao ni ipi, umri wao ni upi, hadhi ya maisha yao ni ipi, kiwango chao cha elimu, wanapatikana wapi pamoja na hali yao kiuchumi ipoje.
Unatakiwa kujua kwamba kila mteja ana aina Fulani ya bidhaa au huduma anayoihitaji na ndiyo maana kumjua mteja wako ni nani ni jambo la msingi sana!
Usipojua hili unaweza ukashangaa unamuandalia mlokole pombe wakati yeye na pombe ni mashariki na magharibi.
Ukweli ni kwamba kuna huduma/bidhaa zinazowafaa matajiri, kuna huduma/bidhaa zinazowafaa watu wa kati na kuna huduma/bidhaa zinazowafaa maskini.
Kwa kusema hivyo ni muhimu ukagundua hadhi ya mteja wako ili uandae huduma inayoendana naye.
Kwa mfano huwezi ukamuuzia maskini bidhaa ya matajiri, kwa sababu hataweza kuimudu gharama na ndiyo maana kulijua soko lako ni jambo la msingi sana!
Ndugu siyo kila mtu anahitaji kipaji chako au uwezo wako, kwa hiyo kugundua uwezo wako siyo kigezo cha kufanikiwa katika kutoa huduma nzuri itakayokufanya utengeneze fedha, bali ni lazima uandae orodha ya watu watakaonufaika na uwezo wako.
Kumbuka mtandao wa watu ulionao ndiyo unapima utajiri wako. Hii ni sawa na kusema kuwa watu unaowajua na hao wanaokujua ndiyo hao hao watakaoweza kutumia huduma yako ukiweza kuwatambua vizuri kuwa ni wepi.
Kwa kusema hivyo ukubwa wa soko utakalokuwa nalo ndilo litapima kiwango cha fedha utakachotengeneza kupitia huduma utakayokuwa unatoa!
Kwa mantiki hiyo kila siku huna budi kuhakikisha unajenga mtandao mpya wa watu, ili kupitia hao uweze kutambua ni wapi wanastahili kupata huduma yako na wapi hawastahili.
Rafiki ili ufanikiwe unahitaji watu, na uwezo wako siyo kwa ajili yako bali ni kwa ajili ya watu wengine.
Na ndiyo maana hata mti hauwezi ukayala matunda yake wenyewe.
Hivyo basi ni muhimu sana kuhakikisha kuwa unawajua hao watu wanaohitaji uwezo wako kwa maana ndiyo hao watakaofanikisha safari ya mafanikio yako!
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!
Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentaship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 Au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment