Je, Ulishwahi Kujiuliza Kwanini Wanaume Wengi Huhalalisha Ngono? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...
Si mbaya endapo nitaanza na usemi usemao; “kila kitu hutokea kutokana na sababu”.
Hii ni sawa na kusema kuwa, "hakuna mwanaume hata mmoja ambaye huhalalisha kuwa ngono ni kila kitu kwake na hawezi kutosheka na mwanamke mmoja bila sababu iliyopelekea awe na mtizamo huo."
Na ukifuatilia takwimu za duniani kote utabaini kuwa, sehemu kubwa ya dunia ni kama imehalalisha kuwa mwanaume anastahili alale na kila mwanamke atakayekatiza mbele yake, amsaliti hata mke/mwenzi wake na afanye ngono kila anapotaka na kwa kila mwanamke atakayemtaka!
Jambo hili limehalalishwa tu na watu wamelipokea na kuliamini chini ya mwamvuli wa "wengi Wape" lakini ukifanya uchanganuzi yakinifu utagundua kwamba siyo kweli!
Bila kukupotezea muda ngoja nikakusogeze kwenye sababu ambazo huwafanya wanaume wengi wawe na mtizamo huo:-
1. Nadharia Ya Kibaiolojia
Huungwa mkono na tafiti za kisayansi. Nadharia hii hudai kuwa mwanaume huchochewa kufanya ngono kwa sababu ya maumbile yake ya uzazi yalivyo.
Hali hii huchangiwa na homoni ya tesistosteroni kuzalisha kiwango kingi cha mbegu za uzazi za kiume!
Na mbegu hizo za uzazi za kiume zikishazalishwa huhitaji kutoka. Na, katika harakati za kutaka kutoka huamsha hisia kwa mwanaume na kufanya kiungo cha uzazi wa mwanaume kusimama.
Mchocheo huo wa hisia ndiyo humfanya mwanaume huyo atafute njia mbadala ya kuzipunguza.
Kutokana na hilo hujikuta akisukumwa atafute mwanamke ambaye anaweza akampa ngono, ili afanikishe azima yake. Na, endapo itashindikana mwanaume huyo anaweza hata akajichua yaani kujichukulia sheria mkononi!
Na, ndiyo maana wanaume wengi ambao siyo watu wa wanawake sana hujikuta wakidumbukia kwenye kundi la kupiga punyeto, kama njia ya kupunguza mbegu za uzazi za kiume, lakini hili hutokea endapo watashindwa kujizuia!
Sina maaana kwamba wanaume wote huhitaji ngono au hupiga punyeto lahasha! Lakini, wale walio wafuasi wa nadharia hii hudumbukia humo.
Wale wasio wafuasi wa nadharia hii kama mimi hawapo kwenye kundi lolote lile kati ya hayo makundi tajwa!
Unatakiwa kujua kwamba, pindi mwanaume akifanikiwa kupunguza mbegu zake za uzazi kwa njia yoyote ile, kitakachotokea ni kwamba, homoni ya tesistosteroni itazidisha kiwango cha uzalishaji wa mbegu hizo za uzazi mara mbili Zaidi ya kile kilichokuwa kimezalishwa hapo awali kabla hazijatoka!
Kwa kusema hivyo mwanaume huyo atachochewa ahitaji ngono mara mbili Zaidi ya vile alivyokuwa akihitaji mara ya kwanza!
Na endapo hali hii itadumu kwa muda mrefu basi mwanaume huyo atajitengenezea mpaka tabia na kuanza kuona kuwa ngono ni kila kitu kwake.
Na ndiyo maana hata kwenye ndoa, tendo la ndoa kwa mwanaume ni hitaji na si upendo bali kwa mwanamke tendo la ndoa ni tendo linaloashiria upendo.
Na, endapo mwanaume huyo atakuwa kaanza kujichukulia sheria mkononi yaani kujichua atasukumwa awe anafanya hivyo kila siku, matokeo yake hujikuta ameshakuwa mraibu, nikiimaanisha kuwa, atajikuta akianza kutegemea nyeto ili ajisikie vizuri au ili Siku yake iende vizuri, na endapo hatafanya hivyo, basi huiona siku yake kana kwamba imekuwa ndefu sana.
Matokeo yake kila wakati atajikuta akifanya hivyo kwa kisingizio eti mbegu zake za uzazi zinataka kutoka.
Unatakiwa kujua kwamba nadharia hii imetengeneza makundi mawili ya wanaume yaani: wale wanaoendekeza ngono na wale wanaoendekeza nyeto.
Hawa wote wameshindwa kutumia akili, badala yake sasa wanatumia mihemko ya mwili iwaongoze.
Sasa kama umepewa akili maana yake ni nini? Ngoja nikusaidie kujibu... Umepewa akili ili zikusaidie kutawala mihemko ya mwili wako!
Hata hivyo, binafsi huwa siamini katika nadharia hii kwa sababu nina akili. Na ifahamike kwamba siyo kile mwenye akili ana akili, ukitaka kuthibisha hili angalia matendo ambayo hufanywa na hao watu waliosoma ambao ninyi mnawaona kana kwamba wana akili... ukishachunguza utaujua uhalisia wa hoja yangu...
Unatakiwa kujua kwamba, usipoandaa mazingira ya kumwaga mbegu zako za uzazi, huwezi kumwaga. Kwa kusema hivyo tumia akili zako ili ushinde mihemko.
Najua umeaminishwa kuwa mwanaume asipofanya mapenzi kwa kipindi kirefu akili yake hushuka na kiwango chake cha ufahamu hupungua. Na hata akili zake haziwezi kufanya kazi vizuri!
Rafiki chanzo cha busara na akili ni Mungu na siyo ngono kama wengi mnavyodhani. Mithali 8:23-31. Sunaona mimi mwenyewe nilivyo na akili hadi zinakujenga kimawazo.
Je, wewe uliyeaminishwa na kuamini hilo umepata akili na fahamu za kuyajua haya yote? Bila shaka ni Hapana! Au tuseme Mimi nina kipaji Cha uandishi? Jibu ni hapana ☺️
Hata mfalme Suleimani ambaye ndiyo "role model" wenu mkubwa aligeuzwa moyo na wanawake mpaka akili zake na hekima zake zote zikapotea. 1 Wafalme 11:1-8
Unatakiwa kujua kwamba endapo ngono ingekuwa huleta akili basi Suleimani angeongezeka kiakili.
Na andiko linasema; Mungu ndiye aliyempa Suleimani akili. 1 Wafalme 3:11.
Ndugu mwanaume usidanganyike, ngono haileti akili! Ushauri wangu kwako, dear brother!
Kama ni wakati muafaka wa wewe kufanya hivyo, huna budi kutafuta kashemu kamoja hivi kazuri kazuri halafu ishi nako na siyo kujitwalia kila mwanamke anayekatiza mbele zako!
Pia, usidanganyike na msemo wa wahenga kuwa uzuri wa mwanamke siyo urembo. Upate kujua kwamba mwanamke siyo kiumbe cha rohoni, bali ni kiumbe kinachoonekana, kwa hiyo hakikisha anaonekana vizuri machoni pako!
Na ifahamike kwamba kuna mwanamke mwanamke asiye mrembo mwenye tabia mbovu, kuna mwanamke mrembo mwenye tabia mbovu, kuna mwanamke asiye mrembo mwenye tabia nzuri na kuna mwanamke mrembo mwenye tabia nzuri vilevile!
Ili kuepuka tamaa ya kutamani kila mwanamke, nakushauri utafute mwanamke aliyakamilika karibu kwenye kila idara japo huwezi kumpata mwanamke aliyakamilika kwa asilimia zote labda uumbe wakwako, kwa maana kuna baadhi ya wanaume huendekeza ngono kwa sababu wanamiliki wanawake wasiowavutia!
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!
Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentaship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment