Hii Ni Kwa Wale Ambao Wameandaa Huduma Au bidhaa Zinazotokana Na Uwezo Wao Lakini Hawajaanza Bado...
Hivi unafahamu kuwa kuna watu ambao wanatambua uwezo wao na pengine labda mara baada ya kugundua hilo, wanatoa mpaka huduma au bidhaa Fulani zinazotokana na uwezo wao lakini hawafahamiki?
Unatakiwa kujua kwamba kutoa huduma fulani au kuuza bidhaa fulani siyo kigezo cha kufanikiwa katika hilo, kama hutajifunza jinsi ya kujitangaza!
Ukweli ni kwamba, unatakiwa ujifunze jinsi ya kujitangaza ili uwafanye watu watambue kwamba kuna huduma au bidhaa unayoizalisha!
Rafiki, unatakiwa uwafanye watu watambue kwamba, hata wewe upo na unatoa huduma au unauza bidhaa Fulani.
Na ifahamike kwamba, kuna kundi kubwa la watu ambalo halijui chochote kile kuhusu wewe, kuhusu bidhaa zako na kuhusu huduma yako.
Hivyo basi ni muhimu kujifunza jinsi ya kujitangaza ili uweze kuwafanya hao watu watambue uwepo wako pamoja na uwepo wa bidhaa zako na huduma yako!
Na, moja ya mbinu rahisi ya kujitangaza ni kupitia kuwazoesha tu watu, kwa maana wanadamu huzoeshwa. Kwa mfano nilivyoanza kuishi career yangu ya uandishi, ushauri , usimamizi na uelimishaji nilianza kwa kuwazoesha kwanza watu, na mpaka sasa watu wananifahamu mimi ni nani!
Kwa kusema hivyo huna budi ujitangaze ili uwafanye watu watambue kuhusu uwepo bidhaa yako, huduma yako pamoja na umuhimu wa bidhaa au huduma yako maishani mwao.
Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya watu huwa hawatambui kwamba kuna tatizo, na kwa vile huduma au bidhaa hutolewa kwa minajili ya kutatua tatizo, basi wajibu wako ni kuwafanya hao watu watambue kuwa kuna tatizo.
Baada ya hayo huna budi upendekeze bidhaa yako ama huduma yako kama mbinu ya kutatua tatizo hilo.
Rafiki unatakiwa kujua kwamba:
Bidhaa nzuri + kutokufahamika = mauzo mabaya
Bidhaa mbaya + kufahamika = mauzo ya wastani
Bidhaa nzuri + kufahamika = mauzo ya ajabu...
Una kila sababu ya kuwafanya watu watambue kwamba wewe upo na unatatua tatizo Fulani lililopo maishani mwao ili kuwarahisishia maisha yao!
Hata hivyo kuna mbinu nyingi sana za kujitangaza, mbinu ya kwanza ni kupitia kutumia mitandao ya kijamii ambapo unaweza ukaposti bidhaa zako au kuandaa maudhui mbalimbali kwa minajili ya kuwafanya watu watambue kile unachokifanya!
Hata hivyo unaweza ukafanya matangazo ya kulipia kwa njia ya Instagram, facebook ikiwa ni pamoja na kujitangaza kwenye vyombo mbalimbali vya Habari kama vile: magazeti, redio na televisheni.
Rafiki haijalishi itakuwaje lakini hakikisha kuwa huduma yako na bidhaa yako inafahamika kwa watu! Jitangaze! Jitangaze! Jitangaze!
Hakikisha jina lako linafahamika na wengi, kwa sababu watu huuza zaidi kupitia majina yao na siyo bidhaa/huduma hakikisha huduma yako inakuwa maarufu na inawafikia wengi!
Jifunze kujitangaza kwa maana huduma au bidhaa inayofahamika na wengi huwa na mauzo mengi!
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentaship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment