Fahamu Kuhusu Aina MBILI Za Wanaume Pamoja Na Utofauti Wa Mitizamo Yao Hasa Linapokuja Suala La Ngono...

Si haba endapo utakuwa uliona baadhi ya machapisho yaliyoanisha aina kadhaa za wanaume kwa kutumia vigezo fulani fulani hivi, na pengine labda hujawahi kukutana kabisa na hizi aina MBILI zitakazojadiliwa hapa!

Hilo si jambo la kushangaza, kwa sababu hata jambo linaloibuliwa hapa huenda halijawahi kuibuliwa, na endapo liliibuliwa huenda namna lilivyojadiliwa siyo sawa na litakavyojadiliwa hapa!

Na ifahamike kwamba, hapa ninaainisha aina MBILI za wanaume kwa kuangalia mitizamo iliyopo kati yao hususani katika eneo Zima la ngono! 

Kwa maana wengi wanaona kuwa; "ngono kwa mwanaume ni kila kitu na hakuna mwanaume anayetosheka na mwanamke mmoja"

Kwa kusema hivyo nitaenda kujadili hili kwa kutumia kigezo cha kiumbo na kigezo cha kiakili na ukomavu wa kihisia, ambapo tunapata aina kuu mbili za wanaume, ambazo ni:-

1.Wanaume-Wavulana: hii ni jamii ya wanaume ambao kiumbo wanaonekana ni wanaume, lakini kiakili na kihisia hawajakomaa. Mawazo ya wanaume hawa ni ya kitoto wala hayaoni lolote kuhusu kesho ijayo. 

Kwa ufupi endapo utachunguza matendo na Mawazo ya wanaume hawa hutaona tofauti iliyopo kati yao na wavulana.

Mara nyingi hutumia muda wao mwingi kufukuzia wanawake, kufanya ngono, kupiga stori zihusuzo mapenzi.

Kwa mfano utawasikia wakisema; "Mimi nisipofanya ngono kwa muda wa wiki MBILI huwa naanza kuumwa mgongo", "huwezi ukakaa miezi sita pasi na ngono labda uwe unapiga punyeto", "huwezi kuishi bila mwanamke"

Unatakiwa kujua kwamba kimawazo huwa wanajiona wako sawa, lakini kiuhalisia huwa hawapo sawa!

Hata hivyo wanaume wanaodondokea kundi hili, huthaminisha kuwa ujanja wa kuishi ni kulala na wanawake Wengi, vilevile wanaume hawa huona kuwa neno mafanikio kwao; "ni ile hali ya kuwa na wanawake wengi kwa wakati mmoja!"

Kutokana na hilo hujikuta wakigeuza ukweli wa maisha na kuhalalisha kuwa; Fahari yao kubwa ni wanawake na huwa wapo radhi kufanya kila jambo hata lisilo la kiutu ili wawanase wanawake. 

Kinachosikitisha zaidi kuhusu Wanaume hawa ni kwamba, huwa hawajui chochote kile kuhusu maisha yao yajayo na hawana mipango yoyote ile kuhusu kesho zao, lakini cha ajabu mipango yao mikubwa  hulenga Zaidi katika kuwanasa na kuwatumia wanawake…

Je, wewe ni mwanaume-mvulana? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo tafadhali soma makala hii mpaka mwisho!

2. Wanaume komavu: hii ni jamii ya wale wanaume ambao wamekomaa kiumbo, kiakili na kihisia. Wanajijua wao ni nani na wapo hapa dunia kwa kusudi gani. 

Wanaamini kwamba ili ufanikiwe katika maisha yako huhitaji wanawake wengi, bali unahitaji mwanamke mmoja tu utakayeanza naye safari ya maisha.

Hawana muda na ngono na wanawake kwa sababu wana malengo na ndoto kubwa wanazopambania. 

Kutokana na kukua kiumbo na kiakili pamoja na kihisia huamini kuwa mwanamke mmoja kati ya wengi anawatosha. 

Hii ndiyo aina ya wanaume unayopaswa uwe. Hata mimi mwandishi nipo kwenye hili kundi la wanaume, kwa hiyo kwangu mimi mwanamke mmoja ananitoshea na sina muda na wanawake wengine. 

Umeona? Sina maana kwamba hutakiwi kutofanya ngono hahasha! Lakini epuka ile ngono ya kutaka kulala na kila mwanamke! 

Hata hivyo, kuwa Mwanaume komavu haimaanishi kwamba hutakiwi kushiriki ngono lahasha! Vipi kama umeoa? Sipo hapa kumkataza mtu asifanye, ila nipo hapa kukueleza kuwa kabla hujafanya yafaa ufanye tafakari ya kina! Hasa ukihusisha na nini unatarajia mara baada ya kufanya tendo!

Je, wewe ni mwanaume-mvulana au mwanaume komavu? Mtu mwenyewe na ujipe tathmini. Bila shaka maelezo yaliyopo hapo juu yamekuweka kwenye kundi mojawapo.

Ukweli ni kwamba wewe ni kiongozi, unatakiwa kujua unayaongozaje maisha yako kwa kesho ijayo. Haupo hapa kuwa kamanda wa ngono na mapenzi. 

Usitumike kama chombo cha kuharibu maisha ya mwanamke, kwa maana kwa kiasi kikubwa wanaume mna mchango katika kuwaharibia wanawake maisha yao, mnawapa mimba halafu mnazikataa, mnawazalisha halafu mnawaacha, nafikiri huwa mnapata nguvu ya kufanya hivyo kwa sababu ninyi huwa hamshiki mimba.

Uanaume wako usifanye mtu ajutie, usitumie uanaume wako kumzalisha mwanamke na kumuacha ateseke na mtoto ambaye ni wa damu yako kabisa, kisa ngono ya saa moja. 

Ndugu mwanaume huo siyo wito ulioitiwa hapa duniani. Unatakiwa kuweka jambo hili akilini mwako; “hukuumbwa kuja kutumikia ngono hapa duniani”. Endapo itatokea Mawazo ya ngono yamekujia yakumbuke maneno hayo.

Bila shaka utakuwa unajiuliza mbali na kuwa wanaume wameumbwa huku wakiwa ni watu wakuu sana na wamebeba ukuu ndani yao, kwanini sasa huwa wanajishushia hadhi zao na heshima zao kwa kutumia sehemu kubwa ya maisha yao kuwaza ngono na kufanya ngono? 

Usijali jambo hili utaenda kuoneshwa kwenye sehemu itakayofuatia. 

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentaship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...