Kama Unataka Kujua Ni Kipi Unapaswa Ufanye Mara Baada Ya Kugundua Uwezo Wako Soma Hii...
Watu wengi wanaujua vyema uwezo wao lakini hawajui jinsi gani wanaweza wakatumia uwezo huo ili uwanufaishe!
Kujua uwezo wako ni kitu kingine na kutumia uwezo wako ili ukunufaishe ni kitu kingine vilevile!
Ukweli ni kwamba, ukishagundua uwezo wako jambo la kwanza unalopaswa kufanya ni kuandaa huduma au bidhaa Inayotokana na uwezo huo!
Unatakiwa kujua kwamba, moja ya eneo ambalo fedha nyingi imejificha ni eneo la bidhaa au huduma.
Kwa kusema hivyo ni wale tu watakaokuwa wanatoa huduma Fulani au watakaokuwa wanauza bidhaa Fulani ndiyo watakaokuwa wanatengeneza fedha!
Wewe mwenyewe unaweza kufanya tathmini binafsi ni kwa namna gani umekuwa ukitumia fedha zako kwa ajili ya kupata huduma au bidhaa Fulani zinazozalishwa na kutengenezwa na watu wengine!
Na umetumia fedha zako ili kupata huduma au bidhaa Fulani kwa sababu kuna thamani Fulani ambazo zimebebwa kwenye bidhaa hizo au huduma hizo!
Kwa kusema hivyo hata wewe huna budi uandae bidhaa au huduma yenye thamani ndani yake inayotokana kuuishi uwezo wako, ambapo watu watakuwa wapo tayari kuilipia!
Kumbuka fedha hufuata thamani, hii ni sawa na kusema ile thamani utakayoitengeneza kupitia huduma yako au bidhaa yako ndiyo itasababisha fedha iweze kukufuata.
Unatakiwa kujua kwamba ukishagundua kipaji chako au uwezo uliozaliwa nao yafaa utengeneze huduma au bidhaa Fulani kupitia uwezo huo.
Kwa mfano kama umegundua kwamba una uwezo wa kushauri watu unaweza ukaanzisha huduma ya ushauri na kupitia kufanya hivyo ukawa unatengeneza fedha, mimi huwa natengeneza fedha kupitia hili!
Au kama umegudua kwamba una uwezo wa kuandika, unaweza ukaanza kuandika vitabu/makala mbalimbali ukawa unauza na kupitia kufanya hivyo ukatengeneza fedha, pia huwa natengeneza fedha kupitia kufanya hili.
Au kama umegundua kwamba una uwezo wa kujisimamia unaweza ukaanzisha huduma ya usimamizi ukawa unawasimamia watu katika maeneo kadha wa kadha, kupitia hivyo ukatengeneza fedha, huwa natengeneza fedha kupitia kutoa huduma ya usimamizi!
Ndiyo maana hata title yangu inaitwa King Mentaship Program, jina hili limetokana na huduma hii!
Au kama umegundua kwamba una uwezo wa kupika michanganyo yenye Ladha nzuri unaweza ukabuni mchanganyo Fulani ukaandaa pakeji yake ukawa unauza, kupitia hilo ukatengeneza fedha.
Rafiki hiyo ni mifano tu, unachopaswa kufanya ni kuangalia fursa zinazoendana na uwezo wako, baada ya hayo, andaa huduma au bidhaa nenda kauze. Kumbuka huwezi ukapata kitu pasipo kufanya chochote kile.
Hivyo basi ni lazima uandae huduma au bidhaa Fulani za kuuza ili utengeneze fedha hali itakayokufanya uweze kujikwamua kimaisha.
Na pasipo kufanya hivyo huwezi kutengeneza fedha!
Ndugu, fedha hufuata thamani, gundua uwezo wako, jiandae vya kutosha, tengeneza bidhaa au huduma halafu nenda kaiuze hapo ndipo utatengeneza fedha!
Kumbuka watu wengi hufanya mengi ili kutengeneza fedha, kwa mfano wengine huenda hadi shuleni wakakaa kwenye mfumo kwa muda mrefu wakitengenezwa waje waajiriwe ili walipwe, kwa kusema hivyo hata wewe huna budi utumie mbadala huu ili utengeneze fedha!
Kwa msaada zaidi au kwa ushauri zaidi usisite Kuwasiliana Nami inbox!
Je, unajua ni nini unatakiwa ufanye mara baada ya kuandaa huduma/bidha yako?
Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentaship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 Au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment