Hakuna Uhalisia Wowote Ule Kwenye Usemi Usemao; "Wengi Wape"
Hivi unafahamu kuwa kuna mambo mengi sana ambayo yanaaminika na kundi kubwa la watu duniani kote, ya kwamba mambo hayo ni kweli na ilipaswa yawe vile yalivyo, ilihali mambo hayo siyo kweli na wala hayapo hivyo ijapokuwa yanaaminika na wengi kuwa yapo hivyo?
Ukweli ni kwamba hapa duniani yapo mambo mengi sana ambayo yamepewa tafsiri fulani fulani hivi fananifu katika ulimwengu wote, kiasi kwamba yamekuwa ni ya kawaida na yamezoeleka kila mahali, na yanaaminika na wengi kuwa yapo hivyo ilihali hayapo hivyo!
Huenda hata wewe ukawa ni miongoni mwa watu ambao wameamini katika mambo yasiyo na ukweli na ambayo hayawezi kuthibitishwa, hali ambayo imekufunga kifikra na kiufahamu nawe ukajikuta ukishindwa kujinasua kwa sababu umenaswa mtegoni!
Rafiki, unatakiwa kujua kwamba hapa duniani hakuna kuteseka pasipo na sababu! Kwa kusema hivyo kwa kila teso unalopitia upate kujua kwamba kuna sababu inayopelekea teso hilo!
Hata hivyo busara imenifundisha kwamba sina budi kutumia sikio langu kuyajaribu maneno ninayosikia kama vile ambavyo kaakaa langu huwa linaonja chakula!
Na ndiyo maana mimi huwa siamini kila jambo, bali huwa natumia akili zangu katika kufanya uchanganuzi wa kina ili nipate kujua yaliyo kweli, na siyo kuamini na kulipokea kila jambo kama linavyosemwa na kuaminiwa na kila mtu kuwa ni kweli!
Ukweli ni kwamba, kwa muda mrefu nimekuwa ni mtu wa kutuliza kichwa changu ili kuutafuta ukweli kwa kufanya uchanganuzi wa kina uliohusisha akili zangu kuhusu mambo mbalimbali.
Matokeo yake nikabaini kuwa yapo mambo mengi sana yanayoaminika na wengi kuwa yapo hivi lakini siyo kweli kwa maana mambo hayo hayapo kama vile yanavyoaminika!
Na watu wengi wamejikuta wakiyapokea mambo hayo na kuyafanya ziwe falsafa zinazoongoza na kusimamia maisha yao pasipo kuyafanyia uchanganuzi, hali ambayo imewafanya wachukuliwe na kila upepo wa kiulimwengu, na MWISHO wao uwe ni mateso na taabu!
Mambo haya hufahamika kama "dogmas concepts". Mpenzi msomaji, upate kujua kwamba dogmas concepts ni orodha ya mambo yote ambayo kundi kubwa la watu/jamii fulani ya watu inayaamini kuwa kweli, wakati siyo kweli, na watu wengi huyapokea na kuyaishi eti kwa vile yanaaminika na wengi!
Na, endapo uchanganuzi yakinifu utafanyika kuhusu mambo hayo, ndipo sasa itabainika kuwa mambo hayo siyo kweli na hayana uthibitisho wowote ule ijapokuwa yanaaminika na wengi kuwa ni kweli!
Kwa mfano jamii ya Tanzania imeamini kuwa; "hakuna mwanaume anayetosheka na mwanamke mmoja" ... Nitajadili hili kwa kina huko mbeleni hii ni kwa mfano tu...
Na endapo utakuwa ni yule mtu unayeamini kila jambo pasi na kufanya uchanganuzi wa kina kwa kutumia akili zako ulizopewa, nipo hapa kukufahamisha kuwa utapitia magumu mengi sana!
Yapo mambo mengi sana ambayo yameaminishwa kuwa yapo hivi ama vile na wengi wanayaishi pasipo hata kudadisi ukweli wa madai hayo!
Unatakiwa kujua kwamba kuna watu huwaaminisha watu baadhi ya mambo ili wao wapate manufaa kupitia hayo!
Kitendo hiki hufahamika kama "hetero suggestion". Unatakiwa kujua kwamba, hetero suggestion ni pendekezo la nguvu ambalo hutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine, na huyo mtu anayeambiwa akillikubali pendekezo hilo basi huliruhusu liongoze maisha yake, ambapo mwisho wake unaweza kuwa ni mateso tu...
Na mara zote pendekezo hilo huwa lipo pale ili kumnufaisha yule aliyelitoa na siyo yule aliyelipokea!
Kumbe usipokuwa makini unaweza ukajikuta ukiamini kila jambo ambalo linasemwa na kuaminiwa na kila mtu, matokeo yake imani yako kuhusu jambo hilo ikaishia kugharimu maisha yako yote...
Mnamo mwezi mei 2024 niliandika KITABU kinachoangaza ukweli halisi unaomhusu mwanaume dhidi ya ile imani inayoaaminika ulimwenguni kote kuwa; "starahe kubwa ya mwanaume ni ngono na fahari yake kubwa wanawake"
Ndani yake nimejadili mengi na kuonesha kuwa imani hii iliyopo dhidi ya wanaume haina ukweli wowote ule, kwa maana fahari ya mwanaume siyo ngono tu.
Lakini kutokana na uwepo wa imani hii wanaume wa leo hii wameliamini dai hilo na wanaishi nalo!
Hata hivyo endapo utachunguza jambo hili kwa undani utakuja kugundua kuwa imani hii imetengenezwa ili imfanye mwanaume asiweze kutumia akili zake katika kufanya uvumbuzi, ugunduzi na maendeleo bali atumie akili zake katika kuwanasa wanawake ili alale nao, awape mimba, azikatae, zikatolewe au zisipotolewa tuwapate single mothers afu tuwacheke....
Halafu yeye aendelee kutafuta wanawake wengine ili wazidi kumstaheresha, huku akiendelea kujizolea Nuksi, mikosi na mabalaa...
Na ndiyo Maana kuna wanaume ambao wanajua kila mbinu ya kumpata kila aina ya mwanamke wanayemtaka, lakini hawajui kwanini Mungu aliziumba hizi jinsia MBILI tofauti!
Hata hivyo nilipokuwa mbioni kumalizia kuandika KITABU hicho, mmoja wa wafuasi wangu akaja na pendekezo, yeye aliniomba niandike kuhusu suala zima la "utoaji mimba" linalofanywa na baadhi ya wanawake.
Ikabidi nitulize akili zangu ili nifikiri kwa kina! Nilipotuliza akili ndipo sasa nikabaini kuwa wanawake hawa, huwa hawajipi mimba wenyewe, bali kuna wanaume wanaosababisha hizo mimba!
Nikiwa bado katika kufanya tafakari, wazo jingine likanijia tena, wazo hilo lilikuwa kama ifuatavyo:
"kama jamii imeamini kuwa Hakuna mwanaume ambaye hutosheka na mwanamke mmoja na fahari kubwa ya mwanaume ni ngono na wanawake, je, ni kwamba kuna wanawake maalumu wako sehemu fulani ambao hao wanaume hufanya nao starahe?"
Baada ya sekunde kadhaa kupita nikapata jibu, na fahamu zangu zikaniambia kuwa hapana hakuna sehemu maalumu iliyo na hao wanawake, bali ni hawahawa wanawake waliopo kwenye jamii yetu, ndiyo ambao hutumiwa na hao wanaume kama vyombo vya starehe!
Nilipokuwa nikiendelea katika kufanya tafakari juu ya Suala hilo la utoaji mimba, simu yangu iliita!
Imekuwa kawaida yangu huwa sipigiwi simu pasipo kufanya "appointment" nilipoangalia ni nani aliyenipigia, nikaona ni mwanafunzi wangu ambaye huwa namsimamia!
Nilipokea simu yake nikafanya naye mazungumzo mawili matatu, na ifahamike kwamba huyu mwanafunzi wangu ni "single mother".
Katika maongezi yake yeye aliniomba niandike makala kuhusu single mothers, na alitaka aje atengenezee audio kabisa...
Nikamjibu limeisha hilo! Kitaalamu ukiwa mwandishi hutakiwi kuandika jambo pasipo kulifanyia udadisi na utafiti, nikaanza kufanya udadisi.
Nilipozama kwenye kufanya tafakari, ndipo sasa nikabaini kuwa ile imani iliyopo kwenye jamii yangu ya kwamba; "hakuna mwanaume anayetosheka na mwanamke mmoja na fahari kubwa ya mwanaume ni wanawake ndiyo inasababisha hili"
Unatakiwa kujua kwamba imani hii imemfanya mwanaume aingie kwenye mahusiano kwa ajili ya starehe kwa sababu hiyo ndiyo fahari yake kubwa!
Na ifahamike kwamba matokeo halali la tendo la kukutana kimwili kati ya mwanaume na mwanamke ni mimba...
Kwa hiyo mwanaume huyu ataingia ili astarehe, na mimba ikitungwa ataikataa kwa sababu hajafuata kuzalisha au kulea bali kafuata starehe!
Upate kujua mwanaume huyu atakuwa na mtizamo huu si kwa sababu anatakiwa awe na mtizamo huo ila ni kwa sababu ni kitu kinachoaminika na wengi!
Kitakachotokea ni kwamba, mwanaume huyo akiwa anashiriki ataamini kuwa anafanya starehe zake, na akishamaliza atamuacha huyo mwanamke na kwenda kwa mwingine akapate starehe nyingine...
Kwa hiyo basi inapotokea huyu mwanamke kapata mimba, huyo mwanaume ataikataa kwa sababu imani yake kubwa ni kwamba alistarehe, asitambue kuwa ile starehe ndiyo ilipelekea uumbaji, mwisho wa siku endapo huyu mwanamke atazaa na atabaki kuwa "single mother"
Tafadhali usinielewe vibaya sina maana kwamba single mothers wote wanatokana na hii sababu lahasha! Pia wapo wanawake wapumbavu, wasio na akili ambao huvunja mahusiano yao kwa mikono yao wenyewe hali ambayo huwafanya wabaki kuwa "single mothers"
Kumbe sasa tofauti ya mwanamke aliyetoa mimba na single mother haipo. Ukweli ni kwamba huyu mmoja atabaki kuwa "mama wa marehemu" huku mwingine akibaki kuwa mama wa mtoto "pasi na baba".
Turudi kwenye chanzo cha haya mambo mawili, ukweli ni kwamba chanzo cha hayo mambo mawili ni ile imani iliyopo dhidi ya wanaume!
Imani hii imewafanya wanaume wajihesabie haki, kwa hiyo wanaona wao ni Kawaida tu kulala na kila mwanamke kwa minajili ya kupata starehe...
Na ubaya ni kwamba kutokana na ujinga wa kuamini jambo pasipo kudadisi wanaume hao hujifanya hawatambui matokeo yanayotokana na starehe hiyo, badala yake hutambua kuwa wapo pale kufanya starehe...
Ndugu nimekuonesha japo kwa ufupi, jinsi gani imani isiyo kweli huweza kuharibu maisha yako hata maisha ya watu wengine...
Habari njema ni kwamba ipo nafasi yako kabla hujaaminii jambo fulani!
Hivyo basi hutakiwi kuamini kila jambo eti kwa sababu linaaminiwa na wengi! Wewe siyo kama nyumbu wala farasi walio hawana akili! Umepewa utashi na akili timamu!
Je, ni halali Mimi nihalalishe upumbavu wa watu wengi, chini ya mwamvuli wa "wengi wape?". Lahasha! Busara zangu ndogo zimeniambia hapana...
Mimi ndiye yule kijana ambaye huwa naenda kinyume na wengine, yaani wao waki "zigzig" mimi huwa na "zagzag" na wao waki "zagzag" mimi huwa "zigzig"
Kwa huduma ya kubadilishwa kimtizamo na kujengwa upya kimtizamo karibu inbox...
SoMo lijalo litalenga kuhusu uhalisia wa mwanaume na ngono...
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentaship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/06713284339 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment